Tendo la Ndoa Wakati wa Ujauzito
Wakati wa ujauzito wanawake wengi hukosa hamu ya tendo la ndoa hivyo mwanaume unahitaji kuwa na mawasiliano mazuri ili mambo yaende vizuri sio wote ila wengi wao huwa hivyo.
Je, Mwanamke mwenye ujauzito anaweza kuendelea na tendo la ndoa?
Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kwamba tendo la ndoa kwa mwanamke mwenye mimba ya hatua yoyote ya ujauzito inaweza kumuathiri mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni.
Hata kama kunatokea miscarriage bado sayansi inathibitisha kwamba chanzo huwa si sababu ya tendo la ndoa wakati mwanamke ana ujauzito, bali sababu zingine kabisa.
Tafiti nyingi zimefanywa kwa kufuatilia wanawake ambao waliendelea na tendo la ndoa huku wakifika kileleni na wale ambao hawakuwa wanafika kileleni wakati wa tendo la ndoa, na wale ambao hawakufanya kabisa tendo la ndoa muda wote wa ujauzito.
Matokeo yalionesha kwamba wanawake wote walizaa watoto ambao hawana tofauti yoyote kiafya.
Hivyo tendo la ndoa ni salama kabisa muda wote wa ujauzito.
Je, ni wakati gani huruhusiwi tendo la ndoa wakati wa ujauzito?
Ni pale tu mwanamke anapojisikia kutokwa na damu au maumivu yoyote au leakage ya majimaji.
Mwanamke mwenye ujauzito haruhusiwi kuingiza upepo kwenye K yake kwani husababisha ambacho kinaweza kusababisha kifo kwa mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni kwani hu-block mishipa ya damu. Wapo wanaume huwa na mchezo wa kubusu huku wanapuliza huko bondeni kabla ya kuanza Mchezo.
Pia kama mmoja ya wanandoa ana magonjwa ya zinaa (STD) haruhusiwi tendo la ndoa hadi daktari athibitishe kwamba amepona ama sivyo anaweza kusababisha mtoto tumboni aambukizwe.
Pia ifahamike kwamba si wanawake wote wakiwa na ujauzito hupenda tendo la ndoa wengine huwa hawapendi kabisa.
Utafiti unaonesha pia kwamba mwanamke mwenye ujauzito hukosa hamu ya tendo la ndoa miezi mitatu (3) ya kwanza, kisha hupenda sana tendo la ndoa miezi mitatu inayofuata na Pia miezi mitatu ya mwisho hukosa tena hamu ya tendo la ndoa kwa sababu ya saikolojia ya kusubiri mtoto kuzaliwa.
Ingawa uzoefu unaonesha kwamba mwanamke mwenye ujauzito husisimka haraka na kufika kileleni mapema sana kwa sababu damu huwa nyingi sana kuzunguka K na hivyo kuwa na hisia zaidi kuliko akiwa hana ujauzito, pia ni dhahiri kwamba mwanamke anayefurahia tendo la ndoa wakati ana ujauzito hupata utamu wa uhakika.
Kitu cha msingi pia ni kuzingatia mikao au milalo wakati wa tendo la ndoa kwani mwanamke mwenye ujauzito anahitaji mikao au milalo ambayo haikandamizi tumbo lake.
Hakikisha mnakuwa na mawasiliano mazuri kuhusiana na suala la tendo la ndoa ili kila mmoja aweze kuwa msaada kwa mwenzake.


No comments: