Tatizo la mwanamke kukosa siku zake (hedhi)

Image result for kupitiliza siku za hedhi


Inafahamika kwamba mwanamke au msichana yeyote aliyepevuka kikamilifu, hupata siku zake za kutokwa na damu isiyoganda katika njia ya uzazi mara moja kwa mwezi. Dalili hiyo inaashiria ukomavu katika viungo vya uzazi.

Hata hivyo, kuna wakati mwanamke au msichana anapatwa na tatizo la kutokuona siku zake, hii ni dalili ya kuwepo kwa tatizo katika mfumo wake wa uzazi.
Ifahamike kwamba kukosa siku kwa mwanamke kumegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni wale wanaokosa siku zao kwa kawaida bila ugonjwa na kundi la pili ni wale wanakosa siku zao kwa sababu ya ugonjwa.
Binti au msichana huchukuliwa amekosa siku zake bila ya ugonjwa pale anapofikisha umri wa miaka 16 bila kupevuka huku akioneka kukomaa kwa viungo vyake vya uzazi.
Mwanamke au msichana aliyekuwa akipata siku zake kama kawaida hapo awali na baadaye ghafla kakosa siku zake kwa kipindi cha miezi 6 mfululizo, basi huchukuliwa kwamba ana ugonjwa au tatizo linalosabisha kero hiyo nyuma yake.
Mambo yanayosabisha mwanamke au msichana kukosa siku zake bila kuwepo kwa ugonjwa (hali ya kawaida na inayokubalika kisayansi) ni pamoja na umri chini ya umri wa kupevuka au kubalehe, kuwa mjamzito, kipindi cha kunyonyesha mtoto na kumalizika kwa umri wa kuweza kupata mimba ( menopause).
Kuwepo kwa kundi hili ni kawaida na kuna sababu yake, hivyo mwanamke hatakiwi kuhofu chochote kwani hayo ni mabadiliko chanya katika mwili wake. Magonjwa au matatizo yanayosababisha mwanamke aliyepevuka au kubalehe kikamilifu, lakini hapati siku zake kama kawaida au ghafla ni mengi, lakini kwa uchache ni pamoja na tatizo katika mayai au vitunga mayai yake. Hili ni asilimia 40, tatizo katika ubongo wake asilimia 19, tatizo katika mfuko wa uzazi ni asilimia 5 huku magonjwa megineyo yakichangia kwa asilimia moja.
Ni vyema kwa mwanamke au binti anayepatwa na tatizo hili kumwona daktari ili uchungizi ufanyike na matibabu yatolewe.

bassa mussa 0765203999

No comments:

Powered by Blogger.