Ishara 12 Za Kuonyesha Iwapo Rafiki Yako Amekuzimia
Ushawahi kuwa na rafiki yako, ama una rafiki ambaye tabia zake sikuhizi zimebadilika? Tabia zake zimekuwa tofauti na kama alivyokuwa zamani? Rafiki yako huyu umemuona amejeuka ghafla kukupa atenshen yake yote kwako?
Well, inawezakuwa amependezwa na wewe kiasi cha kuwa anatamani muwe pamoja. Labda amefall na wewe. Hizi hapa ni baadhi ya mambo unapaswa kuyaangalia kwa rafiki yako utambue iwapo amekuzimia au la.
#1 Wakati wanapojibu texts zako wanatumia muda mfupi sana ama muda mrefu kupita kiasi. Kama anakuchukulia kama rafiki yako wa kawaida basi texts ama jumbe zake huwa anakutumia kwa mwendo wa kawaida. Lakini kama iwapo ana hisia na wewe utaona ukimtumia jumbe anakujibu papo hapo, yaani chini ya sekunde moja :) , ama watapiga hesabu ya kila masaa 5 na dakika 24 ndio wakutumie text nyingine (yaani kuonyesha kuwa wanapendezwa wakiwa karibu yako)
#2 Wanakutumia text nyingi zaidi. Hii ni dalili moja kubwa kwa rafiki yako. Sana sana wao ndio wanaoanzisha maongezi na pia wanakutumia jumbe kwa wingi.
#3 Kila wakati wanakuuliza kama unapendezwa na mtu. Mara nyingi maswali haya watakuuliza wakati usiku wa kiza umewadia na kila kitu kimetulia, nyinyi wawili pekeenu mkiwa mnachat.
#4 Wanasistiza kuwa hawajapenda mtu kwa sasa. Kwa kawaida watasema haya yote kwa kuwa tayari washayalenga macho yao kwako wakiangalia iwapo utawakubali au la.
#5 Hawamkubali yule unayemzimia ama unayedeti. Ushawahi kuwa katika deti flani halafu rafiki yako kila wakati anamkashifu unayempenda? Ama kila wakati unapomtajia mwanaume unayemzimia anakasirika ama atakatiza maongezi yenu? Well, hii ni ishara ya moja kwa moja kuonyesha kuwa rafiki yako anakupenda wewe.
#6 Wanakualika muspend wikendi pamoja mkiwa pekeenu. Kama urafiki wenu pamoja na huyu rafiki yako ulikuwa wa kutangamana na marafiki wengine lakini ghafla wanakualika muspend Jumamosi nyinyi wawili pekeenu basi hio ni ishara ya moja kwa moja kuwa kuna kitu kimeanza kupikika. Mukiwa pamoja na marafiki zenu kuna maanisha kuwa atenshen yote itakuwa kikundini, lakini mukiwa nyinyi wawili itabakia nyinyi wawili. Ishara ya kuwa anakutaka uwe wake kabisa.
#7 Mara moja anaanza kukusifia kiundani. Mumezoea kuwa kila wakati mkiwa pamoja mnaongea kuhusu yule mvulana msiempenda ama habari za udaku, lakini hii siku moja ameanza kukusifia sifa za kama “Waa! nywele zako zinanukia utamu.” Halafu hawakwambii jambo hilo tena.
#8 Wanatafuta visababu vya kukugusa. Wakati ambapo umeangusha neno la kuchekesha, wanakugusa kwa kukugonga mkono. Wakati ambapo hawajakuona kwa muda wa siku nyingi anakukumbatia kwa nguvu kiasi cha kuwa unahisi joto lake. Kweli, hapo kunaweza kuwa na mambo mawili...aidha ni rafiki aliyezoea miguso ama kuna ajenda ya kuwa amependezwa na wewe.
#9 Watu wanawauliza iwapo mnadeti. Ama pia wanaweza wasiwaulize sababu wanachikulia nyinyi wawili mnadeti.
#10 wakati flani wanaleta mzaha nyote wawili mtoke out pamoja. Wanaweza kusema “Ok, kwa kuwa leo ni wikendi hatuna kitu cha kufanya. Wewe uko single na mimi niko single, si tutoke out lakini tuifanye kama deti vile, twende kwa kwa mkahawa halafu twende sinema tukajienjoy. Kirafiki?”
Hapa moja kwa moja hamaanishi kuwa ni mzaha bali anataka kujua reaction yako itakuwa vipi. Ukikubali basi atapata nafasi ya kukusogelea zaidi na zaidi.
#11 Wanataka mpige picha pamoja. Je hii ni ishara ya kuwa anakupenda? La. Kila siku watu hupiga picha mara kwa mara. Lakini kama wataanza kuiweka mikono kwa bega ama kiuno halafu siku ya pili unaiona kwa instagram, ni ishara ya kuwa anakujali – na labda ni zaidi ya kuwa marafiki.
#12 Wanakufanyia favour nyingi sana. Kwa mfano anakusindikiza hadi nyumbani kwenu hata kama mnaishi mtaa wa pili na pia kukulipia bili zako za hotelini. Anakusaidia kutafuta vitu vyako ulivyosahau pale ulivyoweka na kadhalika...
Well. Hizi ni dalili daharihi kuonyesha kuwa kuna kitu ambacho rafiki yako anahisi kwako. Je wewe utachukua hatua gani?
No comments: