FUNGUA FIKRA ....




Image result for NAPENDA UNAYO INGIZA

 niwasalimu nyote mlio fungua uzi huu kwa  mliyo onesha kwani hamkujua nini nimeandika ila natunaini hamta jutia.

Leo napenda tuangalie busara na maarifa yapatikanayo katika vitabu. Hii ni ni kwa jinsi nilivyo elewa, so kama kuna uelewa zaidi basi naomba uchangie kwa staha.

RICH DAD POOR DAR. Hiki ni kitabu kilicho andikwa na Robert Kiyosaki ambae ni muandihi maalufu wa vitabu vya uchumi na ujasiliamali. Katika kitabu hiki unaweza kujifunza mengi sana. Kwa kuanzia tutadukua busara chache katika kiabu hiki ambacho nimejikita zaidi katika kuielimisha juu ya namna ya kufanya maamuzi au machaguo hasa katika uwekezaji.
Sote tunakubaliana kuwa hatika maisha tunapata wakati mgumu sana wakati wa kufanya maamuzi. Tuendelee na Kiyosaki..

"Education is more valuable than money in the long run"
Nakubaliana na muandishi kuwa elimu itabaki kuwa muhimu kuliko pesa. Hapa nataka tuelewana kuwa kuwa na elimu ni tofauti na kuwa na ujuzi(professional). Mtu mwenye elimu akili yake iko tayari kujifunza kila ujuzi ambapo tumeona mara nyingi wenye ujuzi hubaki kuwa wafungwa wa ujuzi wao. Utakuta mtu kwakuwa amesomea sheria basi atabaki kuwa mwanasheria maisha yote na fursa pekee anayo weza kuitumia ni yakisheria tu. Hivyo elimu(uwezo wa kutambua na kujifunza mambo mapya )ni mihimu sana kiliko pesa.Kama umepata elimu ya kukusaidia kuwa na uelewa, unaweza kuwana ujuzi A ila ukajifunza kitu tofauti na kuweza kuwa na wigo mpana wa mafanikio.

"Unfortunately for many people school is the end, not the beginning"
Katika hili pia wengi tumeshuhudia watu wanapo maliza masomo yao hasa vyuo na kupata shahad zao huona kuwa wamefika mwisho. Hapa utakuta mtu kwakuwa lengo lake na kipimo cha mafanikio yake ni kupata degree basi atashinda sebuleni na rimote control hata mwaka mzima akisubiri ajira za serikali. Mtu wa namna hiyo kama angetumia uzoefu wa chuo kama njia yakuondoa uoga na kupata connection angeweza kuona baada ya kumaliza masomo sasa ni wakati wa kuanza maisha na sio kilele cha maisha. Mtu aliye elimika akiamua kuwa konda au machinga, anaweza kufanikiwa zaidi kwakuwa atatumia elimu yake kuziona changamoto na kuzitatua kisomi na kupenya katika ushindani. mfano, wewe ni konda wa gari la abiria ambalo hata wafanya biashara hutuma mizigi yao kutoka mjini yaani wanaweza kumfanya konda ndio mtu wa kwenda kuchukua mzigo. Hapo kwamfano yupo konda njinga ambae hutumwa kila siku na kuleta mzigo kwa uaminifu ila kasoro huwa haziishi kwa kila anaye muagiza yaani kama sio leo basi kesho anakosolewa au kama sio na Juma ni Joseph atamkosoa. Fikiria mtu wanamna hiyo anatumwa mzigo wa boks la dawa toka kwa Pharmacy kubwa mjini, hapa rist ni pamoja na kuleta brand ambayo sio yaani hata kama ni vidonge mfano Panadol kuna za kenya na Tz au India, pia kuna swala la kuleta dawa zilizo karibia expire date. Kama uonavyo hapa ni wazi ikiwa konda ni graduate ataweza kuhimili risk zote na kwa kufanya hivyo ataondoa lawama zote na makosa ya konda mjinga. Baada ya muda konda mjuvi atakua na nafasi kubwa ya biashaara kuliko mjinga. Huu ni mfano tu wa namna elimu inaweza kukupa mafanikio bila hata kutumia ujuzi(profession), yaani mwenye elimu ni mweledi kwa kila jambo, akitaka.

"Work to learn don't work for money"
Wengi tumekuwa na tabia ya kutaka malipo kwa kila tufanyacho na kujua kama inalipa kabla ya kufanya kazi. Binti mmoja aliwahi kunipigia simu akiomba nimtafutie kazi ya Hotel kwani ndicho alicho somea. Nilikuwa na machaguo mawili ya kumsaidia, moja ni kumuunganisha na rafiki yangu na lapili ilikuwa ni kumtafutia flem karibu na hospitali flani ambapo kuna fulsa ya kufungu mgahawa. Baada ya kufikiria ombi lake nikagundua kuwa hana uzoefu hivyo nikamchagulia fursa zote lakini nikaanza na fursa ya kwanza ili ajifunze na kukusanya kianzio/mtaji. Siku nilipo mpigia simu akanijibu "Bro kwanza hio kazi wanatoa shingapi!" kwa mshangao moyoni nikajiuliza, huyu si aliomba kazi bila kunitajia mshahara autakao!? Sijui kama nilikosea ila nilimdaganya nikamwambia wameshapata mtu, miaka imepita sasa mpaka amesha sahau alipo weka cheti chake yaani ni kama hakusomaga vile.Usitangulize maslahi mbele, kwanza uijue kazi kisha tafuta namna ya kuongeza maslahi.

"If you are moving even fire will not hurt you,....
Hii ni phenomena ya kawaida katika maisha yetu, fikiria mtu anaye tembea juani na mtu aliye simama au kukaa juani kisha jiulize ni yupi atakaye lalamika zaidi kuchomwa na jua. Au fikiria jamaa yako amekuacha sehem na kukwambia kuwa anatoka kidogo umsubiri anarudi, na huko aendako hajakaa kupoteza muda sehem, je, baada ya kurudi ni nani ataona kuwa jamaa kakawia? Hapa tunapata somo kuwa hata kama ujafanikiwa ni bora ukawa bize kinamna fulani na hauta hisi uchungu sawa na aliye bweteka. Kuna faida nyingi katika kujishugulisha.


SEHEMU YA PILI.
Kwanza nianze kwa kuwashukuru wote ambao wamechangia mawazo yako katika andiko hili, pia heshima zemwendee ndugu Kiyosaki kwani katika sehemu iliyo pita nilitumia sana kitabu chake na kuhusianisha elimu iliyomo na mazingira ya kwetu Africa. Katika sehemu hii ya pili nitaweka elimu kutoka katika vyanzo mbalimbali. Tunaendelea na hatua ya kuhamasishana na kutiana moyo katika kuchukua hatua za kimabadiliko. Karibuni...

Katika kujitutumua na kuchukua hatua za mabadiliko watu huwa tunasukumwa na mambo kama Dhamila/Ndoto. Kila mtu anatamani kuwa na mafanikio, kitu pekee kinacho tutofautisha ni mbinu na hatu za kuyaendea mafanikio hayo. Msomi anaweza kuwa na matamanio ya kufanikiwa kama mfanya biashara flani lakini na wakati mwingine( na ni mara chache) msomi anaweza kuwa na mafanikio makubwa zadi ya mfanya biashara.
Dhamira ya msomi kuwa tajiri itafanikiwa kwa hatua nyingi zaidi kuliko hatua za mtu asiye msomi. Ninapo sema haya ninamaana kwamba ili msomi awe na mafanikio kwa kupitia usomi wake lazima atimize hatua hizi
1. Kamilisha usomi wako vema (kuwa bingwa katika taaluma yako): Fikiria wewe ni daktari au mwanasheria msomi na umeamua kutumia uanasheria wako kujipatia kipato cha ziada wakati huohuo taaluma yako haitoshi kuwa shindani, matokeo yake utashindwa wakati wa mwanzoni kabisa na endapo utakuwa na rekodi ya kushindwa kesi kwa sababu huna ujuzi shindani basi safari yako ya mafanikio kwa kutumia usomi wa sheria haita kesha. Lakini unaweza kutumia upana wauelewa wako kwa kufanya kitu mbadala.

2. Jenga tabia au tamaa ya kuwa mjasiliamali. Baada ya taaluma yako kuwa imara na shindani, jenga tabia ya kuwa mjasiliamali. Leo naomba nitoe kile ninacho amini kama mbegu ya ujasiliamali. ....... Jiulize maswali katika kila jambo

Nitawezaje au njia gani mbadala??? Hakikisha hayo yanakuwa maswali ya kwanza katika kila wakati unapo kumbana na changamoto flani au hata unapo tafakari jamba lolote hata kama sio changamoto. Epuka sana kusema Hilo siliwezi au hayo yanawenyewe walio jaaliwa, hizi ni kauli kifungo tena za kushindwa. katika jambo lolote ukishasema siliwezi unajifunga milango ya tafakari na fikra na mwisho utabaki kuamini kuwa wewe ni dhaifu. Unapo kosa jambo au kukutana na jambo jaribu kuwa na njia zaidi ya moja ya kutatua, na usipende kupewa maamuzi na mtu mwingine aliye fikiri kwa ajili yako. Hata kama wewe ni mtumishi wa mtu kuwa na njia mbadala unayo amini na ikwa njia ya bosi imefeli kutatua jambo, toa mawazo yako kama ushauri kwa kuanza na Nadhai .... Labd... Hivi ingekuwaje kama..... Tujaribu... na zingine kama hizo. Katika hatua hii itatokea siku mawazo yako yanafanikiwa na itakujenga kujiamini na usishangae siku bosi anakuuliza utoe mawazo yako hata kabla hajafanya hitimisho. 
Kupitia tabia hii ya kujiuliza na kujihoji ipo siku utapata wazo ka kutatua changamoto flani na mwisho utakamata fulsa. Hii ni tabia tunatakiwa kuwa nayo hata kama sio msomi.

2 .Jiandae kuwa mfanyabiashara. Baada ya kuapata wazo mbadala la kutatua changamoto kwa kutumia taaluma yako, jiandae na uingie katika biashara. Mfano wewe umepata changamoto ya kutatua na kitu cha kwanza utajitatulia wewe mwenyewe kabla ya kumtatulia mtu yeyote na endapo hauta geuza innovation (uvumbuzi) wako kuutumia kibiashara hauta fanikiwa. Wapo watu wengi wanazo fursa lakini hawajaweza au hawataweza kuzitumia kibiashara. Sababu ya hayo yote ni UOGA. Baada ya kuwa mfanya biashara utafuata njia zote na kanuni za kibiashara ( leo sio wakati wake, ingawa ni vema uelewe kuwa sio kila ulicho kisoma shuleni kinaweza kutumika kila mahali, biashara Ulaya ni taofauti na Afrika au Dar ni tofauti na Kijijini huko Namtumbo, Mfano:- kijijini mwenyekiti wa mtaa au shehe au mchungaji au mtu mashuhuri, ukikosana naye unaweza funga biashara kwa kukosa wateja.(its real) so ujipange namna ya ku handle customers kulingana na eneo)

3.Ondoa uoga anza biashara. Ndugu zangu naomba niwaeleze ukweli kuwa ni kitu kigumu sana kuacha kazi. Wapo watu wamethubutu kuwa na biashara zinazo ingiza hata mara kumi ya mishahara yao lakini bado wamenaswa katika kuajiriwa. Mtu hataki kuwa Boss ila anataka kumtumikia Boss. Kwanza utaona ndugu hawako pamoja na wewe kukupa sapoti ili uache kazi na hata marafiki hawako na wewe kwa hilo. ILA unaweza kuacha kazi kwa kufuata kanuzu kadhaa (mda wake sio leo).

WASOMI NDIO WANAONGOZA KWA UOGA WA MAISHA
Sababu ya wasomi wengi kuwa waoga wa maisha ni kukosa kujiandaa mapema. Wasomi wengi wanapo pata ajira huanza kuishi kwa hadhi ya elimu yao. Mtu mwenye degree yake anataka avae kidegree, ale kidegree, usafiri wa kidegree na kila kitu kidegree. Ndio hatukatai msije sema ni wivu ila Kwanini uanze kuishi kidegree katika mshahara wa kwanza? Unakuta mtu anaanza na simu kali, tv LG flat, perfume nk, kila kitu cha thamani na unatumia mshahara. Hilo ni kosa kwani tayari umeitangazia jamii kuwa wewe ni wa hadhi flani kidegree na hauta weza kupoteza hadhi yako uonekane umefulia la hasha.
Mnakumbuka yule mkuu wa mkoa aliye tumbuliwa akalia kwenye television? alafu PhD !!! na amewahi kuwa mkuu Katavi na Moro!! yaani hajui kama hiyo ni mikoa ya wakulima tena wapo wanao mziti kipato pamoja na ukuu wake? yaani ni wakulia vile? alishindwa hata kujigawia machamba na kupata mkopo wa ma trekta kwa nafasi yake? mi sijui labda alisome u RC . huo ni mfano unao tuakisi wengi.
Kwanini uanze kukunua anasa badala ya amana? kwani hata hiyo kazi unajua haiwezi kuisha au ukapata janga na ikawa mwisho?

TAALUMA YAKO IKUPE KIBURI, kiburi?! (YES)
Hapa nitaelezea kwa mfano wa tajiri mmoja aliye anza katika utumishi. Huyu ni tajiri namba moja Algeria anaitwa Issad Rebrab mwenye utajiri kwa sasa wa USD 3.2 Billions. Huyu bwana anaeleza kuwa yeye ni Mwalimu kwa taaluma na alianza mapambano akiwa anaendelea na kazi yake mpaka pale alipo amua kwenda kujaribu biashara huku akiwa na matumaini ya kurudi katika aulimu wake endapo mambo yatagoma huko aendako. Inashangaza wasomi wengi ndio wanao ongoza kwa uoga wa maisha kuliko wasio wasomi. Wewe msomi taamuma yako ndio itakayo kubebe endapo hauta fanikiwa na kuanguka, angalau unaweza kujipanga upya. Angalau unakopesheka kuliko akina sisi na flani, angalau unaaminika na unayo adress ya kukupata, angalau unaweza kujifunza kitu kipya na ukachanganya na zako ukaja na wazo bora.

Hivyo, wasomi wanazo hatua kadhaa za kukamilisha ili kuwa wafanyabiashara walio fanikiwa kabla ya kuwa wafanya biashara. Msomi ukiyashinda haya unayo nafasi kubwa ya kufanikiwa katika biashara kuliko asiye msomi.



Kwa leo tukomee hapa, itaendelea. (--- bishara na uwekezaji, anasa na amana,Kuanza na kubadili biashara/gia, kuacha kazi(maandalizi,umri na wakati), kuikuza bishara katika soko la ushindani) tukutane baade..

No comments:

Powered by Blogger.