Leo tunakwenda kuitazama mada iliyopo mezani. Ndugu zangu, kama ingekuwa ni mtihani basi tunaweza kusema hakuna mtihani mgumu kufaulu kama wa kumpata mwenza sahihi wa maisha. Wengi sana wamefeli, najua wewe pia ni shahidi katika hili. Kwa kudhamiria au kutodhamiria, wengi hujikuta wameingia kwenye ndoa na mtu ambaye si sahihi. Ukifanya utafiti kwa sasa, watu waliofunga ndoa miaka kumi au zaidi iliyopita, utagundua kati ya wanandoa kumi, wanne au watano pekee ndiyo watakuwa wanafuraha na amani katika ndoa zao. Wawe na muda mfupi au mrefu tangu waingie kwenye ndoa, wanachokishuhudia kwa sasa ni tofauti na matarajio waliyokuwa nayo. Hii inatokana na nini? Wapendanao wengi wanapokuwa kwenye uchumba, huwa hawatumii vizuri nafasi hiyo kufanya ‘rehearsal’. Kwa kawaida, kuna ‘vimitihani’ vidogovidogo vingi huwa wapendanao wanapitia lakini kwa namna moja au nyingine wanakuwa wakivipotezea. Mtu anaamini mpenzi wake ni rahisi kubadilika mbele ya safari hivyo kumpa nafasi ya kuzidi kushibana. Wengine kutokana na kuzidiwa na nguvu ya mapenzi, hawana muda wa kuangalia hivyo vimitihani. Wanaongozwa na matamanio. Wengine wanaongozwa na tamaa ya vitu kama fedha na mambo mengine. Wanavifuga vimitihani kwa muda mrefu katika kipindi cha uchumba pasipo kujua ni jipu. Hawafikirii kabisa kwamba vimitihani hivyo vinaweza kuwa na madhara makubwa sana vitakakuwa jipu na kutumbuka wakati wakiwa tayari wameyaanza maisha ya ndoa. Hapa nazungumzia zaidi tabia, nidhamu, uvumilivu na hulka mbalimbali. Japo kuna vitu mtu anaweza kuvificha katika wakati wa uchumba lakini Waswahili wanasema nyota njema huonekana asubuhi. Ni rahisi sana kumjua mtu kama anafaa au hafai. Kwenye safari ya uchumba, kama umeona mwenzako ana tatizo la ulevi uliopindukia. Akishalewa anakuwa mkorofi, anaweza kukushikia panga muda wowote, ‘rehearsal’ yako ni kumueleza madhara na kumpa muda wa kubadilika kisha umpime kama amebadilika au laa! Usikubali kumuacha hivyo alivyo ukategemea aje kubadilika wakati tayari mmeshaingia kwenye ndoa. Akiingia ndiyo itakuwa balaa zaidi. Kama alikuwa kwenye uchumba alikuwa anakukosakosa kukukata, anaweza kuja kukukata kabisa mkiwa ndani ya ndoa. Hakikisha hulka hiyo unaitibu, ukishindwa usiendelee mbele. Ukikubali kuingia kwenye ndoa katika hali hiyo, tegemea maumivu huko mbele ya safari. Kama mwenzako ni malaya, hatulii nyumbani, rehearsal yako ni suala la kumbadilisha aachane na hiyo tabia. Mueleze kwa kirefu madhara ya tabia hiyo na umpe muda wa kubadilika, asipofanya hivyo, achana naye mapema. Mpime kuhusu uvumilivu. Kama anaweza kukupenda katika nyakati zote. Uwe kwenye shida au raha. Mpime katika nyakati ngumu. Ikiwezekana mtengenezee mazingira magumu, mpime kuhusu uwezo wake wa kukabiliana na magumu. Kwenye kipindi kama hicho, watu huweza kukimbiana. Unapompa mazingira magumu, akayaona hayawezi ni rahisi kukukimbia. Atamfuata mwingine ambaye hana mazingira magumu. Akifanya hivyo utakuwa umeshapata jibu. Nasema hayo kwa sababu uzoefu unaonesha. Wengi hukurupuka katika ndoa. Hawajiridhishi vya kutosha katika hatua za awali. Matokeo yake wanaishia kukutana na maumivu mbele ya safari. Hapo ndipo wanajuta, wanatamani kuzirudisha siku nyuma ili watengue ndoa lakini wanakuwa wamechelewa.
Si jambo la kushangaza kuwaona au kusikia mwanamke na mwanaume wanapendana. Yaani kila mmoja anampenda mwenzake na hivyo kuanzisha uhusiano.
Hapa nazungumzia upendo wa umoja na si wa wingi. Yaani wale wanaopendana huku kila mmoja akiwa hana mwenza mwingine. Inapotokea mtu ana mwenza halafu akapenda kwingine, huo ni usaliti na si mada yangu ilipolalia wiki hii.
MADA YENYEWE
Mada yangu inajieleza hapo juu; ukitegemea kitu penzi utaliona chungu.
Wapo watu ambao wanaingia kwenye mapenzi kwa sababu ya kupenda kutoka kwenye sakafu ya mioyo yao. Yaani mfano, mwanamke anatokea kumpenda mwanaume fulani pasipo na sababu yoyote. Huo ndiyo upendo unaoitwa wa dhati!
Wapo watu ambao wanaingia kwenye mapenzi kwa sababu ya kupenda kutoka kwenye sakafu ya mioyo yao. Yaani mfano, mwanamke anatokea kumpenda mwanaume fulani pasipo na sababu yoyote. Huo ndiyo upendo unaoitwa wa dhati!
Lakini wapo wanaopenda kwa sababu ya kitu. Mfano, mwanamke anatokea kumpenda mwanaume kwa sababu ana gari, ni msomi, ana pesa, ni mfanyabiashara, ana cheo serikalini, ni staa wa mpira wa miguu, ni mwimbaji mzuri wa Bongo Fleva au ana umaarufu sana mitaani.
HATA MBWEMBWE ZINA UPENDO?
Katika hili, nimewahi kushuhudia dereva wa bodaboda akipendwa na msichana kwa sababu tu ya uendeshaji wake wa bodaboda mitaani. Akiingia watu wanajua huyo ni Yusuf kwani mlio mkubwa, mwendo kasi akiwakwepa watoto wa mitaani, honi nyingi, breki za ghafla, sehemu nyembamba anapita kwa spidi na watu wanamsema vibaya kila siku; ‘huyu Yusuf huyu, iko siku.’
Kwa tabia hiyo tu, msichana mmoja aliondokea kumpenda sana Yusuf. Nilibaini hilo kwani Yusuf alipokuja kunyang’anywa pikipiki na bosi wake akawa hana mbwembwe tena na uhusiano wake na yule msichana ukafa.
Yusuf hakuwa na pesa za kumhonga huyo msichana, kwani yeye alikuwa akifanya biashara zake, sanasana yeye Yusuf ndiye aliyekuwa akipigwa tafu ya vijisenti.
LAKINI KUNA KUNDI HILI
Kundi ninalopenda kulizungumzia kwa leo ni lile la wanawake hasa, ambao wanaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume kwa dira zao.
Utakuta mwanamke anamkubali mwanaume kwa sababu tu amehisi atakuwa akipewa pesa nyingi. Au kama mwanaume ana duka, anategemea akimkubali atakuwa akipewa bidhaa za dukani bure.
Wengine ni wale wanaoingia kwenye uhusiano kwa sababu wanaume hao wana vyeo vikubwa au ni mastaa, hawa ndiyo ninaosema mimi kwamba, inapotokea pesa zimekata, hapewi kama zamani, inapotokea cheo kimeisha, inapotokea hali ya biashara inayumba hivyo hapewi mchele kama zamani ndiyo hujuta na kuliona penzi ni chungu.
KUWA KATIKA KUNDI HILI
Siku zote unapotaka kuingia kwenye uhusiano kubali kwa mwanaume ambaye kila ukipima upendo wako kwake unauona hauna sababu yoyote. Yaani humpendei pesa, humpendei cheo wala ustaa, bali unampenda tu! Ndiyo maana wahenga walisema penye penzi la kweli, mwenye chongo huonekana ana makengeza!
Ukipenda kwa mtindo huu, huwezi kuteseka kwani hali yoyote utakubaliana nayo.
No comments: