Jinsi ya kuongea na mwanamke na kumuacha na hisia nzito juu yako
Wakati mwanaume anapojifunza jinsi ya kuongea na mwanamke, ni muhimu kazijua hizi tips 10 ili uweze kumuacha na hisia nzito / kali juu yako.
Lakini kuongea na msichana unayempenda kwa mara ya kwanza?
Hii ni mojawapo ya kitu kigumu ambacho mwanaume yeyote lazima apitie.
Lakini licha ya hivyo, inatubidi tu umfate kama unampenda.
Kwa wanaume wachache sana maongezi yao ya kwanza kwa mwanamke huenda vizuri na kufanikiwa kuyamaliza vizuri.
Lakini kwa wanaume walio wengi, maongezi yao kwa mara ya kwanza huwa mabaya na wakati mwingine hukata tamaa ya kufata
tena msichana.
[Soma: Jinsi gani ya kumfata msichana usiyemjua na kumvutia!]
Lakini tuangalie, ni kitu gani hutofautisha maongezi mazuri na mabaya?
Jinsi gani sahihi ya kuongea na mwanamke
Kama kweli unataka kmvutia msichana au group la wasichachana kwa maneno yako tu, kuna kitu
kidogo sana unahiyaji kukitilia maanani.
Wasichana wanapenda kufurahi muda wote wa mazungumzo.
Kadri unavyoweza kutambua kuwa msichana anayafurahia maongezi yako, ndivyo hivyo unaweza kumuingia moyoni mwake taratibu.
Kama kweli unataka kumvutia msichana wakati unaongea nae na unatamani akukumbuke fata hizi tips.
Jinsi ya kumfata msichana aliyep kwenye group
Jaribu kumteka kwa muda kwa kumuangalia machoni na ajue unamuangalia, baada ya hapo akishajua yupo mtu kama wewe unamuangalia, isipite muda mrefu mfate na jaribu kumuita ili muweze kuongea.Lakini licha ya hiyo, hatakama utaenda kujitambulisha mbele ya kundi alilopo kama haujui njia sahihi haitasaidia.
Unatakiwa kujua ni jinsi gani unaweza kuongea na kundi la wasichana na kuwatamanisha uendelee kuwepo nao.
Kama unataka kuongea na kundi la wasichana na unataka wakukumbuke na wawe wanakuongelea muda utakapokua umeondoka, fata hizi tips 10 zitakusaidia kupata mbinu rahisi za kuwapagawisha.
Jinsi ya kuongea na mwanamke na kumuacha na hisia nzito juu yako
#1 Jitahidi kuwafurahisha/kumfurahisha. Hili ni jambo kubwa kuliko lingine lolote ambalo linaweza kukupa point kubwa sana ya kuongea mwanamke/ kundi la wanawake. Kama unaweza kumwonesha mwanamke kwamba unaweza kumchekesha na kumfurahisha mpaka akasahau matatizo yake kwa muda, watatamani kila wakati wakuone ili uwafurahishe.
#2 Usiwapanikishe. Wanaume wengi sana hawaelewagi hiki kitu. Hupenda kujionesha kuwa wao ni bora zaidi na hivyo akifika kwa mwanamke / kundi la wanawake anaanza kuwauliza maswali ambayo yanawashangaza. Jaribu kuwa taratibu ukibadilisha mada zako kwa kuyasoma mazingira.
"Kwanini wasichana wengi wananikimbiaga?", "Ukiwa unakula hivyo utanenepa sana, unajua hilo lakini?". "Nimeipenda tishert yako, umeinunua wapi?", "Watu wengi wanasemaga naboa sana, hivi eti nabia?". Maswali ya ajabu kama haya yatawafanya wasichana wakukimbie kila siku. Wafurahishe bhanaa!...
#3 Wafanye waongee. Njia pekee ya kuwafanya wasichana waongee na wewe ni kwa wewe kuwahusisha wao na wajisikie maongezi hayo yanawahusu. Uliza maswali, au toa mada ambayo iyamgusa kila msichana na ataweza kuichangia / kuichokoza na wakaweza kuijadili kwa pamoja.
Hii inawafanya wote wajisikie pamoja na wewe. Na kama unaongelea kuhusu muziki fulani, au mwenendo wa mambo katika mitandao utajichukulia point na kuwaacha wakijiuliza maswali juu yako.
#4 Wamudu wanawake wote. Mwanaume wa ajabu atatilia mkazo kwa mwanamke mmoja tu aliyemtamani na kuwaacha wanawake wengine bored wakati mwingine wakitamani uondeke. Lakini mwanaume wa kweli, atawafana wanawake wote waongee, na kila mmoja atajihisi kama vile yeye kapendwa.
Usitilie mkazo kwa msichana mmoja tu kwenye kundi, labda iwe hivyo pale wanawake wote wanajua kuwa wewe una uhusiano na mwenzao. Jitahidi kuwatizama wote kwenye kundi, na kuwauliza maswali wote.Kumbuka kundi la wasichana ni kama umati wa watu, ukimpoteza mmoja jitahidi kufanya haraka usije wapoteza wote katika usikivu.
#5 Kuwa mchangamfu wakati wote. Tabasamu muda wote na cheka pale inapotokea kuna jambo lakuchekesha. Wanawake wengine hupenda sana mwanaume ambaye huonesha vituko pale anapojaribu kuelezea jambo la kuchekesha au kufurahisha. Hivi vituko havifeli kabisa kwa wanawake, lazima wakupende tuu.
#6 Kuwa mchokozi unapopata nafasi. Maneno ya kichokozi yanafaida zake kubwa sana, ila yana hatari yake sanasana pale unapoogea na mwanamke zaidi ya mmoja. Kama utani au uchokozi wako utamchukiza msichana mmoja, uta haribu maongezi yote. Lakini kama utatumia uchokozi kwa uangalifu, itawafanya wacheke na wafurahie maongezi.
Kwa hiyo mara nyingine ni bora ukatumia hata maneno ambayo mmojawapo aliyaongea na ukayageuza na kuyaweka katika mfumo wa kiutani na kutaka kumchimba aongee zaidi.
Hauhitaji kuropoka kitu chochote cha kuchekesha, badala yake tabasamu kichokozi kama anongea neno ambalo linaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Wasichana wengine wakiona tabasamu lako, mawazo yao mabovu yatawapeleka katika tafsiri nyingine ya neno kitu ambacho kitawafanya wacheke zaidi, hata bila ya wewe kusema neno lolote!
#7 Lugha ya mwili. Kuna vitu viwili vya msingi sana kuhusu lugha ya mwili wakati unaongea na wasichana, Lugha yako ya mwili pamoja na mana. Ukiwa unaongea na msichana / wasichana simama kiume na kwa kujiamini.
Lakini kw upande mwingine unatakiwa uangalie na uisome lugha ya mwili ya msichana unayeongea nae pia. Je,wanakutilia maanani?, au wanaonekana kuboreka na uwepo wako.Je, wanachezesha kichwa (ishara ya kukubaliana na wewe kwa kile unachokiongea?(nodding)), je wanacheka au kutabasamu?, je kuna mmojawapo kati yao anaangalia saa yake ya mkononi au kutizama mbali?. Lugha ya mwili hutoa maana kubwa na halisi zaidi ya maneno yenyewe.
#8 Watumie wasichana wengine kumvutia yule unayemtaka. Kama unataka kumteka msichana mmoja katika group lao, usimtilie yeye maanani sana na ukawatelekeza wengine. Wahusishe marafiki zake na uongee nao pia. Lakini wakati wote, kama utamsemesha yule unayemtaka jambo lifanye liwe zuri zaidi ya wenzake. Marafiki zake wakishakuelewa wao wenyewe kwa wenewe wataanza kukutongozea yule msichana na kumtamanisha kuhusu wewe jambo ambalo litamfanya awe anakuwaza zaidi ya wanaume wengine.
#9 Ondoka zako huku ukiwaacha na butwaa. Hii sehemu ni nzuri sana ya kuwaacha wakati bado walikuwa wakihitaji uwepo wako. Usiwagande sana wasichana mpaka waanza kupiga miayo au kulia njaa au kulalamika wamechoka. Siku zote ondoka wakati ukijua bado wanahitaji uwepo wako.
Kama utaondoka wakati bado walikuwa wakicheka na kufurahi, utawafanya waone kama wamepungukiwa na kitu na waukumbuke na kuutamani uwepo wako kila wakati. Na mmojawapo wa msichana lazima afunguke na kusema jinsi ulivyo mzuri na mwema!. Na hapo unatakiwa kujua kuwa umewashinda wote na umewavutia wote.
No comments: