MAMBO 10 YA KUMWAMBIA MKE, MUME, MPENZI, KILA SIKU.
Wale wenzetu katika mahusiano tunafahamu kuwa usimchukulie mtu kawaida kwa sababu umempata, au kwa kujihakikishia.
Kuwa na muda wa kushirikishana maneno ya mawazo kila siku inasaidia kukomaza na kutunza mahusiano yetu yawe na nguvu. Na hapo kuna mambo 10 ya kumwambia mwenza wako kwa misingi mizuru iliopo.
”Nakuamini”( i trust you)
Imani ni kiungo kikubwa katika mahusiano yote, na inaleta hisia kwa mwenza wako kukuona kuwa ni mtu mkweli.inawafanya kufahamu kwamba unajisikia kuwepo kwenye sehemu salama kwao na utawatia moyo kufanya kazi kwa bidii ili kutunza imani.
”I miss you”
Hata kama mnaishi mbali kwa sababu maalumu , labda kikazi au hata kwa mambo mengine ya msingi, mbali kila mmoja kwa siku kadhaa, Au hamjapata muda wa kutosha kuongea kwa karibu kama mlivyozoea, haya maneno madogo yanaweza yakaokoa kumbukumbu kubwa kwa mwenza wako kwamba unamthamini, na unathamini uwepo wake katika maisha yako.
”I’m sorry”
Haya maneno madogo mawili yana nguvu ya kutunza mahusiano kwa kadri yanavyoendelea, hata kwenye nyakati ngumu.Kama unahitaji kuwa na furaha na mwenza wako, uwe na hekima ya kukumbuka kwamba ni muhimu kuwa kamili kuliko kuwa na neno la mwisho. vitu vidogo vidogo vinaharibu hali ya hewa ya mahusiano. kwa hio jifunze kitu kinachostahili kuongea na mwenza wako na uwe mwepesi wa kuachilia.
”Nakuheshimu”
Fanya kitu ambacho mwenza wako atafahamu kuwa unamthamini , sio kwa mwonekano wake, kazi yake, au vitu vingine vya kuvutia .Wakati wanapofanya maamuzi magumu, kukamilisha malengo au ufahamu wa mawazo kwenye complex subject, waambie jinsi gani unawaheshimu katika maamuzi hayo, na tabia zao .
”You look great”
Hata kama siku zote anapendeza na kuonekana Smart katika mwonekano wake , wanakuwa bado wanapenda kusikia maneno yako , mwambie umetokelezea, na ya kuwa anavutia. usiache nafasi hio akaseme mwingine nje. utamboreshea self-esteem yake kila mara unapomwambia jinsi gani anaonekana smart kwa kila kitu. na mwambie kuwa unajisikia vizuri kuwa nae.
”Nashukuru kuwa na wewe maishani mwangu”
Ni kitu gani mwenza wako anachokuletea? care, affection, friendship, advice, good time? kama uko kwenye mahusiano mazuri yenye afya, watakuletea vitu hivyo hapo juu vyote na zaidi ya hivyo! waonyeshe tu ni jinsi gani unajisikia unapokuwa na wao.
”I will always support you”
Kama binadamu, mwenza wako ana kuwa anapita kwenye changamoto fulani, na atakutazama wewe kwa ajili ya msaada. wahakikishie kwamba utakuwepo muda wote kwa ajili yao wakati mamboyanapokuwa magumu, na watajisikia kutiwa moyo kwa ajili ya kukimbiza ndoto zao, kwa kufahamu uko upande wao.
”I appreciate you”
Watu wote wanapenda kuhisi kuwa wanathaminiwa kama tulivyo binadamu , na kama tulivyoweza kuwa na mahusiano Ulimwenguni. kumwambia mwenza wako kuwa unakubaliana nae, unampa nguvu na unamtia moyo kuendelea kuhifadhi katika mahusiano yenu.
”Let’s go to….”
Mara nyingi mahusiano hufikia mwisho kwa sababu ya kufikiria kuwa uchangamfu umekwisha. marahatua ya honey moon inapopita, endelea kuwasha moto kwa kushauri kwenda sehemu nyingine mpya na kazi mpya nyingine ili kujaribu. hii itapelekea ishara ilio wazi kwa mwenza wako kuwa unamthamini na unahitaji kuwa pamoja.
”I love you”– SEMA NAKUPENDA.
Kila siku sema hivyo, nakupenda. Matendo huongea zaidi kuliko maneno unapotaka kuonyesha kujali na kuwa unamwitaji. Lakini maneno pia huleta hisia nzuri. hata kama mko pamoja kwa kipindi cha miezi michache au miaka mingi, mwenza wako mara zote atakuwa anakubaliana na hilo na kuheshimu kiasi hicho unachomwambia. kusikia maneno ya mapenzi kutoka kwa mwenza yanaweza kufanya siku mbaya kwenda kwa urahisi.
No comments: