Mjue Mpenzi ambae ni MBINAFSI na jinsi ya kumuepuka asiendelee kuumiza hisia zako.
Habari za leo ndugu msomaji na mfuatiliaji wa APP ya UWANJA WA MAPENZI,natumaini wewe ni mzima wa afya njema,kutokana na uzima tulionao basi hatuna budi kumshukuru mwenyezi mungu kwa huu uzima aliotupa.Leo nimeona nije nahii mada ya UBINAFSI kwenye mapenzi,najua wengi wetu mtakuwa mmekutana na wapenzi wabinafsi mara nyingi au mara chache,kama sio mpenzi basi utakuwa umeshakuatana na rafiki mbinafsi.Nimeamua kuandika mada hii kwa kuwa ni moja ya tabia ambayo inawaumiza watu wengi walio kwenye mahusiano .Uhusiano wa watu wengu umevunjika kutokana na h ii tabia hii ya ubinafsi.Unapoanza uhusiano ni ngumu sana kugundua tabia ya mpenzi wako kwamba ni mbinafsi lakini kadiri siku zinzvyozidi kwenda ndio taratibu unaanza kugundua jinsi mwenzi wako alivyo mbinafsi.Mwanzoni ni ngumu kugundua kwamba mwezi wako ni mbinafsi kutokana na penzi kuwa moto moto na wapenzi wengi wanapokuwa wanaanza mapenzi wanaficha tabia zao halisi lakini kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyomtu anapoanza kuonyesha tabia yake binafsi ya ubinafsi.
MTU AU MPENZI MBINAFSI(SELFISH PERSON) ni yule anayejijari yeye mwenyewe kwa kufurahisha nafsi hata kama anamuumiza mwenzie yeye hajali,hajali chochote kuhusu mwenzi wake anachohofia ni yeye kukosa furaha basi.Mtu mbinafsi si mtu mmbaya kwa tabia nyingine na anaaweza kuwa mtu mwema kwa kila mtu,lakini anakuwa mtu mzuri zaidi kama kuna kitu anatarajia kupata kwa watu wanaomzunguka.Mpenzi binafsi anajali furaha yake yeye tu kuliko kitu chochote kile.Kuna mambo mengi ya kumgundua kwamba mpenzi wako ni mbinasi. Tuangalie jinsi mpenzi mbinasi alivyo au tabia za mpenzi mbinafsi
MAENEO AMBAYO MTU MBINASI HUJIONYESHA KWA KIWANGO KIKUBWA
MAWASILIANO
-Katika swala la mawasialo mpenzi mbinafsi huwa anataka kutafutwa yeye tu,hakupigii simu mpaka wewe umpigie au hawezi kukutumia mesegi mpaka wewe umtumie ndio yeye akujibu,hata umpigie mara nne mfululizo yeye wala tena wakati mwingie ataanza kukulaumu wewe kwanini hujamtafuta wakati wewe umemtafuta zaidi ya mara mbili,hakuna jambo linalokela kama hili katika uhusiano,nafsi yako mara nyingi inakuwa inaumia kwa vitendo anavyokufanyia kwenye mawasiliano.
ZAWADI
-Ukiwa na mpenzi mbinafsi hata umpelekee zawadi mara mia yeye hata siku moja hatakupa chochote kile hata tunda la apple la mia tano hata kupa,au anaweza kukupa zawadi mara moja tu kwa mwaka tena mara nyingi kwenye siku yako ya kuzaliwa maana hana jinsi itabidi tu afanye hivyo,
UCHUMI
-Hili ni eneo kubwa analotumia mtu mbinfsi,yeye anachojali anapata nini kutoka kwako hasa swala la pesa,akiwa anataka pesa anakuwa mnyenyekevu kupindukia kila utakachomwambia yupo tayari kukusikiliza ,hata kama alikuwa hakupigii simu atakupigia,au kukutumia mesegi atakutumia siku hiyo tena zenye ujumbe mzuri wa mapenzi,lakini pale atakapopata kile anachotaka hutakuja ukae umwone ,wala hutaona simu yake mpaka wewe umtafute tena ahsante usitegemee utapata kutoka kwake ,wakati mwingine mpaka umuulize yaani hata ahsante husemi?
KUONANA
Pia katika hili eneo mpenzi mbinafsi yeye hana tyme ya kukuona mpaka umwambie mpenzi nataka kukuona,tena atakutolea sababu kibao,siwezi kukuona kwa sababu ya hili na hili,usipomwambia muonane yupo tayari kutokuonana hata kama mwezi ingawa nyinyi wote mnakaa katika jiji moja au sehemu karibu karibu,atakutafuta pale atakapokuwa na haja zake tu basi,jambo hili linaumiza sana,naamini kama umepitia utakuwa unajua uchungu wake.
No comments: