MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA NDOA

Related image

Mungu alimfanya mke kutoka kwa mume, awe mwenziwe na msaidizi wake akaye pamoja naye, kumfurahisha, kumtia moyo na kumpendeza, naye mume amepaswa kuwa msaidizi wake imara. Wote wanaoingia katika umoja wa ndoa wakiwa na kusudi takatifu mume kuyapata mapenzi safi ya moyo wa mke, na mke kulainisha na kuikuza vizuri tabia ya mumewe na kuikamilisha hulitimiza kusudi la Mungu kwao.

YAFUATAYO NI MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA NDOA

1.TATHMINI YA MAISHA YAKO
Itakuwa ni vema kabla ya kutafuta mwenzi wa maisha ujitathmini kwanza wewe mwenyewe na hili unaweza kulifanya kwa kutafuta marafiki wanaokufahamu vema na uwape uhuru wa kukuambia ni wapi una mapungufu na ni wapi unafanya vema. kwa yale unayoyafanya vizuri muombe Mungu akusaidie uendelee kuyafanya kwa ubora zaidi lakini kwa yale mapungufu tafuta namna ya kuyarekebisha. Kumbuka kuwa ni vigumu kujijua mwenyewe.
                "Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; ni nani awezaye kuujua"

2.UCHUMBA
Unapomchagua mvulana au msichana kuwa mchumba wako ni vizuri kuchunguzana kujua uzuri na udhaifu wa kila mmoja. na mkishayafahamu kila mmoja anawajibika kuboresha uzuri alionao na kwa maombi mengi kurekebisha udhaifu alionao. Kumbuka kuwa huwezi kurekebisha madhaifu yote bali unaweza kuyamudu yasilete madhara kwa mwenzako hasa pale unapoyagundua. Pia Mungu ni suluhisho kwa kila jambo kwani hata katika udhaifu anaweza kuleta nuru njema.
 Katika uchumba pia zingatia yafuatayo.

            I.Uaminifu
        Je mchumba wako ni mwaminifu katika mambo yote? hili ni jambo la msingi sana lakini hili litawezekana kwa kumtazama kama ni mwaminifu kwa Mungu wake. Ikiwa ni mwaminifu kwa Mungu wake ni dhahiri kabisa anaweza kuwa mwaminifu kwako. Kamwe msifanye ngono na ikiwa mchumba wako atahitaji hilo basi tambua kuwa hawezi kuwa mwaminifu katika ndoa yako.

        II.Tabia
hakikisha kuwa yule mume au mke mtarajiwa ana tabia njema. Mwandishi mmoja anasema "Utu wa Mtu unatokana na tabia yake" pia ameendelea kwa kusema "Tabia ya mtu huundwa utotoni na ni vigumu sana mtua kuacha tabia yake". hivyo kuwa makini katika tabia ya mchumba wako.

      III. Kupenda kazi
mtu kama hapendi kazi atakuwa mzigo kwako hivyo hakikisha anayetaka kukuoa au kumuoa anapenda kazi. kumbuka mtu mvivu ni kikwazo kikubwa sana kwa mchapa kazi na kwa maendeleo ya nyumba yenu.

     IV. Imani moja Nawe
Hata kama atakuwa dini moja na wewe mfano mkristo kwa mkristo ni lazima uhakikisha ni dhehebu moja na wewe. Tofauti ya imani ya kidini inaweza kuleta mtafaruku mkubwa sana kati ya mtu na mwenzi wake wa maisha. na usidanganyike kwamba utambadilisha. Kumbuka ni Mungu pekee ndiye anayeweza kumbadilisha mtu na sio wewe.

     V. Kutopitana sana kielimu
hili linagusa sana upande wa akina dada. inavyoonekana wanaume wengi ndio wanaoweza kuishi na wanawake wenye elimu ya chini sana, lakini ni mara chache ukute wanawake wanaoweza kuishi na wanaume wenye elimu ya chini sana. hili linaweza kuleta mtafaruku mkubwa sana.

    VI. Kutopitana sana kiumri
hapa kwanza ni kimtazamo, mnapopitana sana umri kila mmoja anakuwa katika ulimwengu wake na hivyo kutofautiana sana kwa mwenendo na mambo yanayozungumziwa sana katika umri husika. pia mwanaume akiwa mkubwa sana atakufa mapema na kumuacha mke wake akiwa bado mdogo na huwa ni vigumu sana kuolewa tena, wakati wanaume wao wanaweza kuoa tena wanapofiwa na wake zao.

     VII. Muonekano unaokupendeza
kila mmoja ana namna yake anayotazama na ana vitu vyake anavyovipenda kwa kijana wa kiume au wa kike. usichumbie tu kwa sababu unataka kuoa lakini tazama pia muonekano unaokupendeza ili kila unapomtazama mwenzi wako uwe ni mtu wa kufurahi na sio kuogopa kutembea naye barabarani. Kumbuka watu wote ni wazuri, inategemea uzuri wako umelenga katika mambo gani.

    VIII. Hali ya kipato
kama kijana anatoka katika familia tajiri hakikisha unafanya kazi kwa juhudi kubwa ili asiishi maisha ambayo hayajazoea tokea utoto wake. kwa maisha yakiwa tofauti sana na alivyozoea hapoa awali, kuna uwezekano wa upendo kupungua.


3. SHEREHE ZA ARUSI
usifanye arusi ya gharama kubwa kuzidi uwezo wako



karibu tena katika mada zinazokuja
shukrani kwa mwl wangu Pr Mange kwa kitabu chake
MAHUSIANO MEMA(mengi nimeyatoa humo)


from Tujifunze Mapenzi https://ift.tt/2EimWXO
via

No comments:

Powered by Blogger.