NIPE NIKUPE

Image result for DEMU WA KIBONGO

BY BASSA MUSSA 0765203999

Hafiiiidhi..nikageuka kumtizama anae niita anakuja hata sijatafakali chochote kashafika na kunikumbatia huku machozi yakimtoka kwa fujo “Hafidhi mwanangu kumbe bado upo hai umerudi mwanangu, nikawa najiuliza maswali kichwani kwangu ndio huyu ni mama yangu mzazi lakini mimi nishakufa ina maana mimi na yeye basi tena inakuwaje anikumbuke na kwa nini nimejivika umbo hili na kujiita Hafidhi, nikapiga mahesabu ya faster na kucheza na akili za washkaji wanisaidie kumkana mama ya kwamba mimi siitwi jina hilo nikamtoa maungoni mwangu nikamshika mabegani kwa kumkazia macho na kumwambia “wee mama vipi kwani umedata au?"
“hapana sijadata wewe ni mwanangu Hafidhi, “mimi siitwi Hafidhi nahisi utakuwa umenifananisha tu, “Hafidhi mwanangu leo hii unanikana kweli mimi mama yako, “nikanyoosha kidole cha shahada kwa mbaali akawa anakuja mtoto wa kike huku akiita “kaka Sephu...wee kaka sephu, nikamuitikia naamu, “mama anakwita ukamchinje yule kuku kibwenzi, “ahaa mama nae bwana kazidi uchu nenda kamwambie kuku achinjwi yule, nikazidi kucheza michezo ya kiini macho kwa kumtengeneza mama yangu wa bandia akaja na kusema “wee Sephu kuku kagongwa na nyoka kule muai kumchinja kabra hajafa hee mbona huyu mama analia tena?" unajuwa nini mama huyu mama kanifananisha na mwanae sijui kapotea au vipi, “dahaa pore sana kwa kupotelewa na mwanao ilikuwaje kwani mpaka akapotea?" kwa sauti ya kwikwi mama yangu original akatoa full story, “kumbe mwanao amekufa tokea miaka 18 iliyo pita basi huyu ni mwanangu mimi anaitwa Sephu shaweji labda kafanania na mwanao tu, mama hakuwa na jinsi zaidi ya kuondoka huku akijifuta machozi nahisi hata begi lake akaliona zito kulivuta, nikawapoteza wale ndugu bandia kumbuka nina uwezo wa ajabu kwahiyo ni vitu vidogo sana kufanya hivyo kwanza nafsi ikaniuma kwa kumkana mama yangu mzazi lakini kama kulia kashalia kwenye msiba wangu inakuwaje aamini bado niko hai wakati washanizika siku hiyo nikiwa nimekaa kitandani nawaza na kuwazua jinsi ya kumpata nipe nikupe gafla kwenye pembe ya chumba changu akaingia mtu akiwa amebeba kikapu akaangaza angaza macho chumba kizima kisha akakiweka kikapu chake chini akapanda kitandani na kuanza kunitambuka tambuka huku akiimba “awilee tungoree awilee,,,tungoreee,,,awileee akanitambuka kama dakika kumi hivi kisha akanishika miguu na kunivutia chini ya kitanda laiti angejuwa mi nani asingefanya upumbavu ule anao ufanya tena mchana kweupe ananiwangia baada kunishusha akanilaza kifudi fudi akatoa kwenye kikapu sijui madawa gani na kuanza kunipaka paka mgongoni huku akikazana kuimba tu nikawa nimejikausha kimyaa
nione mwisho wake nini huyu mama, baada kumaliza akasepa na kuniacha pale pale chini nikataka kumuonyesha mimi noma na nikajuwa amerudi nyumbani kwake nikayeyuka vuu na kwenda hadi chumbani kwake nikawa nipo chini ya kitanda chake ile nafika tu na yeye ndio anaingia si akaniona unajuwa alistuka sana hakutegemea akabaki kujiuliza nani kamleta huyu huku, akatoka mbio kurudi chumbani kwangu kunicheki je nipo nami nikawai kufika tu akanikuta kwanza akajifikicha macho vizuri anaota au akaja kunishika sijui kunikagua kitendo cha kunishika tu nikamdaka pale pale nikamgeuza bata na kumfukuza kwa mateke mpaka nnje kuna mzee nikamsikia anasema "wee Nassoro njoo umkamate bata huyu huku, nikatoka nnje na kumkuta yule bibi kashadakwa kibaya zaidi aliyemkamata ana kisu tayali nikimcheki mchozi unamtoka dahaa, nifanye nini kumuokoa asichinjwe, nikanyoosha kidole mpaka kwa yule kijana na kujikuta anajikwaa akaenda chini puhu na kuanza kupiga kelele “yalaaa babuuuu mguuu wanguuuu...nakufaa....babu yake akatoka mbio mbio akiwa anauliza “nini tena mjukuu Wang?" mguu babuu,' “umefanyaje?" akawa anaushika shika na kuukanda kanda kwa kumnyoosha, “ayiiiiiiii...babu inaumaaaa...babuu niachee nikazama ndani nikiwa nacheka nazani hata hamu ya kuchinja bata hawakuwa nayo siku hiyo,
baada kupita siku tatu mama mwenye nyumba anatafutwa na mumewe watoto zake na ndugu zake wengine huku watu wakisema labda nipe nikupe kashafanya yake kitambo, wakati wanaangaika kumtafuta usiku na mchana mwenzao anawaona anawasikia kinacho mshinda kuongea tu kashakuwa bata siri naijuwa mimi peke yangu siku hiyo usiku wa manane nikaamua kutoka kwenda kumsaka nipe nikupe katika kupiga dolia zangu kwenye kichaka kimoja hivi nikasikia sauti kama ya mwanamama hivi akiomba asiuliwe “nisamehe nipe nikupe nimefanya hivi kuipata dawa tu kwa sababu nimezunguka kijiji kizima dawa hakuna ndio nikaziona katika shamba lako, “sio umeziona katika shamba langu nani umemuomba?"
“sikumuona wa kumuomba nisamehe, nikaweza kuitambua ile sauti kama ya mama hivi, nikawai faster asije akauwa nikatua mbele yao yani kati kati mama nikiwa nimempa mgongo nipe nikupe natizamana nae kwa mara ya kwanza nakutana na kiumbe huyu hakuna mfano wake kibaya zaidi wanakiongozi wao je huyo yukoje?"
akastuka kwa sauti ya kuunguruma akauliza “nani wewe?" niite Hafidhi j ikram, “khakha!Khalkha! kumbe wewe bwana mdogo umekuwa wa ajabu hivi kwanza pisha nimuangamize huyo mwanamke,' “hakuna anaye angamizwa hapa nimekuja kumlinda tu,' “kijana naona maumivu uliyopewa kipindi kile kuzimu hujatosheka sio sasa basi naita jeshi wakukamatee aiiiishiii ni kitendo cha faster nikamtupia kaa la moto mdomoni akabaki kuugulia maumivu akasepa mbio chezea mimi wewe utajamba nikamgeukia mama akiwa anatetemeka nikam beba na kumrudisha nyumbani kwa bibi huku nikimsisitizia arudi mjini haraka sana kesho yake hasubuhi kijiji hakifai hiki nikatoka nikiwa najongea gafla mbele yangu kuna mijitu miwili mireeefu ya kutisha,
Je nini kitaendelea

No comments:

Powered by Blogger.