MKE WANGU HANIPI HAKI, PIA NI MVIVU NA HANA KAZI


Image result for MPENZI WANGU HATAKI KUNIPA HAKI YANGU

Si jambo la kawaida kwa mtu anayeshinda nyumbani siku nzima kuwa na usingizi wa aina hiyo. Hilo linaweza kuwa tatizo la kiafya na ushauri wangu ni kwamba umpeleke hospitalini akaguliwe. Asipopatikana na tatizo lolote basi mshauri awe akilala vya kutosha mchana ili ifikapo usiku aweze kuwa na nafasi yako.
Ndugu zake wamezua vijambo vikatuvuruga
Hujambo shangazi. Nimekuwa na mpenzi lakini tumekosana baada ya ndugu zake kuingilia uhusiano wetu. Wamekuwa wakimwambia kuwa simfai na kwamba watamtafutia mwanaume mzuri. Ninampenda sana na natamani awe wangu wa maisha. Nifanye nini?
Kupitia SMS

Kama mpenzi wako amekuacha kwa kufuata ushauri wa ndugu zake, hiyo ina maana kuwa ushawishi wao umeshinda nguvu penzi lake kwako. Mradi anaendelea kuwasikiliza na kuwaamini, hutampata tena kwa hivyo ni heri tu usalimu amri.

Sijui nitamwelezaje huyu namtaka?
Kwako shangazi. Kuna mrembo amevutia moyo wangu na sijui nitamwelezea vipi kwani hataki hata kunipa nafasi ya kujielezea. Naomba ushauri wako.
Kupitia SMS
Hata kama unampenda mwanamke huyo kushinda nafsi yako, juhudi zako ni sawa na kumkama maziwa kuku kwani hata nafasi ya kujielezea hataki kukupa. Unapoteza wakati wako bure. Achana naye.
Ninatamani sana kuacha kula udongo 
Hujambo shangazi? Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 48. Nimeingiwa na uraibu wa kula udongo. Natamani sana kuacha lakini kukosa kuula ni sawa na kukosa chakula. Nifanyeje?
KHALATI, Kwale
Hali hiyo mara nyingi hutokana na mwili kukosa madini fulani kwa kukosa kula vyakula vyenye madini hayo ambayo pia hupatikana katika udongo. Ushauri ni wangu ni kuwa umuone daktari ili akuelezee chakula au vyakula unavyofaa kula ili hamu ya kula mchanga ikutoke.
Jamaa zake ni chanzo cha matatizo yangu
Shangazi nimeolewa kwa miaka mitatu sasa na nina mtoto mmoja. Tatizo ni kuwa mume wangu huwasikia na kuwaamini sana jamaa zake kunishinda. Hivi majuzi mama yake alinichokoza na nilipomwambia akanipiga akidai mimi ndiye mchokozi. Nilirudi kwetu na sasa anaomba msamaha akitaka nirudi na kuahidi kuwa hatarudia. Nampenda lakini sina hakika kuwa nikirudi atabadilika. Nishauri.
Kupitia SMS
Kulingana na maelezo yako, nimeelewa kuwa bado mnaishi nyumbani kwa wazazi wa mume wako na ndiyo maana kumekuwa na tofauti za mara kwa mara kati yako na jamaa zake. Hali kwamba anakuomba urudi ni ishara kuwa anakupenda nawe pia unasema unampenda. Hata hivyo, suluhisho pekee la kumaliza mzozo kati yako na jamaa zake ni kutafuta makao yako mwenyewe. Mpe hilo kuwa shrati lako kumrudia.
Kimada wangu sasa adai ana mimba
Kwako shangazi. Nina mke lakini nimekuwa na uhusiano na mwanamke fulani kwa muda mfupi tu. Sasa nimegundua ana mimba na anadai ni yangu ilhali bado hatujashiriki mahaba. Anatishia kuwa nisipomuoa atanishtaki kortini. Nifanyeje?
Kupitia SMS
Ninaamini kuwa hilo litakuwa funzo kwako, kwamba mahusiano nje ya ndoa yanaweza kukutia mashakani. Kama una hakika mimba hiyo si yako, mwambie mwanamke huyo asubiri mtoto azaliwe kisha wewe naye mpimwe ukweli ujulikane. Hata akikushtaki, korti haiwezi kukuchukulia hatua yoyote kabla haijathibitisha kuwa mtoto ni wako.

No comments:

Powered by Blogger.