CHOMBEZO; STORI TAMU YA KUSISIMUA SITA KWA SITA 01

Image result for Corazon Kwamboka
Sita Kwa Sita

Mtunzi : Abdul Juma

.
.
.
Raha yake ni zaidi ya raha zote duniani hasa ukiendekeza  na inapozidi inapoteza thamani ya uwepo wako katika uso wa dunia haikifu wala haiboi bali uongeza hamasa ya kuendelea kuwa mtumwa wa kuitumikia mara Kwa Mara
Ndani ya maeneo ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam kilichopo Mlimani siku hiyo wanafunzi walikuwa wamejiandalia karamu kwaajili ya kusherekea kuingia mwaka wao wa mwisho kimasomo Kama ilivyo ada katika sherehe mbali mbali huwa hawakosi watu wa kuzamia katika sherehe ambazo hazikuhusiana nao wala kuchangia chochote kile hapa tunakwenda kukutana na  Osward mwenye umri wa miaka Ishirini na tano Kijana aliyekuwa anapenda sana starehe ila kilichokuwa kina mkwamisha ni suala la kipesa tu kwani kwao  anatoka katika familia duni ya Mzee Paulsen  Mzee anayejishughulisha na ufundi nguo ili watoto wake waweze kusoma, maisha ya nyumbani kwao hayakuwa mazuri hata kidogo kuanzia kula yao mpaka vaa yao  japo Baba yake alijibana ivo ivo  na kuhakikisha watoto wake wanaenda shule ili waweze kuja kumsaidia baadae na kujikwamua katika wimbi hilo kubwa la ukwasi ,kwao walizaliwa wawili tu yeye pamoja na mdogo wake wa kike Veronica mama yao mzazi alifariki Mara tu baada ya kuzaliwa Veronica kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mimba alokuwa ameupata akiwa na ujauzito wa miezi miwili wa Veronica , walilelewa Kwa shida na kusomeshwa mpaka Osward kuweza kufanikiwa kufika ngazi ya chuo na huo ndo ulikuwa mwaka wake wa kwanza akichukua Bachelor Of Science In Meteorology huku mdogo wake ndo kwanza akiwa kidato cha kwanza ,Mzee Paulsen mfuko wake haukuwa mkubwa kiasi hicho ila kutokana mwanae wa kiume Osward kusoma Kwa mkopo pesa alizokuwa akijibanabana alimlipia binti yake Veronica ili nae aweze kumaliza masomo yake ya sekondari , Osward alionekana mtanashati chuoni alijipenda kupitiliza lakini kuanzia mavazi mazuri aliyokuwa akiyavaa yote alikuwa akiazima kutoka Kwa wanafunzi wenzake hata sehemu ya yeye kulala ilikuwa ni kwa marafiki zake kutokana na Baba yake kutokuwa na uwezo wa kumlipia pesa ya bweni,
Leo ata lala hapa kesho ata lala kule hakuwa ni mtu wa kueleweka Kama ndege
Baadhi ya wanafunzi waliweza kumpachika jina la Masala kulangwa yaani Osward Masala Kulangwa , Siyo siri hakuchukiza ukimtazama Kama ndo siku ya kwanza unamwona lazima ungegeuka mara kumi kumi na kumtazama tena wasichana wa chuoni walijigonga Kwa utanashati aliokuwa nao kwa nguo za kuazima na jimwili lake lake atiii alilolibumbabumba kwa kunyanyua vyuma hakuna nguo alioivaa ikamkataa na kumkaa vibaya alionekana mtanashati wakati wote na hiyo ndo silaha yake kubwa aliyoitumia Kwa wanasichana hasa wale  ambao kwao ni mboga saba  hajui kuchezea fursa pindi inapojitokeza ukitaka kupotea njia kutana na Osward utajutraaa utachezewa na pesa utatoa
Siku hiyo ya sherehe Osward hakutaka impite Kama kawaida yake alizunguka Kwa marafiki zake na kuweza kuazima nguo ili akapate kuingia kwenye karamu hiyo isiyomhusu , ilipofika mida ya saa nane mchana watu walianza kuingia mmoja baada ya mwingine  ndani ya eneo la chuo cha mlimani hatimaye muda ukafika wazazi na wanafunzi wote wakiwa wamewadia na kuketi katika viti vilivokuwa vimeandaliwa tayari kwaajili yao , maandalizi yalianza , hotuba kutoka kwa wanafunzi , shukrani pamoja na pongezi kutoka kwa wazazi wenye watoto zao waliokuwa wakisherekea kuingia mwaka wao wa mwisho wa masomo yao muda huo hotuba zikiwa zinaendelea huku nyuma Osward anafanya mambo yake bwenini siyo kupishanisha kule vibinti mara ataingia na huyu baada ya muda anaingia na mwingine hakutaka kupoteza fursa siku hiyo aliitumia ipasavyo hasa kwa wanafunzi ambao hawakufahamu tabia aliyo kuwa nayo hakutulia sehemu moja muda wote alionekana akiangalia muda wake kupitia kisaa chake cha kuazima cha mkononi pamoja na kuchezea simu lake kubwa ya tachi lilokwisha jipasukia kioo, muda kidogo simu yake ikaita akaipokea akawa anatoka maeneo yale ili asogee Kwa pembeni apate  kusikilizana vizuri na mtu aliyekuwa akimpigia mara anajikuta anampamia mdada mmoja kwa bahati mbaya Dada yule alikuwa ameshikilia glasi iliyokuwa na wine alijikuta wine yote inaishia kumwagika katika gauni yake alokuwa ameivaa .


Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

 

  🔞Wakubwa tu: video kali zote na original app download chini
TAHADHARI WAKUBWA PEKEE NDIO WANARUHUSIWA KUBONYEZA HII LINK WATOTO KAA PEMBENI



No comments:

Powered by Blogger.