Kushindwa Kutoa Huduma Kitandani

Tunapozungumzia mwanaume kushindwa kitandani tuna maana kwamba ni mwanaume kutokuwa na uwezo kusimamisha Mashine ili kuweza kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi unaotakiwa, au kuwahi kukojoa au mwanaume kusimamisha kwa muda mrefu zaidi ya saa moja na kushindwa kurudi kwenye hali yake ya kawaida.



Kama mwanaume anaweza kumaliza tendo zima la ndoa kwa muda wa dakika 5 au chini ya dakika 10 na kuwa hana uwezo wa kuendelea tena basi hiyo ni dalili kwamba kuna kitu hakiko sawa.

Data zinaonesha asilimia 10 ya wanaume mahali popote wana tatizo hili,ulimwenguni kuna wanaume zaidi ya milioni 150 wana tatizo hili na pia kila mwanaume anaweza kukutana na tatizo hili angalau mara moja katika maisha yake.

Nini husababisha?
Ili Mashine iweze kusimama lazima damu iende kwa wingi huko na kusababisha kuwa mgumu na kusimama na kuwa tayari kwa huduma.

Sababu kubwa ya mwanaume kushindwa kusimamisha  wakati wa tendo la ndoa mara nyingi huwa ni mawazo.

Pia Inawezekana ni dalili ya ugonjwa mwingine kama Diabetes.
Mwanaume anaweza kuwa na hofu kwamba hawezi vizuri Tendo na hii hupelekea kutojiamini na hatimaye Mashine kushindwa kabisa kusimama.
Pia Inawezekana ndoa ina matatizo na kupelekea kichwa kuwa na limzigo la mawazo na hatimaye kushindwa kabisa kusababisha utendaji wa kazi huko south pole.

Inawezakana mwanaume amefiwa na mtu wa karibu aliyekuwa anampenda.

Kuchoka

Pia stress

Kuwa na hatia ya kitu chochote.

Inawezekana mwanamke aliye naye havutiii kabisa

Kufilisika biashara au kufukuzwa kazi hupelekea kuwa na mawazo.

Kupungukiwa homoni zinazowezesha Mashine kusimama hasa umri ukienda sana.

Matatizo ya mirija ya damu kushindwa kusafirisha damu kwenda sehemu zote za mwili, hii uweza kusababishwa na magonjwa kama BP na arteriosclerosis.

Kuvuta sigara

Magonjwa ya nerves

Kufanyiwa upasuaji hasa ule wa prostate

Pia na Vyakula hasa vya Sukari.

Wanaume ambao huonekana labda ni maarufu sana katika fani zingine bado likija suala la kitandani ni kitu kingine hivyo mwanamke anatakiwa kujua kwamba lazima atoe ushirikiano wa kutosha kwani mwanaume anahitaji kutiwa moyo na mwanamke aliyenaye kwani Inawezekana ni mawazo kichwani mwake ndo hupelekea kushindwa.

Je, unaweza vipi kuepuka hili tatizo?
Hakuna kitu kinachoshushia mwanaume hadhi mbele ya mwanamke kama hili tatizo hivyo basi mwanaume akiona hili tatizo linajitokeza mara kwa mara kwanza ajiamini na kuangalia linaweza kuwa nini kimesababisha kama ni msongo wa mawazo inahitaji kwenda kwa washauri (counselling) na kama ni suala la kimatibabu awaone madaktari. 

No comments:

Powered by Blogger.