Jinsi ya kupata mtoto wa kiume
Uzazi wa mpango ni jumla ya vitu vingi sana
Uzazi wa mpango hauhusu kuzuia kupata ujauzito tu bali hata kupangilia idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi wa mpango..
Wanandoa wengi wamekua wakitamani kupata jinsia flani za watoto ili wapate watoto wachache.
Hata hivyo wakati mwingine inatokea wanapata watoto wa jinsia moja tu ya kike na hivyo hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika yaani mtoto wa kiume.
Zipo familia ambazo hufikia hadi kugombana na kutengana kwa sababu hii.
Baadhi ya kabila na koo za watu upande wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa inapotokea mama anazaa watoto wa kike tu.
Kwenye makala hii naenda kumaliza kitendawili hiki kwa kukueleza njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi.
Endelea kusoma …
Kisayansi mbegu zinazotoa mtoto wa kiume zinaitwa XY.
Mbegu hizi zinapotoka kwa mwanaume huenda kwa mwendo wa kasi sanakwenda kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke lakini shida kubwa ni kuwa mbegu hizi XY hufa haraka SANA zikiwa njiani.
Wakati mbegu zinazotoa mtoto wa kike zinaitwa XX.
Mbegu hizi husafiri taratibu na huchelewa kufika ndani ya mfuko wa uzazi. Kwakuwa mbegu hizi yaani XX huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.
Kwahiyo namna pekee ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume ni kuhakikisha mbegu za kiume XY zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla hazijafa ….
Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume:
1. Shiriki tendo la ndoa siku mayai ya mkeo yanapokua yameshuka
Unaposhiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka (ovulation day) mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike na kuunda ujauzito.
Kwa kawaida huwa ni siku ya 14 kabla ya kuona damu ya mwezi unaofuata na siyo baada ya kuona siku zako.
Ikiwa wewe mwanamke huifahamu siku yai linapokuwa limeshuka basi tumia ishara ya kuongezeka kwa joto mwilini mwako.
Pima joto la mwili wako. Nunua kifaa cha kupimia joto (thermometer) na ujipime joto la mwili wako kila siku asubuhi.
Siku ukipima ukaona joto limeongezeka kidogo basi ujue yai limeshuka (ovulation day) na hiyo ndio siku hasa ya kutafuta mtoto wa kiume.
Pia angalia maji maji ya uke. Shika maji maji ya uke wako na kwa kawaida siku yai likiwa limeshuka utaona maji ya uke kuwa ni mazito na yanavutika kama maji ya mayai mabichi.
2. Mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako
Mwanaume unatakiwa uongeze wingi wa mbegu zako (sperm count). Hili linawezekana hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati ukisubiri mke aanze kuona yai linashuka (ovulation day).
Pia hakikisha hauvai nguo za kubana sana na usikae mazingira ya joto sana.
Kwa kawaida korodani zinatengeneza mbegu nyingi zaidi wakati wa hali ya ubaridi kuliko kwenye joto hivyo mwanaume unatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, acha kuweka laptop kwenye mapaja, acha kuvuta sigara na kunywa pombe.
Wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara wanapata tatizo la kuwa na mbegu chache na mbegu kidogo sawa sawa na wavutaji wa bangi na watumia madawa mengine ya kulevya.
Pia ikiwa mwanaume anatumia dawa za kutibu saratani pia husababisha uzalishaji wa mbegu kuwa mdogo.
3. Tumia staili za tendo la ndoa ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa
Staili hizi huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume yaani XY kufika haraka na kufanya utungwaji wa mimba kuwa rahisi.
Unahitaji utumie staili ambazo zinawezesha mwingiliano mkubwa (deep penetration) na hii ni mhimu hasa kama wewe mwanaume una kibamia.
Wakati unapotumia staili za mwingiliano mdogo (shallow penetration) husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi na hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike (XX) kutungisha ujauzito na hapo anatokea mtoto wa kike.
4. Hakikisha mwanamke anafika kileleni kwanza
Wakati wa tendo la ndoa mwanaume hakikisha mkeo anafika kileleni kwanza kabla ya wewe.
Mwanamke anapofika kileleni huwa anatoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo huwa haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.
Sasa mwanaume utahitaji kuchelewa kufika kileleni lakini uonapo tu mama amefika kileelni basi na wewe ufike muda huo kabla hakujakauka. Namna rahisi kama wewe ni mtu wa kukojoa haraka ni kumnyonya kinembe mama kwa dakika kadhaa na hatachelewa kufika kileleni.
Hapa nguvu za kiume zinahitajika sana. Pia ni mhimu mwanaume uzifahamu dalili za mwanamke anapofika kileleni huwa anakuwaje.
5. Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya yai kushuka
Kabla ya siku yai kushuka (ovulation day) kawaida mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi kama kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya siku hii kupita.
Tumia kila mbinu kila elimu kuhakikisha unaifahamu siku hii yai linaposhuka kwani ndiyo siku pekee yenye uhakika wa kutungisha mtoto wa jinsia ya kiume.
6. Mwanamke aepuke vyakula na vinywaji vyenye asidi
Mwanamke anatakiwa kwa kipindi kirefu ale vyakula na anywe vinywaji visivyo na asidi (tindikali).
Vitu vinavyoongeza asidi mwilini ni pamoja na vyakula vya kusisimua (spiced foods), vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, pombe, chai ya rangi, kahawa, baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, maziwa na bidhaa zingine zitokakanazo na maziwa n.k.
Vyakula visivyo na asidi nyingi ni pamoja na matunda, mboga za majani, maji ya kunywa, mbegu mbegu (za karanga, za ufuta, korosho, za maboga nk), apendelee kula uyoga pia.
Mwisho wa siku usiache kumuomba Mungu kwani yeye ndiye muweza wa yote.
0765203999
No comments: