UKE KUTOA HARUFU MBAYA NA UKE KUTOA HEWA CHAFU (VIJAMBO)

 HOJA ZA KISAYANSI ZAIDI


Naomba nizungumzie tatizo la uke kutoa harufu mbaya, Kwani ni tatizo ambalo linawaathiri WANAWAKE wengi sana, na huwafanya wasiwe na Uhuru pindi wanapokua faragha na wenza wao, na huwafanya wasiwe na raha, kutokubali kuwa na mahusiano na mwanaume kwa kuogopa kusemwa vibaya na kupoteza kujiamini.
TATIZO HILI HUSABABISHWA NA YAFUATAYO
____________________________________________
1.Bacteria vaginosis
Kwa kawaida uke huwa na bacteria ambao huitwa lactobacilli, bacteria hawa ni wazuri na hawamletei shida yoyote mwanamke, bacteria hawa huulinda uke ili usishambuliwe na bacteria wabaya ambao ndio husababisha magonjwa. Kinachowezesha bacteria hawa waweza kukaa kwenye uke ni hali ya utindikali wa uke (vaginal acidity), Hali hii ya utindikali wa uke inapobadilika na kupungua kwa sababu yoyote ile husababisha bacteria hawa kupungua na hivyo hutoa nafasi kwa bacteria wabaya kukua kwa wingi na kushambulia afya ya uke hatimaye husababisha harufu mbaya (harufu hii kutokana na uchafu unaotengenezwa na bacteria hawa). Hali hii kitalamu ndio huitwa bacterial vaginosis. Ni mhimu kufahamu kuwa ugonjwa huu hauambukizwi kwa njia ya zinaa, Japo kua wanawake ambao wanajihusisha katika ngono wanakua ktk hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huu,pia wanawake wanaofanya DOUCHING (kujisafisha ukeni kwa kuingiza kidole) na wanaoshiriki mapenzi kinyume cha maumbile wapo kwenye uwezekano mkubwa wa kupata bacterial vaginosis.
2.Magonjwa ya zinaa(sexual transmitted diseases, chlamydia)
Ugonjwa huu wa zinaa unaoitwa kitalamu vaginal trichomoniasis ndio ugonjwa wa zinaa ambao unaathiri wanawake wengi zaidi kuliko ugonjwa mwingine wowote wa zinaa. Ugonjwa huu unasababishwa na protozoa anayejulikana kwa jina la Trichomona vaginalis. Na huambukizwa kwa njia ya ngono. Dalili za ugonjwa huu kwa wanawake ni kutoa majimaji yenye harufu kali yenye rangi ya njano -kijani, kuwashwa ukeni.
Gonorrhea kwa kawaida pia huweza kusababisha kutokwa na majimaji yenye harufu kali ukeni na huwashwa, Maumivu wakati wa kukojoa ,Maumivu wakati wa kufanya mapenzi, na Maumivu chini ya kitovu (japokua kwa gonorrhea wanawake wengi wanaweza wasionyeshe dalili yoyote kwa muda mrefu). Mara nyingi, inaweza kua vigum kwa Daktari kuweza kutofautisha baina ya magonjwa haya ya zinaa (hasa kwa mazingira yetu duni) :Hivyo basi mara nyingi daktari atatoa dawa kwa ajili ya magonjwa haya matatu ya zinaa pale anapofikiri kuwa mgonjwa wake anatatizo la ugonjwa wa zinaa.
3.Fangasi za ukeni (Vaginal candidiasis)
Fangasi za ukeni pia huweza kusababisha kutokwa na harufu kali ukeni, Japo kua si kwa kiwango Kikubwa sana kama sababu mbili za hapo juu
Pia, mara nyingi mwanamke mwenye tatizo la fangasi za ukeni atalalamika kuhusu kuwashwa zaidi kuliko harufu .
Dalili za fangasi za ukeni ni pamoja na kutoa majimaji mazito ya rangi nyeupe (kama Maziwa ya mtindi) yenye harufu, kuwashwa ukeni, pamoja na kusikia maumivu wakati wa kufanya mapenzi
Vitu ambavyo vinamuweka mwanamke katika hatari ya kupata fangasi za ukeni ni pamoja na kufanya "douching "(kujisafisha ukeni kwa kuingiza kidole ).
Kuvaa nguo za kubana.
Kuvaa nguo za ndani ambazo sio za cotton,
Kuvaa nguo za ndani ambazo hazijapigwa na jua /kupigiwa pasi
Usafi hafifu wa sehemu za siri,
Matumizi ya vyoo vya kukaa na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.
Je nini cha kufanya ili kujiepusha na harufu mbaya ya sehemu za siri kwa mdada?
_________________________________________
A. Epuka kusafisha uke wako kwa kuingiza kidole ukeni, uke usafishwe kwa maji ya baridi pasipo kutumia sabuni nakama kutakua na ulazima wa kutumia sabuni basi tumia sabuni ya pearl soap ya kuogea (Sio medicated soap)ijapo sabuni hazifai sana, na bila kuingiza kidole au kitu chochote ndani ya uke
B. Epuka matumizi ya madawa ya antibiotics kwa muda mrefu bila ya kuambiwa na daktari -kwani dawa hizi zikitumika kwa muda mrefu na bila ushauri wa daktari husabisha mabadiliko katika bacteria wa kwenye uke na kupeleka magonjwa na harufu mbaya.
C. Vaa nguo za ndani za cotton
D. Epuka nguo za kubana sana mwili
E. Nguo ya ndani ianikwe nje :sehemu ambayo itapigwa na jua (na sio ndani ya chumba) :au nguo za ndani zipigwe pasi kabla ya kuvaliwa,
F. Unapokua kwenye siku zako zingatia usafi na kubadilisha pedi za Neplily kama inavyotakiwa (mara 2/3 kwa siku )
G. Epuka kutumia vyoo vya umma vya kukaa
H. Jikinge na magonjwa ya zinaa
I. Epuka kuvaa nyingi na /au nzito wakati wa kulala, Vaa nguo nyepesi ambayo itaruhusu uke kupata hewa ya kutosha.
J. Jisafishe vizuri kila baada ya kumaliza haja ndogo
K. Kitu kingine ambacho ni mhimu sana kufahamu, ikitokea ukaona kuwa uke wako unatoa harufu, kuuosha kwa maji mengi na sabuni mara nyingi Sio suluhisho bali unazidi kuleta matatizo zaidi kwa sababu unazidi kupunguza idadi ya bacteria wazuri na kubadilisha hali ya utindikali wa uke na hivyo kukaribisha bacteria wabaya kwa wingi zaidi
Tumia Neplily sanitary pads tu kwa usafi.
L. Mwisho na mhimu zaidi ni kwa wanaume ,unapoona mwenza wako anatatizo hili usimseme vibaya ,usimkaripie au kumtukana :unatakiwa kutambua kua huo ni ugonjwa na umsaidie kuweza kuonana na wataalamu wa tiba kwaajili ya matibabu.
Namba mbili PAGE 2.
HEWA CHAFU KUTOKA UKENI
_____________________________
hili ni tatizo linalowakumba WANAWAKE wengi sana tena sanaa na wanashindwa wafanye nini kulitatua na pia wengi wao hawajuwi ni kitu gani kinasababisha hali hiyo.
Na tatizo hili zaidi hutokea mnapokua mnafanya mapenzi hasa ile style maarufu ya mbuzi kagoma kwenda kwa sababu mwanamke anakua ameinamisha kichwa chini kiuno juu hivyo huruhusu hewa hiyo kutokea ukeni.
Hali hii inakosesha raha na kutojiamini kabisa na saa nyingine hukufanya usitake kuwa na mwenzio .
Vilevile ni aibu haswa kwa wale walio katika ndoa mpya utatamani aridhi ipasuke utumbukie. Lakini hali hii tunasababisha wenyewe wali tena kwa uvivu wetu kwa vitu tunavyo fanya wenyewe.
SABABU ZINAZOPELEKEA KUJAMBA UKENI NA TIBA YAKE.
1.KUTOJUA KUJISAFISHA UKE
kwa wale wanawake wote wasiojua kusafisha vizur uke wao tatizo hili lazima liwapate kwa hali hiyo basi UKE inatakiwa kuusafisha vizuri na kwa umakini pia hakikikisha baada ya kuusafisha unafuta na kitaulo maalumu kwaajili ya kufutia na sio kanga ulio shindia kwenye mavumbi
2.UTUMIAJI MAJI MOTO
Ikiwa unapenda kusafisha uke wako kwa maji moto tatizo hili lazima likukumbe maana maji ya moto hulegeza uke na kuufanya uwe unatoa hewa chafu wakati wa kufanya tendo la ndoa na hata baada ya kufanya uke unatakiwa usafishwe kwa maji ya baridi na masafi hii inasaidia kubana misuli ya uke pamoja na kuwalinda bacteria ambao ni walinzi wa uke kwa ujumla.
KULEGEA KWA MISULI YA UKE
Pia ikiwa uke umelegea unasababisha vijambo kwenye uke kutokana na uke kuwa wazi.
ULALAJI NA SHAHAWA UKENI
kwa wale wanawake wasio jisafisha ukeni baada ya kufanya tendo la ndoa hali hii lazima iwakute na pia hawatakiwi kulala na shahawa ndani ya uke kunalegeza uke na hupoteza joto la asili la uke, Vilevile kulala na shahawa bila kunawa kunasababisha uke kutoa harufu mbaya na wakati mwingine husabisha kutokea kwa fangasi ukeni
USAFI PINDI UMALIZAPO TENDO LA NDOA
__________________________________________
unapomaliza kufanya tendo la ndoa mfute mmeo na wewe jifute, nendeni bafuni ikibidi muoge ,sio ukimaliza unageukia upande wa pili unakoroma na shahawa kibao ukeni, uke utapoa na kutepeta. Ukifika bafuni chuchumaa kwa muda ili kuruhusu shahawa zitoke kwa urahisi, jikamue kidogo ili shahawa zitoke vizuri, kisha osha uke wako kwa maji safi kisha jifute vizuri kwa taulo safi ili uke ubaki mkavu 0765203999

No comments:

Powered by Blogger.