Tendo la Ndoa Linavyosumbua Wengi

Tendo la ndoa ni inshu inayosumbua sana wanaume na wanawake katika ndoa.
   


Mwanamke katika ndoa huhitaji urafiki na upendo ili ajihusishe na tendo la ndoa wakati mwanaume anahitaji tendo la ndoa na hana mpango na masuala ya urafiki na upendo tu.


Wapo wanawake ambao piga ua wamejipangia kwamba bila kuwa karibu na mimi kimapenzi sahau kuhusu Mapenzi kwani ni kama kuutumia mwili wangu.


Ukweli unaouma ni kwamba wanaume wengi wanaotoka nje ya ndoa (cheat, chepuka) hufanya hivyo kwa sababu wananyimwa katika ndoa zao.

Mwanaume anayetoka nje mara zote ndiye anayebeba lawama na dhambi.

Yeye ndiye mhanga wa tatizo zima hata kama mke wake alihusika katika kutengeneza mazingira ya mwanaume kuchepuka.


Mwanamke huhitaji upendo ili kujisikia vizuri kihisia na mwanaume naye huhitaji heshima kwa mke kutii hitaji lake la mwili  ili kujisikia yupo mke anamtii.


Wapo wanaume ambao kwa kunyimwa hitaji lao la msingi la tendo la ndoa ndani ya ndoa zao huwa hawaoni shida au tatizo kupoteza familia, uongozi, hadhi , uhusiano na Mungu wake au kuaminiwa na jamii kwa kwenda kutimiziwa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.

Inaweza kuwa bado hujanielewa naongea kitu gani hata hivyo umeshaona wanaume wanatoka na kuacha wake zao wazuri na kwenda kutembea na wanawake ovyo ambao kila mtu hushangaa na ni wanaume wazito na wanaoheshimika kwenye jamii.

Ukweli ni kwamba hitaji la tendo la ndoa kwa mwanaume ni kubwa kuliko unavyofikiria.


Inawezekana wewe ni mwanamke ambae mume wako ni mtumishi wa Mungu au mume wako ana cheo au wadhifa au anapenda sana familia na kwa kuwa siku za karibuni umeoana hakutumizii hitaji lako la kupendwa basi na wewe umeamua kumnyima tendo la ndoa hadi abadilike ndipo na wewe umpe mwili wako kwani una amini kwa namna alivyo hawezi kutoka!

Unajidanganya!

Hujasikia watumishi wa Mungu ambao wameanguka?

Hata kama huna mood kinakushinda nini kutumia dakika tano tu kumpa hitaji lake na awe happy na wewe muda wote?


Katika kushauriana na wanawake wengi ambao waume zao hutoka nje wengi huruka na kukiri kwamba wanaume zao ni tamaa na shetani ndo amewatuma kufanya vitu kama hivyo hata hivyo mwanamke mmoja alikiri kwamba ni kweli anajisikia vibaya sana kwamba alihusika katika kusababisha mume wake kutoka nje kwani yeye alikuwa anajihusisha sana na watoto wake na kazi na hakupenda kabisa kumpa Te ndo la Ndoa mume wake kwa muda mrefu.


Mume mmoja alilalamika kwamba:

“Ni kweli simlaumu mke wangu kwa mimi kutoka nje ila hawezi kutoka msafi katika hili kwani alinifanya kujiona mimi ni failure wa kila kitu nyumbani mwetu na sikuruhusiwa hata kumgusa miezi na miezi.

Kama angenitii na kunipa hitaji langu la Tendo la Ndoa basi nisingetoka kwani mwanamke niliyetembea naye alinifanya nikajisikia vizuri muda wote na kila alivyozidi kuniambia mimi ni mwanaume mzuri nilizidi kuwa karibu na huyo mwanamke na sikuwa na lengo la Tendo la Ndoa ila kutokana na heshima aliyonipa ilifika mahali nikaamua kutembea naye hata kama sura na umbo lake ni kama sokwe"


Mwanaume anahitaji mapenzi kama mwanamke anavyohitaji kihisia.

Bila tendo la ndoa mwanaume hujiona hujamtii au kumpa heshima na moja kwa moja huanza kuwa na tabia zisizo za upendo kwa mwanamke.

Wanawake wengi huwa na ndoto za kuhakikisha baada ya kuolewa mahitaji yao ya hisia yanatimizwa na waume zao hata hivyo wao wenyewe hujisahau kuwapa waume zao mahitaji yao ya tendo la ndoa na automatically inakuwa ngumu kwa mwanamke mwenyewe kutimiziwa mahitaji yake ya emotions.


Namna mwanaume aliumbwa ni tofauti na mwanamke ndiyo sababu mwanaume anapenda tendo la ndoa na linampa kulizika ambako humfanya kukumchangamkia na kuchakarika kuhakikisha na yeye anamtimizia aliyemtimizia.



Wewe mwanamke unapenda tendo la ndoa pale mwanaume anapokuwa karibu kimapenzi na wewe hata hivyo kwa mwanaume ni kinyume, tendo la ndoa ndilo humfanya mwanaume kuwa karibu na mwanamke. 

No comments:

Powered by Blogger.