Mambo Muhimu kwa Msichana/Mwanamke Kuzingatia Kabla na Baada ya Kuolewa
Naomba kuleta kwenu mambo ambayo naamini ni muhimu kuyatafakari na kuyapa uzito wenye kustahili......
1) Kujitambua. Kila msichana aweze kutambua nini kinamfanya kuwa mwanamke. Kwa maana kama ni maumbile hiyo ni default settings, kama ni kuzaa mwanaume haendi leba, sasa ni nini kinakufanya kuwa mwanamke? Kujitambua, kujiheshimu na kuwajibika. Nyumba yenye mwanamke anayeheshimika ni Baraka na nyota njema. Nyumba yenye mwanamke asiyejiheshimu na kuheshimika huwa haitamaniki, wewe wataka kuwa yupi kati yao?
2) Kila mwanaume ni tofauti. &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];'wanaume wote ni wale wale tu'' Ni vibaya sana kumchukulia mwanaume sawa tu na wengine (hata kwa rafiki wa kawaida tu). Kuwa unajua au umesikia sifa mbaya za wanaume flani na flani, au umewahi kuwa na mahusiano na ukaona sifa mbaya kadha wa kadha za huyo, ukaja ukampata mwingine then unamchukulia ni sawa na hao wengine tu. (kosa kubwa sana) Kila mwanaume ana sifa zake na mapungufu yake. Sifa na mapungufu ya mmoja sio sawa na mwingine. napia kila mwanamke ana sifa za kipekee. Watch out.
3) kuamua kuolewa au kutokuolewa. Uamue kama unajiona una wito wa kuolewa au la tena uamue kwa utashi wako mwenyewe. Usipokuwa umeamua unakosa nafasi adhimu ya kuwa umejianda kuwa chini ya mume na utaona kama unaonewa vile!! Mabaya aliopitia mama au jirani yako kwa mumewe isiwe ndio determinant factor kwa huwa hutaolewa . kwani utaolewa na huyo mtesaji au huyu unayemchukia? Hakika Utaolewa na mwanaume mwingine mwenye sifa na tabia tofauti na kila kitu tofauti na hao, kwa nini uwatumie hao kama ndio wawakilishi wa wanaume wote na ndio wako hivyo? Kwa nini wengi wenu msijifunze kwa wanawake waliofnikiwa kwenye ndoa kuliko hao role models wa kwenye taarabu na saluni? tunajifunza kutoanguka kwa walioanguka iweje hao walioshindwa ndoa ndio wawe chachu kwako? si unajua ni wanawake wachache sana wanapenda kuona mwenzake akifanikiwa?? wengi wanapenda mabaya au shimbo alioanguka na mwenzake nae aanguke hapo. so sikilizeni na mchanganye na za kwenu
5) Dhana ya haki sawa. Binafsi naamini kila binadamu ni sawa, ila linapokuja swala la mume na mke huwa nashindwa kuelewa ni haki zipi izo zinazopiganiwa wakati katiba ya nchi haitamki jinsia kwenye haki na stahili? ni haki zipi izo labda enyi wana. Au mnataka mke akiwa anakata kitunguu mume awe anakata nyanya?? Mwanamke anapewa heshima ya kuwa msaidizi wa mume. Kuna umuhimu sana wa kutambua na kuchukua nafasi yako kama mwanamke. Beijing waache na wabeijing wenzao. Mwanaume ni Kiongozi wa Mkewe na familia nzima (sifa ya kiongozi- anajali- anawatanguliza wenzake, anasikiliza, anashaurika, anaona mbele, anawajibika, hekima na busara etc)
6) Kujua kupangilia matumizi. Kwa pesa ya familia ya yake kwa ajili ya matumizi binafsi. &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];'spending wisdom'' sio kila nguo mpya unayo, msuko mpya unao, kiatu kipya unacho, saa mpya unayo, mkufu mpya unao, kulikoni kwani u show room yakhee! Kwa kile kingi au kidogo mnachojaliwa, kitumieni kwa hekima na shukrani.
7) Afya &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; kitambi. Nyie wana naona siku hizi mwaona sifa kushindana na sie akina kpt Komba kwenye vitambi eeeh!nyie ngojeni. Kwani nani kawadanganya chipsi ndio default food kwenu? Pizza na burger? Mwapenda sana roast nyie watu! Acheni hizo; tafuneni vitu vya maana. Naona wengi wanafunga mayenu siku hizi kisa vitambi. Mke kitambi mume nae kitambi&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];.. kazi ipo.
8) Kukubali chngamoto za kuishi na familia nyingine (Kuna kupata kibali papo kwa papo, kuna kukosa kibali na kuna kuchelewa kupata kibali. Jikubali as far as una kibali mbele ya mumeo, songa mbele watakukubali tu.
Kuna wadada wenye kupendwa, yaani mara ya kwanza na anakubalika sana kwa wakwe zake hivyo hivyo mwa mwanaume. Kuna akina sie yaani kuonekana tu, kila mtu anakuchukia, watu wa namna hii wengi wao wamekuwa wa maana sana kwenye hizo familia baada ya muda.
