Mpenzi wako anapogombaniwa ndio wakati wa kujua kama unapendwa au mwenzio ndio mambo yote
Nimekuwa nikifikira juu ya swala hili kitambo na hatimaye kuamua kulileta mezani ili tulijadili kwa pamoja.
Kumekuwa na mitafaruku ya kimapenzi ya hapa na pale (kuingia kwenye mgogoro na mtu ambaye mnampenda me au ke mmoja)hasa kwa wale ambao ndo kwanza wamo katika kipindi cha upenzi au uchumba tu,na mitafaruku hiyo hutokea eiza kwa kusababishwa na mpenzi au kwa kujitokeza yenyewe tu.
Katika mitafaruku kama hii huwa kuna yule anayependwa kikweli na yule anyetumiwa kama part time(hii husababishwa na mpenzi mwenyewe eiza wa kike au wa kiume kwa kuamua kuwa na mtu mwingine wa ziada huku akijua kabisa kuwa na mtu anayempenda kwa dhati)
Na pia hali nyingine kuna mtu kujikuta tu kuwa ana nyota ya kupendwa(hapa mtafaruku hutokea bila matarajio ya mpenzi ila mtu hujikuta katika hali ya kugombaniwa ili mpendwaji amilikiwe na mmoja wa marivals)
Katika hali kama hizo wengi wao huamua kuingia kwenye mpambano ili kuhakikisha yeye ndo anakuwa mmiliki halali wa mtu huyo.
Lakini mimi leo nina maoni tofauti, nafikiri kama mtu anaweza kujikaza kisabuni(nasema hivi kwani najua linapokuja swala la mapenzi inahitaji moyo jamani kwani mapenzi yanauma usiambiwe)na anapenda kujua ikiwa kwa kweli yeye ndo chaguo la mgombaniwa, nafikri kukaa kimya bila kurudisha tusi au shambulio lolote kwa yule aliyeanzisha ugomvi ni njia nzuri zaidi.
Kwani kama mgaombaniwaji anakupenda wewe na wala hujaonesha ugomvi wa kumgombania basi atasimamia upande wako wewe anayekupenda na mwisho wa siku atakuwa na wewe.
Lakini ukisema na wewe uingie kwenye ugomvi huwezi kujua ikiwa unapendwa au mwenzio ndo mambo yote,kwani huenda ukashinda ugomvi na hata kama hukupendwa wewe ila yule aliyependwa akaamua kabisa kuachana na huyo unayempenda na hivyo unayempenda wewe kujikuta hana jinsi zaidi ya kuwa na wewe.
Na zaidi ni kama kujishushia heshima yako kwa yule anayekupenda.
Maoni yangu ni hayo tu kwa leo wadau wengine mnasemaje?karibuni tutiririke kwa pamoja
from Tujifunze Mapenzi https://ift.tt/2Elprc3
via
No comments: