Nini cha kufanya mke wa jirani anapozoea kukuomba pesa?

Wakuu hii ni miongoni mwa changamoto inayonikabili hapa nilipopanga.
Ni hivi miongoni mwa wapangaji wenzangu yupo jamaa mmoja ana mke na mtoto mmoja lakin jamaa mara nyingi hayupo maana anajiendeleza kielim mjini ( Twaish wilayani).
Jamaa ni mtumishi wa umma mkewe ni mama wa nyumban mwenye kama miaka 23-25 na jamaa ake huja mara moja moja weekend.

Ninachoomba ushaur ni huyu mke wa jamaa ana tabia ya kuniomba omba vihela mata ya juis mara ya soda n.k. mimi sijaajiliwa ni mtu wa mishe za kuzugia kupata mkate wa kila siku. Sasa wakuu sielew huyu manzi nakabiliana naye vip au anaweza kuwa na nia gani hasa na je nikiendelea kumtimizia maombi yake haya kuna ubaya gani?

No comments:

Powered by Blogger.