MAMBO YA KUFANYA UNAPOKUWA NA MPENZI MWENYE WIVU KUPITA KIASI

Kila binadamu ameumbwa akiwa na wivu ndani yake. Hakuna binadamu ambaye ahajwahi kupatwa na hali ya wivu. Hata watoto wadogo huwa na wivu sana.
Utakubaliana na mimi kuwa wivu umeanza tokea mtu akiwa mchanga, ukichukua mfano mdogo tu wa mtoto anapokuona ukiwa na mama yake au mama ambebe mtoto mwingine wakati wa kwake anamuona. Wote tunajua kitakachotokea. Hivyo hivyo kwa watu wazima hasa ukija kwenye suala la mapenzi.
Kimsingi wivu ni mzuri sana katika mapenzi kwani humfanya mtu kuwa mwangalifu na kumjali mwenza wake ili asije akampoteza.
Lakini wivu unapopitiliza kiwango, huo unaweza ukawa hatari katika mahusiano. Badala ya kujenga wenyewe ndio ukaharibu.
Kuna kiwango cha wivu ambacho kinavumilika, lakini wivu ule ambao mpenzi wako hataki kukusikia hata ukiongea na mwanaume/ mwanamke mwingine kwenye simu hata kama ni rafiki wa kawaida tu basi huo ni wivu mbaya na hatari.
KAma una mpenzi mwenye wivu mkubwa (uliopita kiasi) kuna mambo machache unayopaswa kuyazingatia kila mara ili kumfanya ajisikie amani na kuupunguza wivu wake kama siyo kuuondoa kabisa.
Yafuatayo ni mambo ya msingi ya kufanya kama mpenzi wako ana wivu mkubwa juu yako
Mfanye atambue kuwa unampenda
Jitahidi kadri ya uwezo wako kumfanya ajue kwamba kweli unampenda. Unaweza kufanya hivyo kwa kumpa zawadi mara kwa mara, kumtumia jumbe za kimahaba, na kupenda kuwa nae kila wakati.
Anapaswa kutambua kuwa huna nia na watu wengine zaidi yake
Mpenzi mwenye wivu huwa ni vigumu sana kuendana naye kama bado hujatambua. Lakini pale unapotambua hakikisha anajua wazi kuwa yeye pekee ndiyo chaguo lako na si mwingie yeyote. Ukikutana na mtu mwingine ambaye ataonyesha kuvutiwa na wewe mjulishe wazi kuwa una mpenzi na epuka kufanya matendo yatakayomtia mashaka kama vie kurudi usiku sana ama kutumia muda mwingi kwenye simu yako.
Epuka kumtengenezea mazingira yatakayompa wasiwasi
Umeshajua kwamba una mpenzi mwenye wivu kupita kiasi, ya nini kwenda kupokelea simu chumbani au nje? Fanya mambo yako hadharani ikiwezekana na yeye ajue kinachoendelea kama tu yeye kujua hakutaathiri chochote. Epuka kutoka hasa nyakati za usiku na marafiki ambao hawaamini. hii itamfanya apate amani na kuwa na furaha na huenda wivu wake ukaisha kabisa.
Tenga muda mwingi wa kuwa pamoja nae
Unapokuwa na mpenzi wako kwa muda mwingi utamfanya ajisikie furaha, ajiamini na ajisikie amani kwani utamjengea mazingira kuwa huna mpango na watu wengine zaidi yake.
Usimwache atembee peke yake
Mnapokwenda mahali, mfano kwenye sherehe, ama matembezi hakikisha unakuwa naye muda wote. Waache watu wafahamu kuwa ni mpenzi wako. Hii itampunguzia kiwango vha wivu na kumfanya awe mwenye kujiamini.
Kuwa mvumilivu
Mpenzi mwenye wivu anaweza kuonekana kama mzigo katika mahusiano lakini kadri unavyozidi kumuonyesha kuwa unampenda ndivyo hivyo naye kiwango chake cha wivu kinazidi kupungua. Hivyo usichoke, mfanye ajisikie kupendwa na misho wa siku utaona mabadiliko.
Mwonyeshe kuwa unamfikiria kila muda
Hasa unapokuwa mbali na mpenzi wako, muoneshe kuwa yuko katika fikra zako kila mara kwa kufanya mambo kama vile kumpigia simu, kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi. Unaweza pia kuachaujumbe mfupi kabla hujaondoka

No comments:

Powered by Blogger.