Mbinu za kumshawishi mpenzi wako asikusaliti

Image result for UTAMU WA MWANAMKE
Ni jambo muhimu sana kwa wapendanao kujenga na kuimarisha nguvu ya penzi lao, kwakuwa husaidia kujenga uhusiano bora, imara na wa kudumu. Pia itakufanya umuone mpenzi wako mpya kila siku na wakati mwingine itakufanya ujiskie ni kama mnalianzisha penzi lenu changa.

Nina maana gani ninaposema nguvu ya penzi?

Nguvu ya penzi ni ule muunganiko, hamu au shauku kubwa unayojisikia moyoni juu ya mpenzi wako. Unakumbuka jinsi nafsi yako ilivyokuwa ikiwehuka mlipokuwa mnaanza mapenzi yenu, hasa ile wiki ya kwanza mlipokubaliana kuwa pamoja kama mtu na mpenzi wake? – Ile shauku iliyokuwa imeujaa moyo wako kila mara hata unapolikumbuka jina lake , ndio jambo ninalolizungumzia  hapa.
Zifuatazo ni mbinu 6 unazoweza kuzitumia kuongeza na kuimarisha nguvu ya penzi lako.
  1. Livutie subira tendo la ndoa.

Kwa kukaa siku kadhaa bila kushiriki tendo la ndoa na mpenzi wako, kutakusaidia kuongeza hamu ya kumshirikisha hisia zako za mahaba, hali ambayo itapelekea kuiamsha shauku yako juu yake. Mnapokaa kwa kipindi Fulani bila kushiriki tendo, mnajipatia nafasi ya kuyapitia na kufurahia maisha yenu kiurafiki zaidi.
  • Ni vyema kama utamshirikisha mpenzi wako kuhusu mpango wako wakutaka kuongeza na kuimarisha nguvu ya penzi lenu ili isijeleta mtafaruku kati yenu.
  • Pia unapopata mafundisho mazuri ya kuboresha penzi lenu, jitahidi kumshirikisha na mwenzi wako ili mpate kwenda sambamba.
  1. Wasiliana na mpenzi wako mara kwa mara.

Mawasiliano ya mara kwa mara kati ya wapenzi husaidia kujenga na kuimarisha nguvu ya penzi lao. Hakikisha unatenga muda wa kutosha kufanya mawasiliano na mpenzi wako kumjulia hali, kufanya utani, kumchekesha, kumfundisha na pia kujua maendeleo ya kazi zake. Usiruhusu siku ipite bila kumjulia hali mpenzi wako.
  • Acha visingizio vya muda, unayo simu ya mkononi na kwa neema za Mungu gharama ya vocha ni nafuu na ukweli ni kwamba kama kweli unampenda mpenzi wako lazima utatenga muda hata dakika 10 kwaajili yake.
  • Kumbuka moja ya nguzo muhimu kabisa za mahusiano bora ni mawasiliano. Tumia muda wako kwa busara!
  1. Toka nae “Deti”

Kutoka na mpenzi wako ni njia nzuri mojawapo ya kuimarisha nguvu ya penzi lako. Kutoka na mpenzi wako kunasaidia kujifurahisha kwa kubadili mazingira kutumia vyakula na vinywaji vilivyoandaliwa na watu wengine na katika mitindo mbalimbali. Pia inawapatia muda mzuri wa kuyafikiria maisha yenu chanya.
  • Sio lazima mwanaume ndiye akutoe out, hakuna sheria inayomzuia mwanamke kumtoa mpenzi wake out hivyo unao uhuru wa kulifanya jambo hilo kuwa moja ya chaguo lako binafsi.
  • Unapotoka na mpenzi wako epuka kuifanya nafasi hiyo kuwa fursa ya kutatua migogoro yenu  vinginevyo muwe mmekubaliana hivyo.
  1. Mjadili hofu na matatizo yenu.

Unatoa nafasi kubwa ya kujenga na kuimarisha nguvu ya penzi lenu ikiwa kama mtajadiana hofu na matatizo yenu pamoja, kufunguka, kutafuta ufumbuzi na kutiana moyo kutaleta hali ya kuthaminiana katika shida na raha.
  • Katika kutafuta suluhu ya matatizo yenu, mnatakiwa kuwa wawazi na wakweli, Kumbuka kuwa hata ukienda kwa daktari au mtaalamu wa masuala ya saikolojia atakusaidia kulingana na utakachomweleza.
  1. Msafiri pamoja.

Ipo raha ya kipekee sana ukisafiri na mpenzi wako. Binafsi napenda sana kufanya utarii na hata kama sio mbuga za wanyama, napenda kutembelea mazingira mapya na kuchunguza mambo mbalimbali kama uoto wa asili, kilimo, na hali ya hewa ya sehemu husika. Amini nakwambia hakuna jambo linaloleta furaha ya nafsi kama kushiriki mambo yote hayo na mtu umpendaye, kwa kufanya hivyo unajitengenezea wewe na mpenzi wako shauku ya kufurahia mambo mbalimbali pamoja.
  • Jitahidi kupanga bajeti yako vizuri itakayowezesha kutoa nafasi angalau hata ya safari tatu au mbili  kwa mwaka.
  1. Kupika Chakula Pamoja.

Kupika chakula pamoja ni moja ya njia bora za kuimarisha nguvu ya penzi lenu kwasababu inatoa nafasi yako wewe na mpenzi wako kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu. Pia inatoa nafasi ya kuendeleza ubunifu na kuwaweka tayari kusaidiana wakati ujao hasa inapotokea mkeo anaumwa.
  • Ondoa imani potofu na mawazo hasi kwamba ukionekana unampikia  mkeo utasemwa kuwa umepewa limbwata. Kumbuka maisha ni yako wewe na wewe pekee ndiye mwenye uamuzi wa kuyaishi utakavyo, sasa kwanini watu wakushike masikio hata kwa mambo binafsi kama hayo, mbona ratiba za kufanya tendo la ndoa haupangiwi na mtu?!

Mapenzi yanahitaji ubunifu na kujifunza, hivyo basi usikae ukabweteka ukidhani yale mapenzi unayoyaona kwenye muvi yatajileta yenyewe.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome


No comments:

Powered by Blogger.