Sifa za Mume/Mke mtarajiwa tuzitafutazo ndio zinazoibeba ndoa kweli!!!?

Image result for sifa za mwanaume handsome site:www.jamiiforums.com

Nimekua nikipitiapitia post nyingi humu ndani  watu kutafuta mke/mwanaume, lakini sifa zinazoanishwa hapo haziendani na zile post zingine zinazoelezea malalamiko na kero za ndoa. 
Yaani niseme labda mtu anasema mimi natafuta mke…. 1. Msomi mwenye degree 1 na zaidi. 
2. Awe mrefu na mweupe
3. Awe na wowowo yenye haja 
3. Asiwe anatoka maeneo ya mikoa flani na kabila flan
4. Asiwe single mother… nk


Na mke nae anatafuta mume… 
1. Awe na pesa za kutosha saana
2. Awe mrefu na handsome 
3. Awe na kucha ndefu za kuvalia sandle
4. Awe na gari
6. Awe na elimu kubwa zaidi 
7. Awe napendelea kutoa out… nk

Lakini ukija kwenye malalamiko ya ndoa na kero za ndoa, nasoma hapa vitu tofauti kbs, 
1. Mke wangu sio mwaminifu
2. Mke wangu mchoyo
3. Mke wangu ni mbinafsi hataki nijue kipato chake 
5. Mke wangu nimegundua ana uhusiano na x wake wa zamani
6. Mke wangu hataki kunipa unyumba… 

Na mke pia ana malalamiko ya kwake yanayofafa na hayo,.. 
Sasa najiuliza, .. Wakati wa kuchagua ulitangulia kuanisha uzuri na elimu ukasahau mambo ya msingi yanayoibeba ndoa na hivyo vyote ukapata, iweje leo unakuja kulalamikia vilivyo nje na sifa ulizotaka? Mimi kwa upande wangu nilijua ukipata mume handsome utavumilia yote hata akichepuka kwakua huo uzuri ndio ilikua ndoto na kiu ya moyo wako katika ndoa. 
Kama umepata mpododo usijali hata akichepuka kwakua ulitaka mwenye mpododo na umepata lakini hukujali na kuipima tabia yake ya uaminifu na hofu ya Mungu, usilalamikie usichokipendekeza wakati wa kuchagua,… 


[15]Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.

No comments:

Powered by Blogger.