Mbinu 30 Rahisi Za Kutongoza Ambazo Unaweza Kutumia Kwa Mwanaume Yeyote

Kando na kuwa ni jukumu la mwanaume kumuapproach na kumtongoza mwanamke, ni muhimu pia kwa mwanamke kutambua kuwa aliyelala haamshwi. Usitarajie mwanaume awe na uwezo wa kutambua kuwa umependezwa naye au la. Ni wajibu wako angalau mara moja au nyingine uhakikishe unatuma ishara fioa kwa mwanaume ili naye pia awe na interest na wewe.
So utatumia mbinu gani mpaka mwanaume akutambue kuwa uko interested na yeye? Hizi hapa ni baadhi ya mbinu ambazo ni rahisi za kufanya ambazo zitamfanya mwanaume aanze ama afikirie kukuapproach mara moja.

#1 Msogelee. Halafu uvunje vizingiti vya macho kwa kumuangalia machoni kwa muda mrefu halafu kwa mdomo wake. Hii ni ishara fioa (fiche) ya kumuonyesha kuwa uko wazi kwa yeye kukupiga busu.

#2 Tafuta nyimbo ya utambulisho kwako. Cheza nyimbo ambayo itakuwa utambulisho wako na uhakikishe unafanya mazoezi kwa nyimbo kwayo. Halafu wakati utakapoiskia nyimbo hio ukiwa out ama katika sehemu flani, utajihisi confidence na poa – na kukupa ujasiri wa kusalimia yule anayependeza kati ya wote.

#3 Valia vipuli vikubwa na vya kumeta. Hii inavuta atenshen kwa shingo yako ya upanga – na pia ni mbinu fioa ya kuonyesha ngozi yako.

#4 Weka ubani ama ball gum kwa mkoba wako. “Unataka moja?’ ni tamshi rahisi ambalo litachangia mazungumzo.

#5 Onyesha upande wako wa furaha. Wakati umeenda sehemu ambayo umemwona mwanaume unayemzimia, ni bora uonyeshe ule upande wako wa furaha. Cheka na wenzako, furahia nk. Akikuona tu atakuappoach.

#6 Jifunze stadi ya kujigongesha mbele ya umpendaye. Wakati umemtambulishaunayemzimia, tembea ule upande alioko halafu ujigonganishe nayeye kana kwamba hukumuona. “Oh, samahani. Pole – huwa najisahau mara nyingi ninapozungukwa na wanaume wakupendeza.” Halafu jitambulishe.

#7 Panga deti ya hapo kwa hapo.  Mtext “Natamani chips na kebab!! Nataka uache kila kitu sahizi unipeleke katika mkahawa? :)”

#8 Mtese kiasi. Mfano: Wakati aliyekupendeza anakwambia jina lake ka mara ya kwana, sema, “Wasema?” ili apate kuegemea karibu yako aweze kujirudia kwa mara nyingine.  Halafu sema, “Nini?” huku ukitabasamu. Utakuwa umeyaanzisha maongezi yenu na ucheshi. 

#9 Jifanyie mazoezi ustadi wako. Ingiza mbinu yako uliyobobea ya kusuka mara moja au nyingine, kama vile wafanyavyo wahudumu wa kike hotelini. Amini usiamini hili litaongeza confidence yako wakati unapoongea na mtu unayempenda.
#10 Mwache akuone unamchungulia. Wakati na wao watakuangalia, tabasamu – itawapatia ile hamu ya kutaka kukuapproach.

#11 Kuwa interested.  Wakati anapoongea na wewe hakikisha kuwa unaonyesha interest yako kwa kumuuliza maswali ili na yeye apate nafasi ya kujibu.

#12 Hifadhi mzaha mmoja. Hii itakuhakikishia kuwa mazungumzo yenu hayatakwama mahali flani. Na pia iwapo utamfanya acheke basi atakukubali kirahisi.

#13 Mwagize mtoke out kibahati mbaya. Mtext “Leo usiku una plans gani?” Akikujibu, mwambie, “Samahani huo ujumbe ulikuwa unaenda kwa rafiki yangu – lakini hakuna shida, wewe kwaendaje?” Kumwambia hivi kutamfanye afanye ziada.

#14 Angalia nguo zake. Muulize timu anayoipenda, mchezaji, gemu nk kutokana na mavazi yake. Bila shaka atagundua kuwa umemnotice.

#15 Jipulize marashi kwa shingo yako. Hii bila shaka mwanaume unayemzimia atagundua tu.

#16 Tabirika wakati mwingine. Ule wakati ambao umejigongesha maksudi mbele ya mwanaume, hakikisha kuomba radhi kwako unakuzidisha kiasi cha kuwa atagundua unajaribu kufanya maksudi.

#17 Andika jumbe katika Instagram yake. “Hii picha inachekesha. Hivi ulikuwa unafanya nini hapa?” Wakijibu sema’ “Unapaswa kuniambia ana kwa ana. :) Wataka hii wikendi tumeet ama?”

#18 Usimjibu.  Jaribu kuitumia hii mbinu. Wakati ambapo anakutext, usijibu kila swali ambalo atakuwa akikuuliza. Acha maswali mengine yakielea. Hapa utakuwa unampa wakati wa kukufukuzia zaidi kutaka kukuelewa.

#19 Facebook sinema, vipindi ama gemu ambazo unataka kuziona.  Kama yuko interested na moja wapo ya hizo basi atapata kisababu cha kutaka mkutane.

#20 Mtambulishe mvulana anayependeza kwa marafiki zako. Mbinu hii itakupa nafasi kwa marafiki zako nao kutambulisha wavulana warembo kwako na utakuwa na nafasi ya kuongea nao.

#21 Pitisha karatasi iliyoandikwa kwa mkono katika party ambayo inasema, “Nilikuwa nakusalimia!” Ipitishe kwa mfuko wake  - hii inafanya maajabu zaidi kuliko text za kawaida.

#22 Msuke kabla hujamuona. Mtext umwaambie, “Unapaswa kuvalia ile tsheti ya blue leo usiku – inayafanya macho yako yapendeze.”

#23 Mtie wasiwasi.   Hivi ndivyo vya kufanya: Mara ya kwanza umpendaye anapokutext, mjibu, “Wewe ni nani?” Atakapojieleza,sema, “Lo! ntakosaje kukutambua?!? :)” Atavutika.

#24 Mpe wakati mgumu. Wakati ambapo anaonyesha dalili za kukutongoza usikubaliane na yeye hapo hapo. Msumbue na umpatie wakati mgumu mpaka ile siku utaona imefikia wakati wa kumkubali.

#25 Mfanye atake zaidi. Wakati ambao unataka kumuwish gudbye, fanya kumsogelea kana kwamba unataka kumbusu lakini nenda hadi kwa sikio lake na umwamnie’ “Usiku mwema.”

#26 Mtumie jumbe ya kumsuku pindi tu atakapokupatia namba yake ya simu. Hii itamshika kwa saprise. Mfano akikupa namba yake unaweza kumtext neno, “Una tabasamu zuri. Hii ndio namba yangu.”

#27 Waite. Wakati umenotice kuwa kuna mtu anakuangalia, mwonyeshe kuwa uko interested naye na utakuwa na confidence ya hali ya juu. Unaweza kutoa mzaha kama, “Tafadhali usuniambie kama  umeona kitu katikati ya meno yangu” Hii itamfanya acheke.

#28 Mtumie picha ya sinema flani. Halafu mwambie “Sinema ya saa kumi – wataka twende? Nitagawa bisi zangu ikiwezekana.”


Well, hizi ni baadhi ya mbinu ambazo unaweza kutumia iwapo unataka kumsuka mwanaume yeyote. Usiogope. Aliyelala haamshwi.

No comments:

Powered by Blogger.