FAHAMU KITU HATARI SANA KATIKA MAPENZI NA FAMILIA
WAPENZI wanagombana, ndoa
zinavunjika na familia nyingi zipo kwenye
msoto kwa sababu ya ubinafsi.
Tunazungumza mengi lakini ukweli ni
kwamba endapo kila mmoja atafanikiwa
kuushinda ubinafasi, upendo utashamiri
kila kona.
Ubinafsi una matawi mengi. Mtu
anaposaliti, maana yake ametekwa na
tamaa binafsi. Anashindwa kutambua
kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa
hiyo anatakiwa kulinda penzi la
mwenzake. Hajui kama anachokifanya ni
dhuluma ya hali ya juu.
Ukweli ni kwamba unapoanzisha
uhusiano na mtu, maana yake umeamua
kumchagua yeye ndiye amiliki penzi lako.
Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine,
huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi
kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za
ndani ya mwili wako mwenyewe.
Kwa nini ukimfumania mwenzi wako
panachimbika? Ni kwa sababu
alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako,
kwa maana hiyo amekutendea dhuluma.
Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana
kwa sababu haki yako imetumika ndivyo
sivyo.
Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi. Umeingiwa
na jeuri kwamba unacho ndani ya mwili
wako, kwa hiyo unaweza kukitumia bila
kumshirikisha mwenzi wako. Hiyo ni
tabia mbaya mno. Kabla ya kusaliti, fikiria
utakavyoumia pindi utakaposalitiwa.
Kama inauma, ni kwa nini umtende
mwenzako? Je, umemuona yeye hana
moyo? Anza leo kukemea ubinafsi.
Popote pale utakapoona unachukua
nafasi, upinge kwa sababu ni adui
mkubwa mno kwenye mapenzi. Siku zote
usiseme "nipo", sema "tupo".
Unapozunguka, usiwaze "upo",
unatakiwa kuwaza "mpo". Hii itakusaidia
kulinda siti ya mwenzako kila
utakapokwenda. Hakikisha nafasi ya
mwenzi wako haichafuliwi au kutolewa
mkopo. Kama ilivyo kwenye soka,
wachezaji huchezea timu nyingine kwa
mkopo ndivyo na mapenzi ya sasa
yalivyo.
Ni kweli mtu ana mpenzi wake lakini
anavyojieleza anatoa picha kwa muulizaji
kuona kwamba aliyepo si muhimu sana.
Hii husababisha muulizaji aombe kukaa
na baadaye hukaribishwa. Wengi
walikaribishwa kwa mkopo, mwisho
wakawa wamiliki wa jumla.
Kwa nini umwambie huyo mtu kwamba
anaweza kukaa, wakati unajua siti ina
mmiliki wake halali? Kwa porojo za
kitoto, eti mnaambiana mfanye siri.
Kinachosikitisha ni kwamba ukisikia na
mwenzako naye kagawa siti yako kwa
mwingine, macho yatakutoka kwa hasira.
Si wakati wa kuchukia unapotendwa, bali
unatakiwa uache ubinafsi. Haliitwi penzi
bila kuwepo watu wawili. Lazima
uhakikishe unalinda la mwenzako ili na
lako lilindwe. Somo la mkuki kwa
nguruwe kwa binadamu mchungu,
linafundisha kuacha ubinafsi. Mfikirie
mwingine.
Kama ambavyo ubinafsi unavyowatesa
wananchi pale kiongozi mwenye
dhamana kiserikali anaposhindwa
kutimiza majukumu yake na kuamua
kushughulikia shida zake binafsi, huku
akitumia rasilimali za umma, ni kirusi
hatari kila upande.
Baba anapoamua kufuja fedha wakati
anajifahamu anayo familia
inayomtegemea, huo ni ubinafsi.
Anafikiria kutumbua yeye binafsi, wakati
anatakiwa kujenga msingi wa familia.
Anashindwa kujua kwamba fedha
anazotafuta si zake peke yake.
Kama anaona anatakiwa kutumia fedha
zake peke yake, basi hapaswi kujipa
mzigo wa kumiliki familia. Mtu
anapokuwa baba au mama, uamuzi wake
unatakiwa uwe kwa ajili ya wengi.
Kumaliza mshahara kwenye kumbi za
starehe ni ukatili kwa familia hususan
mtoto ambaye hakukuomba umlete
duniani.
Usijidanganye kwamba unajimiliki
mwenyewe. Wewe unamilikiwa na
familia yako, kwa hiyo una deni na
wajibu mkubwa kwa wale wanaohusika.
Kabla ya kwenda nyumba ya kulala
wageni na huyo unayemtamani, fikiria
kwamba unamilikiwa.
Baba au mama, anapokwenda hoteli na
mpenzi wa nje. Akakubali kuvua nguo na
kufanya mapenzi. Ajitambue kuwa
anachezea maisha ya watu wengine.
Kuna maradhi, kwa hiyo unatakiwa uwe
na afya njema ili wanaokumiliki
waendelee kupata huduma yako.
Unafahamu kwamba mapenzi yanaua.
Unaelewa kuwa unaposhindwa kuwa
mtulivu nyumbani, unaiba muda wa
familia yako. Kumbe sasa, fedha siyo zako
ila ni za familia. Unaweza kupata picha
kwamba viungo ni vyako lakini penzi si
lako. Ukilitoa ni wizi, ni dhuluma
iliyopitiliza.
zinavunjika na familia nyingi zipo kwenye
msoto kwa sababu ya ubinafsi.
Tunazungumza mengi lakini ukweli ni
kwamba endapo kila mmoja atafanikiwa
kuushinda ubinafasi, upendo utashamiri
kila kona.
Ubinafsi una matawi mengi. Mtu
anaposaliti, maana yake ametekwa na
tamaa binafsi. Anashindwa kutambua
kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa
hiyo anatakiwa kulinda penzi la
mwenzake. Hajui kama anachokifanya ni
dhuluma ya hali ya juu.
Ukweli ni kwamba unapoanzisha
uhusiano na mtu, maana yake umeamua
kumchagua yeye ndiye amiliki penzi lako.
Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine,
huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi
kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za
ndani ya mwili wako mwenyewe.
Kwa nini ukimfumania mwenzi wako
panachimbika? Ni kwa sababu
alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako,
kwa maana hiyo amekutendea dhuluma.
Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana
kwa sababu haki yako imetumika ndivyo
sivyo.
Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi. Umeingiwa
na jeuri kwamba unacho ndani ya mwili
wako, kwa hiyo unaweza kukitumia bila
kumshirikisha mwenzi wako. Hiyo ni
tabia mbaya mno. Kabla ya kusaliti, fikiria
utakavyoumia pindi utakaposalitiwa.
Kama inauma, ni kwa nini umtende
mwenzako? Je, umemuona yeye hana
moyo? Anza leo kukemea ubinafsi.
Popote pale utakapoona unachukua
nafasi, upinge kwa sababu ni adui
mkubwa mno kwenye mapenzi. Siku zote
usiseme "nipo", sema "tupo".
Unapozunguka, usiwaze "upo",
unatakiwa kuwaza "mpo". Hii itakusaidia
kulinda siti ya mwenzako kila
utakapokwenda. Hakikisha nafasi ya
mwenzi wako haichafuliwi au kutolewa
mkopo. Kama ilivyo kwenye soka,
wachezaji huchezea timu nyingine kwa
mkopo ndivyo na mapenzi ya sasa
yalivyo.
Ni kweli mtu ana mpenzi wake lakini
anavyojieleza anatoa picha kwa muulizaji
kuona kwamba aliyepo si muhimu sana.
Hii husababisha muulizaji aombe kukaa
na baadaye hukaribishwa. Wengi
walikaribishwa kwa mkopo, mwisho
wakawa wamiliki wa jumla.
Kwa nini umwambie huyo mtu kwamba
anaweza kukaa, wakati unajua siti ina
mmiliki wake halali? Kwa porojo za
kitoto, eti mnaambiana mfanye siri.
Kinachosikitisha ni kwamba ukisikia na
mwenzako naye kagawa siti yako kwa
mwingine, macho yatakutoka kwa hasira.
Si wakati wa kuchukia unapotendwa, bali
unatakiwa uache ubinafsi. Haliitwi penzi
bila kuwepo watu wawili. Lazima
uhakikishe unalinda la mwenzako ili na
lako lilindwe. Somo la mkuki kwa
nguruwe kwa binadamu mchungu,
linafundisha kuacha ubinafsi. Mfikirie
mwingine.
Kama ambavyo ubinafsi unavyowatesa
wananchi pale kiongozi mwenye
dhamana kiserikali anaposhindwa
kutimiza majukumu yake na kuamua
kushughulikia shida zake binafsi, huku
akitumia rasilimali za umma, ni kirusi
hatari kila upande.
Baba anapoamua kufuja fedha wakati
anajifahamu anayo familia
inayomtegemea, huo ni ubinafsi.
Anafikiria kutumbua yeye binafsi, wakati
anatakiwa kujenga msingi wa familia.
Anashindwa kujua kwamba fedha
anazotafuta si zake peke yake.
Kama anaona anatakiwa kutumia fedha
zake peke yake, basi hapaswi kujipa
mzigo wa kumiliki familia. Mtu
anapokuwa baba au mama, uamuzi wake
unatakiwa uwe kwa ajili ya wengi.
Kumaliza mshahara kwenye kumbi za
starehe ni ukatili kwa familia hususan
mtoto ambaye hakukuomba umlete
duniani.
Usijidanganye kwamba unajimiliki
mwenyewe. Wewe unamilikiwa na
familia yako, kwa hiyo una deni na
wajibu mkubwa kwa wale wanaohusika.
Kabla ya kwenda nyumba ya kulala
wageni na huyo unayemtamani, fikiria
kwamba unamilikiwa.
Baba au mama, anapokwenda hoteli na
mpenzi wa nje. Akakubali kuvua nguo na
kufanya mapenzi. Ajitambue kuwa
anachezea maisha ya watu wengine.
Kuna maradhi, kwa hiyo unatakiwa uwe
na afya njema ili wanaokumiliki
waendelee kupata huduma yako.
Unafahamu kwamba mapenzi yanaua.
Unaelewa kuwa unaposhindwa kuwa
mtulivu nyumbani, unaiba muda wa
familia yako. Kumbe sasa, fedha siyo zako
ila ni za familia. Unaweza kupata picha
kwamba viungo ni vyako lakini penzi si
lako. Ukilitoa ni wizi, ni dhuluma
iliyopitiliza.
No comments: