NILILALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI

Tokeo la picha la FUMANIZI
ILIPOISHIA
“Unamfahamu mzee mmoja anaitwa Samike? Ana nywele nyeupe, nyus…” kabla sijamaliza kuzungumza, kijana alibadilika na kuwa yule mtu wa ajabu aliyekuwa akinifukuza. Nikaanza kukimbia.

ENDELEA KUISOMA…
Nilikimbia kufuata barabara niliyokuja nayo. Naye alinikimbiza. Kama kawaida alishika upanga. Niliutazama kwa jicho la kuibia, tofauti na siku zote safari hii upanga...
ulisafishwa, ukanolewa vyema na ulikuwa na makali kuwili. Nilikimbia kuyanusuru maisha yangu.

Watu walinishangaa kwa jinsi nilivyokimbia. Mtu yule wa ajabu niliweza kumwona mimi pekee. Wao hawakumwona. Wapo waliosikika wakinibeza: “Unafanya mazoezi mchana wote huu!” wengine walizomea: “Huyoo! Kafumaniwaaaah,” hawakukosea, walikuwa sahihi. Ni kweli nilifumaniwa. Nilifumaniwa na kifo.

Nilipita Kamara nikikimbia kama bodaboda. ‘Rafiki’ mwenye upanga aliendelea kunifukuza. Nililoa jasho chapachapa. Sikujali, nilitambua jasho la mtu haliendi bure. Nikachanganya miguu. Mbio tu.
nikiendelea kukimbia, aliyenikimbiza alianza kutoa miungurumo ya kutisha. Nikajua leo nimekwisha… sitasahau.

Nilikimbia kufuata barabara niliyokuja nayo. Naye alinikimbiza. Kama kawaida alishika upanga. Niliutazama kwa jicho la kuibia, tofauti na siku zote safari hii upanga ulisafishwa, ukanolewa vyema na ulikuwa na makali kuwili. Nilikimbia kuyanusuru maisha yangu.

Watu walinishangaa kwa jinsi nilivyokimbia. Mtu yule wa ajabu niliweza kumwona mimi pekee. Wao hawakumwona. Wapo waliosikika wakinibeza: “Unafanya mazoezi mchana wote huu!” wengine walizomea: “Huyoo! Kafumaniwaaaah,” hawakukosea, walikuwa sahihi. Ni kweli nilifumaniwa. Nilifumaniwa na kifo.

Nilipita Kamara nikikimbia kama bodaboda. ‘Rafiki’ mwenye upanga aliendelea kunifukuza. Nililoa jasho chapachapa. Sikujali, nilitambua jasho la mtu haliendi bure. Nikachanganya miguu. Mbio tu.

nikiendelea kukimbia, aliyenikimbiza alianza kutoa miungurumo ya kutisha. Nikajua leo nimekwisha.

Nililiona gereza la Bangwe mbele yangu. Pia, niliwaona wafungwa wakiwa wamevaa mavazi yaliyoandikwa ‘magereza urekebishaji’. Na kitu kilichotia matumaini katika wakati ule mgumu, nilimwona mfungwa mzee mwenye nywele nyeupe, nyusi nyeupe, sharubu nyeupe… na alijaa misuli. Hakuwa mzee, lilikuwa pande la mzee!”

Nilikimbia kuelekea aliposimama. Sikufanikiwa hata kumsogelea. Askari alinitega nikadondoka chini mithili ya gunia la viazi. “Puuuuuh!” watu wakajaa kushuhudia sinema ya bure.

Nilijiokota nikasimama. Nilipotazama nyuma, aliyenifukuza sikumwona. Nilipotazama mbele zaidi yule mzee hakuwepo. Macho yangu yakatua katika paji la uso wa askari aliyenitega nikaanguka.

“Kijana kwa nini unapita ukikimbia hovyo eneo la magereza? Unampango gani? Kutorosha wafungwa?” alihoji askari kwa sauti ya kiaskari.
“Nisamehe mkuu. Shida zimenifanya nikimbie hovyo!”

“Ondoka hapa nisikuone.”

Niliondoka kimyakimya. Katika umati ule, wengi walishika simu zao na kwa vyovyote lazima walinipiga picha ili wapate mada katika mitandao ya kijamii. Nilijikokota taratibu kurejea sehemu yangu ya kupumzika.

Usiku sikulala. Nilitafakari hatma yangu dhidi ya mtu wa ajabu aliyeamua kuniwinda mfano wa simba mwenye njaa amuwindavyo swala.
Pia, niliwaza kama mzee niliyemwona ndiye Samike. Nilishindwa kugundua sababu ya kukamatwa kwa Samike. Kwa nini mzee yule afungwe? Au si yeye nimefananisha tu?

Nilitambua majibu ya maswali yangu siwezi kuyapata pasipo kwenda gerezani kuzungumza na mzee yule. Sikuwa mzoefu na mambo ya gerezani ila nilitambua kwamba, huwa kuna siku maalumu za kuwatembelea wafungwa na si kila siku unaweza kufika. Sikujali, niliitambua mbinu ya kufanikisha adhma yangu.

Nilifanikiwa kupata usingizi kiasi. Ulikuwa usingizi wa mang’amung’amu. Usingizi wangu ulijawa na ile shauku ya kuujua ukweli giza litakapopotezwa na nuru. Nilitabasamu kidogo kwa sababu mzee niliyekuwa nikimtafuta, kesho ningekutana naye katika gereza nililomwona ili ayamalize matatizo yangu.

Atafanikiwa kumpata mzee? Matatizo yake yatakwisha? Tukutane kesho… 

0765203999

No comments:

Powered by Blogger.