Kama unashidwa kumdekeza, atadekezwa na mwenzio!

Mpenzi msomaji kama una mpenzi wako na ukashindwa kumbembeleza basi tegemea kubembelezewa na wanaume au wanawake wenzio.
Angalia usije ukaishia kulalamika kila siku kuwa kila mpenzi unayekuwa naye unaibiwa, unapokonywa au anakuacha bila kujua sababu ya kuachwa kwako.
Penzi ni kitu kimoja laini sana ambacho wala huwezi kukielezea au kukishika. Na hata utamu wake ni mtamu ila huwezi kumuelezea mtu akauelewa uhalisi wa utamu wa penzi unaoumaanisha.
Hata hivyo penzi hilo limekuwa likiwatesa watu wengi sana wakiwemo wapenzi wachumba na hata wanandoa.
Kwa mtu ambaye hafahamu, mapenzi yanahitaji mambo mengi ili kulifanya penzi lako liweze kuendelea kudumu na kuwa bora, moja ya kitu hicho ni kubembelezana iwe kwa mwanaume au mwanamke na inapotokea huna muda wa kumbembeleza mpenzi wako basi tegemea kukaribisha usaliti ndani yako.
Hivi jaribu kutafakari kuwa umetoka kazini umevurugwa, kichwa kimejaa msongo wa mawazo ya kazi, maisha na mambo mengine halafu unafika nyumbani kwa mwenza wako ambaye ulidhani atakuwa sehemu ya kukubembeleza iwe kwa maneno au vitendo ili kukupunguzia msongo ulionao lakini yeye anaonekana yuko bize na hamsini zake, unadhani nini utakuwa unawaza kwenye akili yako.
Ulitegemea kupata faraja kwa mwanamke au mwanaume uliyempenda lakini anakuwa ni sehemu ya kukuongezea mawazo.
Bila shaka utajisikia vibaya na utamuona ni mwanamke au mwanaume nuksi.
Kama huwezi kumbembeleza mwenza wako ikatokea akapata mtu ambaye anamjali, anambem
beleza basi uwezekano wa kusalitiwa ni mkubwa.
Kubembelezana kunamfanya mwenza wako auhisi uhalali wa kukumiliki, ajione yeye ni mwenye bahati kubwa sana ya kupendwa. Unapombembeleza hata kama kichwa chake kinakuwa kimevurugwa lakini uwepo wako humfanya abadilike na kuchangamka kama hakuna jambo lolote gumu au lililomkwaza.
Katika kubembelezwa huku wanawake ndiyo hasa wanapenda na wanajua kuwa wanastahili wao zaidi kubembelezwa kuliko wanaume.
Kama wewe ni mwanaume hili unapaswa ulifahamu kuwa mwenza wako anategemea nafasi kubwa zaidi ya wewe kumbembeleza. Inawezekana hukuwa unalijua hili au ulijisahau basi ni vyema ukaelewa somo hili na kuliweka akilini mwako ikiwezekana hata ukalifanya kwa vitendo ili kuboresha uhusiano wako.
Kama ulikuwa hujui kuna wakati mwenza wako anatamani hata ashinde nawe ndani, mkicheza, mkitaniana, mkikwaruzana na michezo mingine ya kimapenzi lakini muda huo haupati kutokana na majukumu au mazingira yako ya kazi lakini ni vyema ukatenga hata siku yako ya mapumziko kushinda na kufurahia na mwenza wako kuliko kujifanya uko bize.
Kama utaendelea na ubize wako ipo siku utakuja kujutia kwani mwenza wako anaweza kufika sehemu akahisi labda pengine huna mapenzi naye, au upendo wako umeanza kuchuja au umepata mchepuko basi na yeye atatafuta mtu wa kumfariji.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
No comments: