Mwanamke mfupi mwembaba vs mrefu mnene
Kwenye suala na mahusiano hasa ya kwenye ndoa ni muhimu kujua hili ili kuepuka matatizo ambayo hayana ulazima
Kuna ka utafiti kamefanyika ambako sio rasmi sana kihivyo lakini kanaweza kuwasaidia watu kupata baadhi ya majibu ya maswali waliyokuwa wanajiuliza siku nyingi
Najua kuwa yameshawahi kusemwa mengi sana kuhusiana na maumbile ya mwili lakini sidhani kama yamewahi kuongelewa kwa namna ambayo nakwenda kuzungumzia
Yaliyoongelewa nadhani ni yale ambayo yanahusu kwenye kitanda zaidi kuliko kwenye mambo mengine,mimi nitakwenda kuzungumzia kwenye mambo mengine zaidi tofauti na kitandani
Matokeo ya ka utafiti hako yanasema kuwa mwanamke ambae ni mfupu halafu mwembamba mara nyingi anakuwa na tabia zinazoweza kusababishwa na umbo lake hili
Baadhi ya tabia ambazo mwanamke anakuwa nazo mwenye umbo hilo ni kama ifuatavyo
Msemaji sana
Inasemekana uwa mwanamke ambae ni mfupi na mwembamba anakuwa ni mwepesi sana kwenye mdomokitendo ambacho wanaume wengi hawakipendi kwani wanaume wameumbwa kusema machache na wasingependa sana kubishiwa hasa kwa sauti kubwa
Mwanamke ambae ana umbo la namna hii inaonekana ni mwongeaji sana na sio anaekubali kushindwa mara nyingi,kitendo hicho kinamfanya aonekane mkorofi sana hivyo kumfanya asiweze kupata baadhi ya fursa nyingi
Tabia hii inaelezwa na baadhi ya wanasaikolojia kuwa inasababishwa na na kitendo cha mwanamke huyo kutokujiamini kulikosababishwa na kutokujikubali kwa namna alivyo kwani jamii nyingi zinamchukulia mwanamke mfupi kama "asiefaa" hivyo kumpa wakati mgumu sana kujikubali kitendo ambacho yeye anamuangalia kila anaejaribu kutokukubaliana nae kwenye jambo fulani kuona kama anamnyanyapa
Mwanamke ambae ni mfupi na mwembamba inadaiwa kuwa na ka tabia ka kupenda kutembea sana,hii nayo ni aina ya tabia ambayo baadhi ya watafiti wanasema kuwa inasababishwa na umbo la mhusika,watafiti hao wanasema kuwa mwanamke ambao ni mnene au mwenye umbo ambalo linakaribia unene ni mvivu sana kutembea na hata kuongea sana,jambo hilo linawafanya waonekane kama wanaofaa sana kuolewa lakini hilo ni tofauti kwa hawa wa umbo la ufupi na wembamba
Miili ya hawa wembamba na wafupi inaonekana kama ni sababu tosha ambayo inaweza kuwafanya wakawa na hiyo tabia japokuwa inasemwa kuwa malezi nayo yanachangia kwa kiwango kikubwa sana
Tabia hiyo imekuwa ikiwafanya wanawake hao kuonekana kama wasioweza kuwa wake wanaofaa sana kwani hakuna mwanaume atataka kuingia kwenye ndoa na mwanamke wa aina hiyo kwani haipendezi
Kwa uchache ni hizo na ngoja niishie hapo kwani mada itakuwa ndefu sana na kuwachosha wasomaji lakini kuna sifa nyingi sana ambazo zinawahusu hawa wanawake wa aina hii,sifa ambazo zinaonekana ni kikwazo kwao kwenye mahusiano ya kindoa
Lakini pamoja na hayo hii haina maana kuwa kila mwanamke mwembamba na mfupi anaingia kwenye kundi hili lakini wengi wao wako hivyo!
No comments: