Mambo 3 muhimu unayopaswa kumwambia mpenzi wako kila siku
Kutengeneza uhusiano wenye nguvu ni moja ya mambo yenye changamoto kubwa. Japo hakuna maelekezo maalum, kuna mambo machache na rahisi ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako yakaujenga . Weka desturi ya kusema mambo haya kwa mpenzi wako na muda mfupi tu mtakuwa couple itakayowapa wivu marafiki zetu.
1. Nakupenda ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.
2.Nilikuwa nakuwaza
Ni muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu moja. Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe.
3. Siku yako ilikuaje?
Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati ya muda mnaokuwa pamoja.
No comments: