Utafiti: Asilimia Kubwa ya Wanaume Hawana Nguvu za Kiume

Utafiti wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) umebaini kuwa asilimia 33 ya wanaume 672 mkoani Dar  es salaam wamebainika kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.

Hayo yamezungumzwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Dk. Pedro Pallangyo ambaye ameeleza kuwa idadi kubwa ya wagonjwa hao wanasumbuliwa na tatizo kubwa la shinikizo la damu  na kisukari.

Utafiti huo uliofanywa na JKCI, umebainsisha kuwa  katika wanaume watatu mmoja aligundulika kukosa nguvu za kiume.

”Hali hii inaashiria kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara jambo ambalo linasababisha athari ya nguvu za kiume kuwa kubwa ,” amesema Dk. Pallnagyo.

Aidha amesema changamoto hiyo inaweza kutatuliwa iwapo jamii itakuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema na kupata matibabu.

Pia alichukua nafasi kutoa ushauri kwa wanaume kupunguza sana matumizi ya chumvi nyingi mwilini na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi kwani hivyo huchangia kwa kiasi kikubwa sana magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari na kupelekea nguvu za kiume kushindwa kufanya kazi yake kama mabavyo inatakiwa.



No comments:

Powered by Blogger.