ACHA KUZUBAA!! Haya ndiyo Mambo yanayomfanya Mpenzi wako akukubali na Akupende wakati wote, Cheki hapa
Wewe kama mwanamme au mwanamke, najua unahitaji sana kulitunza penzi lako na kufanya lidumu milele kama wenyewe mnavyosema. Lakini wacha nikwambie kutunza penzi si ghalama kama watu wengi wanavyodhani, ila kuna vitu vichache ambavyo ukivifanya basi utadumu naye. Maana ingekuwa mapenzi ni ghalama basi maskini wasinge dumu kwenye mapenzi yao, lakini badala yake maskini ndiyowanaongoza kudumu katika ndoa Na hizi ni hatua 10, ukizifanya mtadumu.
(1) Kushukuru Kwa kawaida wasichana huwa wanapenda sana kusikiliza maneno yanayotoka midomoni, mwa wapenzi wao. Hivyo kumfurahisha mpenzi wake, ni lazima kumshukuru kwa chochote atakachokufanyia kwakusema hasante, hata kama ukimtuma akakuletee soda kwenye friji, au kitu chochote, hata kama alichokuletea si sahihi kumkosoa papo hapo ni bora kumshuruku na kumwambia taratibu.
KUWAPAMOJAMwanamke anapenda sana kuongozana na mpenzi wake, anapenda kuona kila saa akiwa karibu na ampendaye. Inawezekana mkaongozana wakati wa starehe, kama kwenda beach, disko, kwenye harusi au kuongozana kwenda kazi, sokoni kama Supermakert ,Kliniki wakati wa ujauzito au maradhi ya kawaida ni bora kufuatana. Wanasema kuongozana mara kwa mara kunafukuza maadui, kwani hakuna mtu anayeweza kuingiza chuki kwani hata yeye ataogopa.
KULALA Najua kila wapenzi wanakitu ambacho wanakipenda pamoja.Japokuwa kati ya hao, wengi hupenda kutizama Tv, filamu. Kama mtakuwa mnaangalia filamu, ruhusu mwenzawako, alale kifuani kwako, au sehemu yoyote ya mwili wako.Na pindi akipitiwa na usingizi usimwamshe, mwache alale hadi atakapoamka mwenyewe kwakuwa mwili pia unahitaji mapumziko. Kama kuna joto, iwe usiku au mchana, jitahidi umwache apitiwe na usingizi mwilini mwako, hii inasaidia sana kwani siku akilala peke yake, atajikuta akikukumbuka zaidi.
BUSU Wanasema busu au kiss huongeza ukaribu baina ya wapenzi. Hivyo penda kumkisi mpenzi wako, shavuni, kwenye paji la uso au mdomoni..
KUMVALISHA NGUO YAKO WAKATI WA BARIDINi vema kama kipindi cha baridiuonyeshe ni jinsi gani unamthamini, au unamfanya yeye kuwa kipaumbele zaidi kwako kwa kuchukua nguo yako, koti au shati na kumvisha au kumfunika.Yeye kutumia nguo yako sehemu ambayo unahisi hamnakitu kingine cha kumfunikia au kumkinga na joto, au baridi, jotoatakalo pata ni sawa na lile joto la mapenzi.
KUMSAIDIA KUOSHA VYOMBO Jamani, sio ujinga kumsaidia mpenzi wako katika suala zima la usafi wa nyumbani. Muwe mlishinda wote nyumbani, au mmerudi wote kazini au safari . Kama mwenzako ataingia jikoni,akapika na kuandaa chakula, ni vema ukawa unamsaidia kwa kuandaa vitu vingine. Pia ni vema ukawa unasafisha chombo ulichotumia wewe au yeye kama grasi ya maji ya kunywa au kijiko, hii inamfanya aamini kama yeye si mtumwa kwako, na akumbuke wema wako popote aendapo.
KUMSIFIA Unapokuwa na mpenzi wako penda kuchumnguza jinsi anavyovaa, anavyokula na chochote anachofanya. Siku ukiona ameongeza kitu cha ziada katika kile kitu cha kawaida basi msifie. Mwanamke au mwanaadam yoyote anapenda sifa, akipika wali nyama siku akiongeza na njegere mwambie, Chakula cha leo kitamu sana, akivaa nguo auakisuka mwambie mwambie umependeza. Basi atakupenda kwakuwa atahisi yeye ni bora zaidi ya hao unaokutana nao nje.
ZAWADI Jamani jamani!! Hebu nisikilizeni mimi, watu wanaogopa neno zawadi, zawadi si lazima mtu umpe nyumba au gari. Mpenzi wako anahitaji vizawadi, vidogo vidogo, kwa mfano kumnunulia ua la upendo, kumnunulia kadi, kumnunulia Bazoka, fenesi, embe, peasi, gauni, chungwa nakitu chochote ambacho unahisi unakimudu. Zawadi inaonyeshani jinsi gani unavyoweza kushea kile ambacho unakipata,hivyo hatojali ukubwa wa zawadi na atathamini zaidi hali yako kwakuwa anajua ipo siku atapata kubwa huku uzee unasogea.
KUMKUMBATIA Wanasayansi wanasema kumkumbatia mtu kunamsaidia kumpunguza mawazo, kwakuwa kunaonyesha ni jinsi gani unavyomthamani na hata kuonyesha unaweza kuwa sehemu ya suruhisho la tatizo lake. Hivyo ni vizuri kupenda kumkumbatia si kitandani pekeeyake, bali iwe beach, kwenye kochi, ndani ya gari sehemu yoyote ambapo panastahiri kumkumbatia mkumbatie. Hebuchunguza, watu waliopoteana kwa muda mrefu na wanapokutana, angalia kwenye misiba na sehemu zingine. Penda kucheza naye kwa kukumbataiana utaona matokeoyake.
KUAGANA NA KUKARIBISHANA Kama asubuhi unaondoka kwenda sehemu yoyote penda kumuaga mpenzi wako kwa staili ambayo wewe unaipenda, kama utachagua ya kumkumbatia, kushikana mikono, au kufanya ishara yoyote, ingawa njia nzuri zaidi ni ya kupigana kisi. Mkisi mpenzi wako wakati unarudi kazini, au wakati wa kwenda kazini, ni njia bora ya kukumbuka popote unapoenda. Na kufanya hivyo utakuwa umeweka ulinzi katika penzi lako.Jamani hapo ndiyo mwisho… kufanya hivi utakuwa umelilindapenzi lako.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
🔞Wakubwa tu: video kali zote na original app download chini
TAHADHARI WAKUBWA PEKEE NDIO WANARUHUSIWA KUBONYEZA HII LINK WATOTO KAA PEMBENI
No comments: