Dalili njema, mbaya kwa mwanamke anayetokwa damu ukeni

Image result for KUTOKWA NA DAMU UKENI

MWENYEZI MUNGU alimuumba  kwa namna ya kipekee, ili kwamba kupitia yeye viumbe au binadamu wengine waweze kuzaliwa. Ili mwanamke aweze kupata ujauzito na hatimaye kujifungua, atahitaji kuwa na mabadiliko mbalimbali katika mwili wake. Mabadiliko hayo ni pamoja na kwanza kabisa ni awe mwanamke aliyepevuka kwa maana ya kuvunja ungo, lakini pia inahitajika mifumo yote inayohusika na uzazi katika mwili wake iwe katika hali ya afya iliyo nzuri.
Kwa upande wa mwanamke siku zote umekuwapo uhusiano baina ya ujauzito na kutokwa na damu sehemu za siri, kitendo hiki cha kutokwa damu pia ni ishara ya hali ya kiafya ya uzazi kwa mwanamke na kipindi hiki hujuitwa kipindi cha hedhi.
Mara baada ya yai la mwanamke kutengenezwa, huruhusiwa kusafiri ili liweze kuja kukutana na mbegu za mwanamume na kutengeneza ujauzito. Endapo yai hilo halitokutana na mbegu za mwanamume, litaharibika na kutolewa nje likiwa katika mfumo wa damu, hali hiyo au kipindi hiki ndicho huitwa hedhi.
Mara nyingi siku hizi za hedhi hutofautina baina ya mwanamke na mwanamke. Inawezekana hedhi ikawa ni siku tatu hadi tano. Katika kipindi hiki mwanamke anaweza kupata maumivu ya tumbo, homa, chunusi usoni na dalili nyinginezo. Dawa ambazo inashauriwa kutumia ni zile zitolewazo bila cheti cha daktari kulingana na hali iliyojitokeza mfano dawa za maumivu na kushusha homa.
Pia kuna nyakati ambazo mwanamke anaweza akaona hedhi kwa zaidi ya siku tano au zaidi mfululizo na ikaambatana na maumivu makali kiasi kwamba akawa anachukia kila ifikapo kipindi hiki. Inawezekana hali hii ikawa imejitokeza mara moja katika kipindi cha mzunguko au imekuwa ni hali ya siku zote, katika hili tahadhari inafaa kuchukuliwa kwani inawezekana ikawa ni dalili ya maambukizi yanayosababishwa na bakteria katika njia ya uzazi. Inashauriwa kutumia dawa za maumivu pamoja na zile zitolewazo kwa cheti cha daktari ili kupambana na maambukizi ya bakteria.
Kutokwa na damu wakati mwingine ni dalili ya mwili kutokuwa na uwiano mzuri wa homoni hususani za kike, hivyo matumizi ya vidonge vya homoni au vidonge vya uzazi wa mpango vimekuwa ni msaada mkubwa wakati huu.
Katika kipindi cha ujauzito, pia huwa inajitokeza kwa baadhi ya wanawake ambapo pamoja na kwamba ni mjamzito, anajikuta akitokwa na damu sehemu za siri, hii ni dalili ya hatari kwa mjamzito, cha kufanya ni kufika katika kituo cha tiba ili kuweza kuchunguzwa zaidi na kupatiwa matibabu stahiki.
Inawezekana pia ikawa ni muda ambao mwanamke hategemei kuona siku zake za hedhi au mfano ni mama au bibi ambaye tayari umri wake umeshapita na hayupo katika umri wa kushika ujauzito lakini akajikuta akitokwa na damu sehemu za siri, hii pia si dalili nzuri, inawezekana ikawa ni dalili ya maambukizi au saratani hivyo ni vyema akafika mapema kwa wataalamu kwa uchunguzi zaidi.
Dawa ambazo inashauriwa kutumia ni kulingana na hali iliyopo mfano maumivu au homa lakini kikubwa zaidi ni kutumia dawa kulingana na matokea ya uchunguzi wa kitaalamu.
Hali ya kutokwa na damu sehemu za siri kwa mwanamke ni kawaida, lakini endapo kuna dalili yoyote ambayo si ya kawaida ni vyema kuonana na wataaalamu mapema ili kubaini tatizo, hatimaye kupata ufumbuzi.

BASSA 0765203999

No comments:

Powered by Blogger.