Love Story: AISIIIII……….U KILL ME 04

Related image

ILIPOISHIA
“Kweli Dany”
“Nitaghairi sasa hivi, chukua moja tu”
Maria akachukua noti moja kwa haraka kisha akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kunipiga mabusu mfululizo mashavuni mwangu, busu la mwisho lililo nisisimua ni busu la mdomo. Lipsi zake ndogo kiasi ila zenye unene kiasi, zilipogusana na zangu, nikajihisi kitu cha tofauti sana hadi ndani ya moyo wangu. Ni wanawake wengi sana ambao ninawabusu ila huyu Mariam amenipa msisimko ambao umenishangaza kwa kiasi kikubwa. Mariam akaniachia akataka kuondoka, ila nikamdaka mkono na kumtazama kwa macho ya matamanio nikatamani arudie japo kwa sekunde kadhaa kunipa busu kama hilo.
ENDELEA
“Nini tena mbona unanizuia?”
Mariam alizungumza huku akitabasamu, nikamtazama Mariam usoni mwake, nikazidi kugundua mambo mengi sana, hususani wa uzuri wake.
“Aaaha….hakuna kitu”
“Haya niachie nikaichenchi kwanza”
“Unajua zinapo chechiwa?”
“Ndio nachukua bodaboda hadi Mlimani City”
“Ahaaa sawa niletee zawadi basi?”
“Unataka zawadi gani?”
“Yoyote”
“Yoyote kweli?”
“Ndio”
“Sawa ngoja niende”
Nikamuachia Mariam, aliye anza kunipagawisha, akatoka chumbani kwangu na kuufunga mlango. Nikawasha feni langu na kupanda kitandani. Kila nilipo jaribu kuyafumba macho yangu, picha ya Mariam ikanijia kichwani na kukumbuka busu alilo nipatia.
“Huyu mtoto ana nini?”
Nilijiuliza huku nikijigeuza geuza kitandani kwa maana sio kawaida ya mimi kuweza kupagawishwa na busu tu, tena la msichana kama Mariam ambaye anaishi maisha ya kawaida tu. Kila nilipo jaribu kulala sikuweza mwisho nikaamua kunyanyuka kitandani na kusha tv kufwatilia mechi za mpira zinazo onyeshwa kila mwisho wa wiki.
Masaa yakazidi kwenda na kukatika. Hadi inatimu saa tatu kasoro, ndipo nikakumbuka kwamba sijaweka kitu chochote tumboni mwangu tangu nilipo kula na K2 asubuhi. Nikanyanyuka, nikachukua tisheti yangu kabatini, kabla sijatoka, mlango wangu ukagongwa.
“Nani?”
Sikujibiwa zaidi ya mtu huyo kugonga mlango tena, ikanibidi kupiga hatua hadi mlangoni ambapo, nikaufungua kwa tahadhari, nikamkuta Mariam amesimama huku mkononi ameshika mfuko mweupe wenye maandishi ya kijani ‘NAKUMATI’
“Tanataraaaaaaa suprizee”
Mariam alizungumza huku akiingia ndani, nikamtazama jinsi alivyo pendeza, hapo sasa asilimia za msukumo wa kimapenzi zikazidi kupanda moyoni mwangu. Suruali nyeusi aliyo ivaa, imeyabana makalio yake vizuri na kuzichonga hispi zake nene kiasi. Kjijiguo cha juu alicho kivaa, kiliyabana maziwa yake yaliyo simama vizuri, huku nywele zake alizo ziongezea na vigi lenye rangi ya gold zilishuka hadi mgongoni.
“Nimekufanyia shooping ya vitu vya ndani”
“Wacha wee”
“Ndioooo. Kwa maana natambua mabachela siku zote huwa hawanunui vitu, nikifungua friji naweza nikakuta halina kitu”
“Wewe umejuaje?”
“Nimejua tu”
Mariam akaweka mfuko juu ya meza, akapiga hatua hadi kwenye kafriji kangu ambako si refu kwenda juu. Akainama na kutazama ni vitu gani ambavyo vipo kwenye friji langu. Kitendo cha yeye kuinama huku makalio yake akiwa ameyaelekezea kwangu, nikabaki nikiwa nimekodoa macho. Akasimama huku akiwa ameshika sahani, akaniongelesha ila kusema kweli nikabaki nikiwa nimemkodolea tu macho wala nisielewe ni kitu gani ambacho anakizungumza.
“Dany si nakuongelesha”
Mariam alizungumza huku akiwa amenishika mkono, ndipo nikarudisha kumbukumbu zangu na kumtazama usoni vizuri.
“Ulikuwa unasemaje?”
“Ahaaa ina maana umesimama hapa na hapa hujanisikia?”
“Akili yangu nahisi haikuwa hapa”
“Mmmmm kwa hiyo ilikuwa wapi?”
“Tuachane na hayo, sema ulikuwa unasema…..?”
“Hizi soseji kakupikia nani?”
“Nimepika mwenyewe”
“Mbona kama sahani ni yakwetu hii?”
“Acha utoto unataka kusema kwamba sahani hizo zipo kwenu tu”
“Zimefanana”
Mariam alizungumza huku aking’ata soseji moja, akaaiweka sahani mezani, akaanza kupanga vitu alivyo leta huku vingi vikiwa ni vijwaji. Alipo maliza akalifunga friji na kunigeukia.
“Sasa hiyo ndio zawadi yako”
“Asante”
“Kuna matunda, soda, juisi za kopo, maziwa ya kopo. Ila niliogopoa kukununulia bia nikajua wewe si mnywaji”
“Na kweli mimi sio mywaji. Ila nina njaa nataka kwenda kununua chakula”
“Ohoo nilitaka nikujie na piza, ila nikaona uvivu kubeba mboksi wake”
“Haina shida”
“Basi twende wote”
“Wapi?”
“Si huko unapotaka kwenda kununulia chakula”
“Mama yako yupo?”
“Bado hajarudi”
“Poa”
Nikazima Tv, tukatoka ndani Mariam akatangulia nje na mimi nikamalizia kuufunga mlango wangu kisha nikaanza kutembea kwenye kordo ndefu, vyumba viwili kabla sijatoka nje kabisa nikasikia kilio katika chumba cha kushoto kwangu, huku sauti ya mwaume ikigomba sana.
‘Wanagombana nini hawa nao?’
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikipiga hatua mbili mbele kabla sijafika hata mlango wa kutokea nikastukia kumuona Asma akitoka mbio ndani kwake huku akiwa amejifunga kanga moja, akilia akionekana kukimbia kipigo cha mume wake. Sija kaa sawa mume wake naye akatoka kasi akiwa ameshika kisu mkononi mwake akielekea uwani ambapo ndipo alipo kimbilia Asma.
Bila hata ya kutaka kupoteza muda na mimi nikakimbilia uwani kwa kasi nikamkuta Jumaa akimfwata Asma kwa hasira haku kisu akiwa amekinyanyua juu. Kwa haraka nikamuwahi Jumaa na kumdaka mkono alio shika kisu.
“Jumaa unataka kufanya nini wewe”
“Niachie nitamuua huyu malaya”
“Mwanamke hapigwi hivyo Jumaa”
“Toka hapa na wewe msenge, ina kuhusu nini?”
“Nashukuru kwa matusi yako ila usifanye hivyo Jumaa”
Nikastukia Jumaa akinipiga kisukusuku cha kifua na kunifanya nimuachie mkono wake alio shika kisu, kitendo hicho kinanifanya nikasirike, nikamuangalia Asma aliye jibanza kwenye ukuta wa fensi ya nyumba yetu, asijue ni wapi atakimbulia.
Kwa haraka nikamuwahi tena Jumaa, mkono wake ule ule ulio shika kisu. Nikaukunja kwa haraka na kumgeuza Jumaa, nikampiga mtama mmoja mkali ulio muangusha chini kama zigo la kuni. Nikavikunja vidole vya viganja vya mkono wake ulio shika kisu na kumfanya Jumaa kutoa ukelele mkali.
“Utarudia tena kumpiga mkeo?”
Nilimuuliza Jumaa kwa ukali huku nikizidi kuvikunja vidole vyake kwa kuvirudisha nyuma. Asma na Mariam ambaye sikujua hata ameingia saa ngapi huku uwani walibaki wakiwa wamesimama huku wametukodolea macho. Jumaa kwa jeuri hakujibu kitu chochote na kunifanya nizidishe kuvikunja vidole vyake, hapo ndipoJumaa alipo zidi kupiga kelele kwa maumivu makali.
“Simpigi, Simpigi”
Jumaa alizidi kulalama kwa maumivu.
“Muombe msamaha mke wako”
“Ehee”
Nikazidi kumkunja kiganja chake na kumfanya Jumaa aanze kumuomba msamaha Asma aliye jkunyata kwa woga.
“Dany msamehe bwana”
Mariam alizungumza huku akinitazama usoni. Nikamuachia Jumaa huku nikumkazia macho makali. Taratibu Asma akamfwata mume wake na kunyanyua chini nilipo mlaza. Jumaa akanitazama na macho makali kisha wakaondoka na mke wake na kuelekea chumbani mwao.
“Twende zetu”
Mariam alizungumza, sikumjibu kitu chochote zaidi ya kutoka nje huku akinifwa kwa nyuma. Tukakatiza mitaa miwili na kufika kwenye kimgahawa kimoja ambacho wanauza vyakula mbalimbali.
“Agizia unacho hitaji”
“Ndio unazungumza na sauti nzito hivyo, au bado una mahasira yako?”
Mariam alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, nikashusha pumzi na kurudi katika hali ya kawaida. Akaja muhudumu, akatuuliza tutatumiua nini.
“Nahitaji nyama choma ya ng’ombe na bia”
“BIA…..!!?”
Maarim aliniuliza kwa mshangao, hadi muhudumu akastuka.
“Ndio kwani vipi?”
Mariam hakujibu kitu zaidi ya kuagiza kitu ambacho ana hitaji. Haikuchukua muda sana chakula kikaletwa pamoja na vinjwaji.
“Dany kumbe unajua kupigana eheee?”
“Kwa nini?”
“Nimeona jinsi ulivyo mkaba Jumaa, yaani yule kaka kila siku anakazi ya kumpiga mke wake”
“Hivi chanzo kinakuwa ni nini?”
“Wivu tu waa ajabu, jaani Jumaa hataji hata mke wake awe na marafiki wa kike. Ni ndani nay eye”
“Mpuuzi, nikisikia tena nitamlaza ndani”
“Utamlaza ndani?”
“Aahaa tuachane na hayo”
Jinsi Mariam anavyo kula chajula chake, nikawa na kazi ya kumchunguza uzuri wake. Kitu ambacho hakikuwahi kutokea kwenye maisha yangu ni kushindwa kumtongoza mwanamke ambaye nina muhitaji, ila kwa Mariam nikajikuta ninakuwa mzito sana kutamka kitu chochote. Kadri muda na msaa yanavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo zidi kuzigida pombe kushindana na hisia, nikiamini kwamba nikiwa nimekunywa sana nina weza kumtamkia Mariam kwamba nina mpenda.
“Dany inatosha bwana, usinywe tena pombe”
“Kwa…kwani hii ni bia ya ngapi?”
“Bia ya tisa”
“Ahaa tisa mbona chache”
Sauti yangu ilibadilika kabisa na kuwa sauti ya kilevi. Mariam akaninyanyua kwenye kiti nilicho kalia. Nikasimama wima, na kutoa toti za shilingi elfu kumi zipatano nane na kumkabidhi muhudumu, sikuhitaji kujua anatudai bei gani kwa maana kiasi nilicho mpa ni kikukbwa kuliko na kiasi ambacho tumetumia eneo hilo.
“Dany tuchukue bajaji”
“Bajaji….!! Bajaji ya nini sasa?”
“Umelewa wewe huwezi kutembea njiaa nzima na sasa hivi muda umekwenda”
“Kwani sasa hivi ni saa ngapi?”
Mariam akatoa simu yake mfukoni mwa suruali na kuangalia saa.
“Ahaa saa sita na nusu usiku”
“Sasa unasema usiku kwani sioni giza”
“Dany acha masihara bwana, tazama hapa umesimama tu unayumba yumba”
“Ahaa kwanza sihitaji kurudi nyumbani kwa sasa”
“Ahaa!!”
“Unashangaa nini sasa. Mimi sihitaji kurudi nyumbani”
“Sasa unataka kwenda wapi jamani Dany, kumbe ukilewa unakuwa na vituko kiasi hichi”
“Ahaa achana na mimi nataka kwenda kulala kwenye hoteli moja nzuri”
“Mungu wangu, sasa Dany unataka kwenda hoteli gani?”
“Wewe rudi nyumbani, mimi nakwenda kulala hotelini”
“Siwezi kurudi mwenyewe kama vipi nikudishie bajaji inipeleke nyumbani”
Mariam akaita bajaji moja, akaingia kwenye bajaji na mimi nikaingia kwenye bajaji.
“Ahaaa wewe si umesema unataka kwenda kulala hoteli nzuri vipi tena na huku?”
“Hei dereva tupeleke KC Hoteli”
“Sawa kiongozi”
“Dany mimi nakwenda nyumbani, nataka nikalale mapema kesho nina mtihani asubuhi chuoni”
“Unataka kulala mapema gani, wakati saa hizi inakwenda saa saba. Dereva endesha bajaji”
“Dany kumbe ukilewa upo hivi”
“Nipoje”
“Mmmm haya, ukifika hotelini dereva ananirudisha nyumbani”
Bajaji ikafika katika hoteli niliyo hitaji kufika. Nikamlipa kiasi anacho kihitaji. Nikashuka na Mariam naye akashuka.
“Unakwenda wapi?”
“Sirudi mwenyewe nyumbani”
“Rudi wewe, mama yako atakuchapa”
“Ahaa nimekuwa mtu mzima nirudi nisirudi hilo halimuusu”
Sikuwa na chakuzungumza huku moyoni mwagu nikiwa na furaha sana kwa maana naona Mariam anaingia kwenye kumi na nane zangu. Nikalipia chumba kimoja wala Mariam hakuzungumza chochote zaidi ya kukaa kimya akaanza kunifwata kwa nyuma, tukapandisha hadi gorofa ya pili kisha tukaingia katika chumba amacho nimelipia.
Kitendo cha kufunga mlango kwa funguo, nikamuwahi Maria kwa nyuma na kumshika kino, kwa haraka Mariam akakurupuka mikononi mwangu na kunigeukia. Akanitandika kofi moja zito la shavu huku akiachia msunyo mkali na mzito.
“Mimi sio malaya wa kujirahisha kwa mwanaume, na sijakuja hapa unitomb*, lala zako kitandani mimi nitalala hapa kwenye kochi”
Mariam alizungumza huku akiwa amekunja sura, akapiga hatua hadi lilipo sofa akajirusha na kukaa, huku akinikazia macho makali.
ITAENDELEA



No comments:

Powered by Blogger.