9) Kujua kuusoma mchezo. Kwa wapenda mpira Sir Alex Furgason alikuwa na sifa kubwa moja; Anaweza kuusoma mchezo na anajua apange mchezaji gani kwa mechi ipi na akitoa sub imekaa vizuri unlike kocha wangu Wenger. Huyu alifanikiwa sana.Sasa kwenu nyie watu, Lazima ujitahidi sana kucheza na saikolojia ya Mwanaume, uje hapa anastahili kuambiwa nini na hapa kamaanisha nini, anahitaji space etc wanaume ni wagumu kuliko mnavyowafikiria (siongelei wavulana apa)
10. Kujenga Nyumba. Majengo twajenga sie wanaume, ila Mwanamke kapewa kibali cha kujenga familia na nyumba kwa maana ya watu na mahusiano. Kwa familia yenye amani, furaha na upendo mkubwa, kaichunguze, utakuta Mke ndio ufunguo vinginevyo mke akiwa mtu wa magomvi, chuki, uchoyo na mengineyo ya kufanana na hayo, kila kitu huenda kombo. Marafiki wa mume wanaishia tu kukutana Bar, Ndugu zenu mnakutana tu kwa vikao, na majirani mnaonana tu kunapokuwa na msiba karibu.
11) Maombi. Katika eneo ambalo ni la muhimu lakini limesahaulika ni hili la kumuombea Mume. CC ablessed na gfsonwin . Mke ndio kishikilio cha mume asianguke na hata akianguka Mke ndio anacheza sehemu kubwa kumuinua
12) Kuchagua Familia, Ajira au Kuajiriwa. Msinipige mawe jamani ukweli lazima usemwe. Ukifuatilia historia tangu na tangu, mwanamke amekuwa mlezi wa familia na mume amekuwa ndio anayetoa matumizi yote ya familia. Na ndio majukumu yao. Kwa sasa mwanamke nae amekuwa akihusishwa kutoa matumizi ya familia of which is wrong ila kutokana na ugumu wa maisha tumehalalisha. Mwanamke anaacha watoto ambao ndio msingi wa familia na wenye thamani kuliko vyote na kukesha kwenye kusakanya hadi usiku mzito. Watoto hawana maadili tena, wamekuwa wakilelewa na mtu baki tena mtoto mwenzao na siye na elimu hata kidogo. Sasa mnataka malezi gani kwa watoto wenu? Na ikitokea wahudumu wa ndani wamewaharibu nani wa kumlaumu&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];. najua wengi watakua wakali apa wasipolitazama kwa upana wake....
13) Mavazi. Katika eneo ambalo halizingatiwi ni hili? Mnavaa nguo za wadogo zenu, nguo za kulalia mnavaa kwenye matukio au mnatoka nazo barabarani etc. sio kwa wasichana pekee hata baadhi ya walioolewa wanakosea sana katika hili. Wengine wanabweteka na komenti za wanaume eti mmetokelezea, hamna kitu apo, kakutamani na gia ya kuanzia ndio hiyo hujapendeza wala nini. Mavazi yenye kuusitiri mwili humheshimisha sana mwanamke
14) Kujipamba. Unakuta mtu kapaka kila kucha rangi ya nchi tofauti (sijui mguu huu rangi ya Malawi, southern sudan, Congo DRC, na Angola huu mwingine kapaka Tz, Kenya, Somalia na Kongo Kinshasa) kulikoni nyie watu? Lipsi nyeusi tii zimepakwa sijui ni coral paints ni nyekunduuuu. Nyusi zote zimeondolewa then kapaka apo wanja mweusi kachora kama nyusi (hio ni akili kweli? Walioanza kutinda nyusi wanabakisha nyingi kuliko wanazoondoa ila ninyi (sio wote) either zinaondolewa zote au zinazoaki ni chache kuliko zilizoondolewa. Mtu usoni kapaka vitu vingi yaani kama hujamzoea ndio unamuona mara ya kwanza akiwa amejipara lazima umpite au yeye ndio akushtue. Si vibaya kujipamba lakini iwe kwa kiasi, Mnapendeza zaidi mkiwa kwenye uhalisi wenu zaidi.
15) Kusamehe... kwa kuwa hisia zina mchango mkubwa sana kwenye maamuzi yenu, tafadhali jueni kulipa kisasi si juu ya mwanadamu bali ni Mungu, Basi ndugu zangu mkajitahidi kujifunza kujisamehe na kuwasamehe wengine. Vifua vyenu na vikajazwe kumbukumbu nzuri mnazotamani kuzikumbuka wakati wote, na fikra zenu mkaziongoze kuyatafakari yale myapendayo kuliko yale myachukiayo (hasira za kulimbikiza na tamaa ya kulipa visasi visitajwe tena kwenu). Maisha ya mwanadamu ni mafupi nayo yapita kama kite, Basi mkaelekeze nguvu zenu kujitendea mema na kuwatendea wengine mema. Furaha yenu na ikadhibitishwe kwetu kwa yale mema mnayoyatenda kuanzia na jamaa zenu. Mkazidi kuimarika katika kuwapenda watoto na waume zenu; maana hakuna hadi leo alieyewahi kuotesha mabaya akavuna mema, bali mema yameendelea kuzaana kizazi hata kizazi, Basi mkawaotesheeni kizazi chenu neema na mema kwa kuwa Mungu hulipiza kizazi cha kwanza hadi cha nne yale wayatendayo wazazi (mema kwa mabaya). cc dada zangu wapendwa snowhite,na Karucee
Mungu awabariki.
from Tujifunze Mapenzi https://ift.tt/2zQMVSu
via
No comments: