HIZI HAPA DALILI KUMI ZA KUONYESHA MUWA WAKO WALIWA NA MABAZAZI
MARA nyingi tumekuwa tukizungumza jinsi ya kumtambua mume au mwanamume anayesaliti.
Lakini dunia siku hizi imeharibika, wanawake nao wamekuwa hodari wa kusaliti ndoa zao au mapenzi yao na wanaume hushindwa kuwagundua kwa sababu mara nyingi akina dada ni wataalam wa kuficha hisia zao.
Unaweza ukaona anakuchekea, anakupa huduma zote muhimu, anakuheshimu na hata kunyenyekea. Pamoja na yote hayo usishangae sana utakapogundua muwa wako unafyonzwa na mabazazi wasiokuwa na simile.
Katika mazingira haya utajuaje kama anakusaliti? Zifuatazo ni baadhi ya dalili ambazo mkeo ama mpenzi wako msichana akianza kuonekana nazo huenda hali sio shwari:
1. Haonyeshi mapenzi tena anapokuwa nawe
Wanawake hufanana katika kupenda, akimpenda mwanaume siyo rahisi kuficha hisia zake kwani huonyesha hata pale anapokuwa na mpenzi wake kwa kumjali kumfanyia utundu wa hapa na pale.
Hata kutamani kuwa nawe kila wakati ni dalili mojawapo ya kukuonyesha mapenzi, lakini ukimuona mwanamke wako hana ukaribu nawe tena, wala hajali uwepo au usiwepo, basi huenda kuna jambo.
2. Anapoteza mhemko faragha
Mwanamke anapokuwa na mpenzi wake faragha huwa na mhemko wa ziada, lakini ukiona amepoteza hali hiyo na hata ukiwa naye haonyeshi kufurahia, hii ni wazi kuwa ana mwanaume mwingine ambaye anaweza kumpa furaha hiyo.
3. Anaepuka kujifunga kwako
Hasa ikiwa bado hajafunga ndoa. Kwani kuna baadhi ya akina dada huwa na matarajio ya kupata mume. Na atakuwa karibu nawe na hata kukusaidia majukumu mengine ya nyumbani kwako, aidha akufulie, akupikie na hata akusafishie nyumba yako. Lakini ukimuona mwanamke anaepuka kujifunga kwako, yale aliyokuwa akiyatenda aidha ameyapunguza ama kuyaondoa kabisa, basi huenda chombo kimeenda mrama.
4. Muda wote ana shughuli binafsi
Unaweza kuwa unataka kumpeleka sehemu kwa maongezi, ukimtaka mtoke atakwambia ana shughuli zake. Ukijaribu kumtumia ujumbe aidha sms au whatsapp anakujibu baadaye sana au asikujibu kabisa. Ukimpigia hapokei, anakuja kukupigia baadaye na kukuambia alikuwa amebanwa na shughuli.
5. Usiri wa kupitiliza
Ukiona mwanamke anakuwa msiri sana hata kwa vitu ambavyo alikuwa akikushirikisha moja kwa moja, jua tu huna nafasi tena kwake.
6. Kuwa makini zaidi na mwonekano wake
Mwanamke hupendelea kuonekana amependeza hasa anapojua atakutana na mpenzi wake au anapokuwa anatoka na mpenzi wake.
Ukiona mkeo au mpenzi wako anavaa ovyo mkiwa mnatoka wote na akivaa vizuri ni pale anapotoka mwenyewe au na marafiki zake, wewe elewa tu kuwa anamvalia mwenzako.
7. Simu yake anaweka neno siri
Mwanamke akikupenda huwa wazi kwa vitu vyake binafsi ikiwemo simu ya mkononi. Ukiona mwanamke wako ameanza tabia ya kuweka neno siri kwenye simu na kujificha pale anapoongea ama kuacha kupokea baadhi ya simu ukiwa naye, elewa kuna mwanaume amevuruga hisia zake.
8. Anakwepa maswali
Wanawake wengi hushindwa kuficha jambo kwa maana ni wakweli, ukitaka kumtega mhoji maswali mengi utamkamata kiurahisi, sasa ili kujiondoa kwenye kumjua atajitahidi kukwepa maswali.
Ukijaribu kumbana kwa maswali mengi huku ukimuangalia usoni utaona jinsi atakavyokuwa mkali na majibu yake yatakuwa ni ya wasiwasi.
9. Malalamiko yanazidi
Iwapo utabaini malalamiko ya mpenzi wako kila siku hayana ukweli, jua moja kwa moja anatafuta njia ya kutokea. Huenda amepata mwanaume mpya hivyo anashindwa kukwambia zaidi ya kukulalamikia ili hata akienda kwa huyo mwingine ujihisi ulimkosea.
10. Usipomtafuta hakuulizi
Mwanamke ukimkalia kimya kwa siku nzima bila kuongea naye au kumjulia hali kama ni mpenzi wako kweli au mumeo, huwa anaumia lakini ukiona anaona sawa na kukaa kimya ujue ndege wako ameruka.
from Tujifunze Mapenzi https://ift.tt/2rqGyk6
via
No comments: