Nani hufika kileleni zaidi na nani mara chache, na kwa nini

TAFITI zaidi zinatoa mwanga juu ya ‘tofauti katika kufika kileleni,’ ambazo hutazama namna wanaume wanavyofika kileleni mara nyingi zaidi wakati wa kufanya mapenzi kuliko wanawake.
Lakini ni kwa nini tofauti hii ya kijinsia ipo, na kitu gani kinaweza kufanyika ili kufikia kileleni kwa usawa?
Pamoja na yote, kiasi cha asilimia 60 ya wanawake wanakabiliwa na matatizo yanayotokana na masuala ya kujamiiana, yanayosababishwa na tatizo sugu la kushindwa kufika kileleni.
Wataalamu wanajibu baadhi ya maswali.
“Makundi yote ya wanaume – mashoga, wale wenye jinsia mbili, na wale wanaopenda watu wa jinsia tofauti – hufika kileleni kuliko makundi kama hayo ya wanawake,” alisema David Frederick, Profesa msaidizi wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Chapman nchini Marekani, ambaye amebobea katika masuala ya kujamiiana kwa binadamu.
“Makundi ya wanawake wanaolala na wanawake wenzao hufikia kileleni mara nyingi zaidi ya wanawake wanaolala na wanaume, japokuwa si mara nyingi kama wanaume,” alisema. “Kinachowafanya wanawake kufika kileleni ni suala kubwa ambalo wengi wamekuwa wanakisia tu. Kila mwezi, magazeti, majarida na hata makala za kwenye mitandao hutazama njia tofauti ambazo zinaweza kuwasaidia wanawake kufika kileleni kwa urahisi zaidi. Ni suala la uandishi wa vitabu kabisa. Kwa watu wengi, kufika kileleni ni sehemu muhimu katika mahusiano ya kimapenzi.”
Kinachosababisha tafauti hiyo inaweza kuwa ni sababu ya kijamii au kutokana na mabadiliko ya kimaumbile kwa binadamu, Frederick alisema.
“Wanawake wanauwezekano mkubwa zaidi wa kushindwa kuridhika na hali fulani katika maisha yao kuliko wanaume, na na hilo huweza kuingilia maisha yao ya kingono. Hili linaweza kuathiri kuridhika kwao wakati wa kujamiiana na uwezo wa kufika kileleni iwapo watu wanakuwa wanapeleka nguvu zaidi katika mambo yanayowapa wasiwasi zaidi ya tendo lenyewe la ngono,” alisema.
“Lakini pia kuna unyanyapaa zaidi dhidi ya wanawake ambao wanakuwa wa kwanza kuomba ngono na wanaosema ni kitu gani wanapendelea kitandani,” alisema, na kuongeza, “kitu kimoja tunachofahamu ni kwamba kwa wapenzi wengi, kile wanachotamani wanashindwa kusema. Mpenzi mmoja anaweza kuwa anatamani kufanya mapenzi mara nyingi zaidi ya mwenzake. Katika mahusiano baina ya mwanaume na mwanamke, mtu huyo mara nyingi huwa ni mwanaume.”
Kwa hiyo, mwanamke anaweza kufanya mapenzi na mwenzi wake wakati mwingine akiwa hajisikii kufanya hivyo, na hivyo inakuwa ni vigumu zaidi kwake kufika kileleni, Frederick alisema.
Pia kuna wazo kwamba kufika kileleni kwa mwanaume kunasaidia kizazi, kwa kuwa uzazi unatokea iwapo mbegu zitatoka. Kwa wanawake, hata hivyo, hakuna uhusiano wa wazi baina ya kufika kileleni na uzazi, Frederick alisema.
“Lakini mamilioni ya miaka iliyopita, inaweza kuwa kulikuwa na uhusiano huo,” aliongeza.
“Nadharia mojawapo inasema kwamba kwa mababu zetu, kufika kileleni ilikuwa ni rahisi zaidi kwa sababu kazi yake ilikuwa ni kufanya yai la kike kutoka yaani ovulation. Hili hutokea kwa wanyama wengi,” alisema Frederick. “Mara moja kila mwenzi mzunguko wa hedhi ulianza kufanya kazi hiyo, hivyo kufika kileleni haikuhusishwa na uzazi kwa wanawake. Hili lilisababisha uwezo na wepesi wa kufika kileleni kwa wanawake kutofautiana kupitia mamilioni ya miaka na ndiyo maana kufika kileleni kwa wanawake kunatofautiana sana kwa wanawake kuliko ilivyo kwa wanaume.”
Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa wameumbwa kufika kileleni mara nyingi, alisema Elisabeth Lloyd, profesa wa biolojia na filosofia wa Chuo Kikuu cha Indiana huko Bloomington, Marekani, ambaye ameandika kitabu juu ya sehemu za siri na kufika kileleni wakati wa kujamiiana.
Urefu baina ya kinembe na mlango wa mkojo kwa wanawake, ambapo mkojo hupita, inaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kufika kileleni, kulingana na utafiti, uliochapishwa katika jarida la Hormones and Behavior mwaka 2011.
Lloyd alichambua taarifa kutoka tafiti tofauti mbili juu ya uhusiano baina ya maumbile na kufika kileleni kwa wanawake akiwa na mtafiti mwenzake Kim Wallen, profesa wa saikolojia na tabia wa Chuo Kikuu cha Emory.
“Tuligundua kuwa urefu baina ya kinembe na mlango wa mkojo, ambao unafahamika kwa jina la kitaalamu kama CUMD, inaonyesha iwapo mwanamke anaweza kufika kileleni wakati wa kujamiiana au hapana na iwapo urefu huo ni chini ya sentimita mbili, basi kuna uwezekano atafika kileleni wakati wa tendo hilo,” Lloyd alisema.
“Iwapo umbali huo ni mkubwa zaidi, iwapo unafika sentimita tatu, basi uwezekano wa kufika kileleni ni mdogo wakati wa kujamiiana,” alisema. “Huo ni ugunduzi wetu, ambao tayari umethibitishwa kwa kufanya majaribio. Hivyo hilo linamaanishwa kwamba, iwapo mwanamke atashindwa kufika kileleni wakati wa kujamiiana, si kosa lake au la mwenza wake. Sio kosa la mtu yeyote. Inawezekana inatokana na maumbile yake.”
Kwa mwanamke mwenye maumbile ya namna hiyo kuweza kufika kileleni, Lloyd anapendekeza kujaribu kutumia njia mbadala ya “kuchezea kinembe wakati wa kufanya mapenzi.”
Aliongeza kwamba kujifunza ni mara ngapi hufika kileleni imebaki kuwa ni eneo muhimu la utafiti kwa kuwa kufika kileleni kuna uhusiano wa moja kwa moja wa kuridhika kwa ujumla na uhusiano baina ya wapenzi.
“Wanawake ambao wana mahusiano bora kingono na wenza wao pia wana mahusiano mazuri zaidi na watu wengine kwa ujumla, na inathibitishwa kwamba ubora wa mahusiano yao,” alisema Lloyd. “Hivyo kwa ujumla, maisha bora ya kingono yanapelekea mahusiano bora zaidi, ambayo pia yanapelekea maisha bora zaidi ya kingono. Ni kama mzunguko.”
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
🔞Wakubwa tu: Pata mautamu ya chumbani live bila chenga
TAHADHARI WAKUBWA PEKEE NDIO WANARUHUSIWA KUBONYEZA HII LINK WATOTO KAA PEMBENI
No comments: