KAMA UKO KWENYE MAPENZI JUA KUWA MAISHA YAKO NI YAKO HAYAMHUSU MPENZI WAKO!
Ukishajua kua maisha yake ni yake na hayakuhusu unapaswa kujua pia kua maisha yako ni yako na sio tu hayamhusu mpenzi wako bali hayamhusu mtu mwingine yoyote yule, kwamaana hiyo basi unapaswa kuwa na malengo yako binafsi ya kiuchumi. Hapa ni bila kujali kuwa una mpenzi au la.
Nimeamua kuzungumzia kwa wale wenye wapenzikwakuwa wanawake wengi wanapokua katika kimuhemuhe cha mapenzi hujisahau na kuwaza mapenzi zaidi kuliko kuwekeza. Wanawake wengi wanapokuwa katika mapenzi hujihisi kama mabinti na kufanya mambo ya kimabinti mabinti, wanapoteza mkuda wao mwingi katika muonekano wao na kusahau kuwa maisha ni zaidi ya muonekano.
Kama una mpenzi naamini umefikia umri wa kuolewa hivyo acha kujiona binti na anza kuwa na malengo ya kiumeume. Waza mambo kama kumiliki viwanja, kujenga, kufungua biashara au kufungua biashara nyingine. Weka malengo yako kana kwamba hutakuja kuolewa hata kama jamaa kashajitaambulisha kwenu na unajua anakupenda kama malaika.
Hapa nazungumzia malengo ya kiuchumi, katika malengo ya kimapenzi unaweza kuwaza labda atanioa kwakuwa wanawake hawaamui sana kuhusu kuolewa, lakini hayo yasiingilie kabisa katika malengo yako ya kiuchumi. Waza vitu ambavyo vitakufanya ujitegemee wewe mwenyewe na wala usimuweke katika mipango yako.
Inawezekana akawa mtu mzuri akawa anakushauri vizuri, pokea ushauri wake pale unapoona unakufaa wewe na si kuona unawafaa nyinyi. Kama nilivyosema kama hajakuoa basi siwako hivyo asishiriki kufanya maamuzi yanayohusiana na maisha yako, ashauri tu lakini sio kusema mfanye mambo kwa pamoja, muweke malengo ya pamoja!
Masuala ya kupangiana baby tufanye hiki kwanza kabla ya hiki sijui hiki kabla ya kile usiyaendekeze labda kama anapangia pesa zake lakini si zako. Wakati mwingine hapaswi hata kujua mipango yako ya kimaendeleo na kamwe usipoteze hata sekunde moja kusimamia mambo yake wakati yako yakiwa juu ya mawe, unaweza kumsaidia kama binadamu wengine lakini si kwa kuharibu malengo yako.
Usiache fursa ikakupita eti kwakuwa una mchumba ambaye mnaweza kuja kuoana. Kuna fursa ya kusoma nnje ya nchi ichangamkie kama haeleweki, mume tu ndiye anaweza kukuzuia, kuna fursa ya kufanya kazi sehemu flani ambayo ina maslahi mazuri zaidi usiipoteze eti kwakuwa utakua mbali nayeye, kamata fursa na kama ni suala la umbali mtawaza mkishaoana.
Kama ni fursa ya kibiashara ichukue hata kama hapendezewi. Kwakifupi weka malengo yako binafsi ya kimaisha, mikakati yako binafsi na kamwe usipindishe malengo yako eti kwakuwa kuna uwezekano wa kuoana. Wapo watu ambao hupoteza muda katika uchumba sugu wa miaka kumi wakawekeza kila kitu kwa wapenzi wao na kuja kuachwa mchana kweupe na kuambulia kuzeeshwa tu, usikubali tengeneza maisha yako.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
🔞Wakubwa tu: Pata mautamu ya chumbani live bila chenga
TAHADHARI WAKUBWA PEKEE NDIO WANARUHUSIWA KUBONYEZA HII LINK WATOTO KAA PEMBENI
No comments: