Sababu za mwanaume kushindwa kurudia tendo la Ndoa!

Kusema kweli hili sio tatizo kubwa linalohitaji tiba ya matatibu kwa kiasi hiki, isipokuwa ni kupata elimu ya kutambua uwezo wa miili yetu. Kwa maana hiyo maelezo ya dondoo zifuatazo yanaweza kumsaidia mwenye tatizo hili.



MAZOEA YA MWILI: Watu wengi wenye mjukumu hujikuta wakiizoeza miili yao kufanya mapenzi kwa tendo moja kutokana na kukosa nafasi, kwao kukutana na mwanamke ni short time.

Kwa maana hiyo miili yao hukosa hamasa ya kurudia kutokana na mazoea. Hivyo mhusika anapotaka kwenda raundi nne lazima aanze kuuzoeza mwili kidogo kidogo asifikiri atakurupuka mara moja na kwenda mara tano.

Huo ni upofu wa kielimu. Kwa maana hiyo mwanaume kabla hajalalamikia kushindwa kurudia aangalie historia yake kwamba amekuwa anashiriki mara ngapi!
UMRI WA MTU: Kuna watu wengine wa ajabu sana wanajikuta wakihangaika kutafuta dawa za nguvu za kiume eti kwa sababu hawaendi kama zamani, ilhali wanajua fika nguvu za mwili hupungua kutokana na umri unavyokwenda.

Maana itakuwa ni ujinga kumwabia Firbat Bayi atimue mbio kama zamani! Kumbe kinachotakiwa ni kukubaliana na hali na kutulia na kuachana na hofu ya kupungukiwa nguvu za kiume!
HAMASA KUSHUKA: Upofu mwingine wa kimawazo ni kwa wanaume na wanawake kutotambua kuwa hamasa ya kimapenzi hushuka kulingana na muda wa wapendanao kuwa pamoja. Kuna wengine wanadhani kuwa watadumu kwenda mara sita au saba kama walivyokuwa wakati wa uchaga wa penzi lao.

Na wakiona dosari wanaanza kulaumiana, "mbona zamani mume wangu ulikuwa unakwenda mara saba!" Ukweli ni kwamba kakuchoka miaka kumi, kunakipi kipya kitakachoamsha hamasa ya penzi na endapo mitindo ni ile ile na migogoro kibao?
Kwa maana hiyo ukichunguza kwa makini utaweza kubaini kuwa watu wengi wanawake na wanaume wanajitesa na mawazo ya kupungukiwa nguvu za kufanya mapenzi bila sababu. Kama wangekuwa na ufahamu juu ya mabadiliko ya miili yao wangekubaliana na ukweli wa mambo na kuacha kujisumbua kulilia ujana ambao umeshawapita.

Mwisho kama nilivyosema katika mfululizo huu wa mada za upungufu wa nguvu za kiume ni kwamba siku zote mwili wa mwanadamu una desturi ya kuzoea kile ambacho kinafanyika kila siku. Kwa mfano kama wewe huna desturi ya kunywa chai asubuhi, mwili wako hauwezi kudai chakula hicho kamwe kutokana na kwamba sivyo ulivyozoezwa.

Lakini kama mwili huo huo utazoezwa kinyume chake na kulishwa chai kila asubuhi basi itakuwa vigumu sana kwa mtu husika kupitisha masaa hayo kama hakutia kinywaji hicho mdomoni. Hivyo basi kabla ya kwenda hospitali au kubwia madawa ya kuongeza nguvu jiulize maswali juu ya mazoea yako.

Na kama ukitaka kubadilisha mazoea hayo kumbuka kuwa haitakuwa jambo la leo bali litachukua muda kuliwekea kumbukumbu katika mwili wako. Hivyo basi nawashauri wale wote ambao wanashindwa kurudia kufanya tendo wafanye utafiti juu ya nini kinapungua katika ushindwaji wao.

Lakini pia wasikubali kukata tamaa na kujiona hawawezi eti kwa sababu wamekutana na mwanamke fulani na wameshindwa kufanya hivyo.

Kwani mbali na hayo niliyosema kuna jambo la nguvu za mwili kutokana na siku husika. Kuna siku nyingine mtu anaweza kuwa dhaifu tu kwa namna moja au nyingine. Anaweza kuwa kachoka, ana mawazo, anaumwa, hana furaha kutokana na sababu wazi au zilizojificha na mambo kama hayo!
Hivyo isiwe jambo rahisi kwa mhusika kujilaumu na kujiona hafai, kufanya hivyo kutazalisha wasiwasi na matokeo yake mtu huyu atakuwa akitokewa na hali hiyo kila anapokutana na mwanamke na pengine akabaki na kumbukumbu kuwa mara ya kwanza kutokewa na hali hiyo alikuwa na mwanamke fulani na hivyo kuingiwa na mawazo kuwa pengine alirogwa na kusahau ukweli kuwa kajiroga mwenyewe na hofu yake! Leo tupige kambi hapa tuonane tena wiki ijayo. Nawatakia kazi njema!


No comments:

Powered by Blogger.