Makosa 5 Unayoyafanya Wakati Wa Kudeti/Mahusiano
Kuna makosa ambayo yanajitokeza katika maswala ya uhusiano bila ya mtu kuyatambua.
Makosa haya yanachangia pakubwa kwa mwanaume kupoteza raha ya mahusiano ama kueza kuachwa na mpenzi wake bila yeye kufahamu kosa lilitokea wapi.
Well, nimekuja na baadhi ya makosa ambayo hujitokeza katika mahusiano.
Lengo langu kuu la kuandika chapisho hili ni kuona ya kuwa umejiondoa katika lile kundi la asilimia 99 ya wanaume ambao wanafanya makosa haya bila wao kujitambua.
Makosa katika mahusiano
1. Kushikikwa kwa mwanamke mmoja
Jambo hili hutokea hata kwa wale ambao wanajiita ma-pro wa kutongoza. Umekutana na mwanamke mrembo fulani ukaanza kujiambia “huyu mwanamke ni kila kitu kwangu”. Tatizo hapa ni kuwa utaanza kuamini ya kuwa mwanamke huyu ni kila kitu mpaka itafikia wakati flani hisia zako zote unaziweka kwake. Haya ni makosa makubwa kwani utajisahau ya kuwa pia wewe una maisha yako ya kuishi.
Tatizo kuu hapa ni kuwa utajaribu kila kitu kadri uwezavyo ili uhakikishe ya kuwa unamridhisha mwanamke huyu. Bila shaka itafikia wakati flani mahusiano yenu yatapotea.
2. Kuiga mifano ya wengine
Hii ni njia hatari zaidi kama umekita mizizi ya sanaa ya kuiga wengine. Kuiga mitindo ya wengine kutaharibu nafasi yako ya kupendwa na wanawake. Usijaribu kumuiga yeyote yule ambaye umemuona yuko sawa katika kutongoza wanawake. Wakati ambapo unaiga tabia za wengine, utakuwa unazificha nguvu zako halisi ambazo unapaswa kuzitumia kuwatongoza wanawake. Pia kuiga tabia za wengine kunakudhalilisha na pia kukupunguza motisha ya kujiamini.
3. Kufikiria kuwa ngono ndio mchezo wa mwisho
Cha kusikitisha ni kuwa kuna baadhi ya wanaume wanaowaona wanawake kama chombo cha starehe bila cha zaidi. Tatizo hapa ni kuwa iwapo lengo lako ni kufanya mapenzi, basi utakuwa ukijinufaisha wewe binafsi.
So badala yako kufikiria na kukwama kwa kufikiria ngono pekee, fanya hivi. Jiunganishe na wanawake kwa kuwa mkweli na wa hakika. Jionyeshe kwake, mtongoze kwa njia ya uhakika, na umpatie nafasi ya kuchagua kati yako na wengine ambao wanajaribu kumfukuzia. Wakati haya yote yakitokezea, hisia za kimapenzi kwake zitakuja kiasili. Haina haja ya kulazimisha vitu.
4. Kutumia Sanaa za Kutongoza bila mpangilio
Tatizo la kutumia sanaa ya kutongoza ni kuwa inafanya kazi katika baadhi ya sehemu ama situation flani pekee. Vibaya zaidi ni kuwa kutumia michongo ama mistari kunakufanya ujifanye kuwa mtu mwingine (soma point 2 hapo juu). Ok. Usinisome vibaya hapa. Kwa kawaida kutumia michongo na mistari si mbaya lakini kunafaa kuwe na ustadi wake flani. Sio kila mahali unatumia tu. Mwanzo mwanamke akianza kuonyesha interest kwako inahaja gani ya wewe kujitesa kwa kutumia sanaa ambazo zinahitaji ustadi? Jaribu kutumia asilia yako.
5. Kutumia njia fupi…halafu kukata tamaa
Kosa jingine ambalo baadhi ya wanaume hufanya ni kukata ama kupoteza tamaa wakati wanapotemwa. Ok tuweke wazi. Hakuna kitu kibaya kama kujaribu kufanya kitu halafu usione mafanikio. Kukataliwa na mwanamke kunaudhi! Lakini huku hakumaanishi kuwe ndio mwisho wa maisha.
Usitumie mbinu fupi ama za haraka za kuapproach mwanamke. Njia ndefu na yenye mafanikio ya asilimia 99 ni kutumia njia ya kumtongoza mwanamke kirafiki ambayo unaitumia polepole.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
No comments: