Jinsi Ya Kutambua Kama Mwanamke Unayempenda Ana Boyfriend


Related image
#1 Muulize swali lisilo moja kwa moja. Kumuuliza mwanamke swali fiche kama iwapo ana boyfriend ni muhimu sana. Kama ataona swali limekuja bila lengo flani basi atakwambia ukweli. So unaweza kumuuliza swali kama, “Sasa itakuwaje boyfriend wako akuache mahali kama hapa pekeako?”
Kumuuliza hivi atakujibu kiukweli wala hatohisi unashambulia himaya yake. Bora tu swali kama litokee kama utani na utulivu haitakuwa shida.
#2 Mwambie kuwa “boyfriend” wake bila shaka anampenda. Unaweza kusema neno kama hili ama ukatamka kitu kingine kama hiki. Ukimtajia kuhusu kitu ambacho boyfriend wake anapenda kumhusu, unaweza  kujua iwapo ana mmoja. Anaweza hata kukuambia, “Mimi sina boyfriend”
#3 Mwambie kuwa yeyote anaye kuwa naye amebahatika. Hii kando ya kuwa ni mbinu ya kujua iwapo ana boyfriend, pia ni mstari ambao hufanya kazi vizuri wakati unapotongoza. Hapa una uhakika kuwa utapata majibu mawili, “Sina boyfriend” ama “Ndio, ni kweli amebahatika.”
#4 Muulize kama yuko pekeake. Kama amekaa akiwa pekeake haimaanishi kuwa yuko pekeake. Anaweza kuwa ako na mtu mwingine ambaye ameenda kumchukulia kinywaji ama kujisaidia. Kama utapata nafasi ya kuongea na yeye unaweza kumjulia hali na iwapo yuko hapo na mwenzake. Hii haumuulizi moja kwa moja kama yuko na boyfriend, lakini anaweza kukuambia kama yuko na yeye hapo.
#5 Mwambie kuwa unatumai hujakalia kiti cha boyfriend wake. Wakati umekaa kando yake, tumia huu mstari. Kando na kuwa huu ni mstari mzuri wa kuanza mazungumzo na yeye, pia ni njia moja yakufahamu kama ana boyfriend. Mara nyingi wanawake katika hali hii hujibu, “Sina mmoja” na wala si “Haujakalia”
#6 Mwambie kuwa ungependa kukutana na yeye siku nyingine. Mwambie kuwa ungependa kukutana na yeye siku nyingine iwapo umekuwa na maongezi mazuri na yeye.Mtamkie haya maneno iwapo bado hujajua kama ana boyfriend au la. Hii ni njia nzuri ya kujua kama anakupenda. Kama anatakaa na kusema kuwa ana boyfriend basi ni hivyo.
#7 Muulize kuhusiana na wiki yake.  Kumuuliza mtu kuhusu programu zake za wiki huwa wakati mwingine bila kujua wanaweza kutaja wapenzi wao. Mfano unaweza kumuuliza mwanamke siku ya alhamisi na ijumaa ataispend vipi halafu akujibu, “Alhamisi nitakuwa kazini na ijumaa naspend katika club Savanna na boyfriend wako.” Pia wanaweza kuongea mambo ambayo utajua tu anaashiria yuko na boyfriend.

#8 Mnunulie kinywaji. Ukiwa umeenda klabu halafu ukakutana na huyu mwanamke, mnunulie kinywaji. Mbinu hii inaweza kuwa tricky kidogo. Wanawake wengine wanaweza kukubali uwanunulie kinywaji ilhali wako na boyfriends. So unachotakiwa kufanya ni kumwangalia kwa macho na umwashirie kile unachopania kutaka kutoka kwake. Kama atahisi kuwa unataka kitu kutoka kwake atafunguka na kukuambia.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome


No comments:

Powered by Blogger.