Sababu 6 Kwa Nini Hupaswi Kudeti Mwanamke Asiyependa Gharama

Kuwa na mwanamke asiyependa gharama ni ndoto ya kila mwanaume katika sanaa ya kudeti. Kwa kawaida wanawake aina hii hawana drama wala stress. Lakini je ni muhimu kweli kuwa nao?
Hebu jiweke katika hii hali: uko na mwanamke ambaye ukifika nyumbani tu ashakuandalia kila kitu, hakuulizi kwa nini umechelewa, hajibizani na wewe, hana time ya kukupa vikwazo kwa nini humpatii hela za kwenda kula bata wikendi wala pesa za kumnunulia viatu design latest ama kutaka kujua kila kitu unachofanya unapokuwa mbali na yeye. Yeye lake muhimu ni kukupa penzi ambalo huwezi kulisahau. 

Raha ilioje hii?


Hii ndio aina ya wanawake ambao wanaume wengi wangetamani kuwa nao maishani. Uzuri ni kuwa wanawake hawa hupatikana katika dunia ya sasa, na ni wengi mno. Wanawake aina hii wanatoa mtizamo wa kuwa na maisha ya raha mstarehe lakini ukweli ni kuwa hawa wanawake ndio wabaya zaidi. Wanakata kwa sehemu mbili, mbele na nyuma. Wataua hisia zako za kimapenzi na pia wataua matamanio yako.

Je, aina hii ya wanawake ni ipi?


Mwanamke asiekuwa na gharama hujitambulisha kama mwanamke asiyekuwa na drama nyingi kama wale wengine. Unaweza kumtambua na hizi tabia.

#1 Kila kitu chake huwa sahala/simple. Katika kabati lake la nguo utaona zile nguo anazozivaa, na bathroom yake haijapangwa vipodozi vingi ambavyo wanawake wengi hupenda kupaka wakati wa kujiandaa kutoka out. Hii inamaanisha mwanamke huyu hachukui muda mwingi kujiandaa kutoka nje. Dakika 10 zatosha kwake.

#2 Ni mchumi. Ya nini kwenda kujivinjari katika mkahawa ambao utatumia pesa nyingi ilhali mnaweza kuweka deti yenu kwa nyumba mkiwa mumenunua vinywaji vyenu mkichangana na viumio mlivyoviandaa wenyewe? Mwanamke aina hii anajali vile anatumia pesa zake na vile unavyotumia pesa zako kwake. Ni mwanamke ambae hahitaji kutumbuizwa kila jioni ama kununuliwa nguo za gharama ili afurahie maisha.

#3 Anapenda mahusiano ambayo hayana drama. Si lazima umpeleke mkahawa wa pesa nyingi ili umfurahishe, yeye yuko sawa na penzi unalompa. Hutawahi kumskia akilalamika kuwa hukumpigia simu jioni umjulie hali, na si lazima umpangie saprize kubwa ama kumnunulia gift wakati wa happy birthday yake sababu hatajishughulisha. Yeye ni kama beste na girlfriend kuchanganya pamoja.

Matatizo ya mwanamke asiyependa gharama.


Ijapokuwa mwanamke aina hii anaweza kuonekana mwanamke bora wa kuoa, unawezakuwa umekosa kujua matatizo ambayo yanahusiana na mwanamke aina kama hii. Hebu zama nasi tukufafanulie.

#1. Anaweza kutarajia pia wewe uwe mwanaume usiyependa gharama. Mara itokezee kuwa yeye hapendezwi na maisha yako, ama umependa kuspendi sana mara moja au nyingine? Kama girlfriend wako anapenda mambo yawe rahisi, unaweza kujipata umeachwa kwa sababu ya kujifanya diva sanaa.

#2 Kuna nafasi ndogo ya romance na upendo. Moja wapo ya sababu ambazo hufanya watu kupendana ni romance. Huyu mwanamke wako asiyependa gharama anaweza kuwa mzuri kukaa mbele ya runinga, lakini nafasi ya kuwa romance ama kutoka deti kujifurahisha mara moja au nyingine iko wapi? Usijisumbue kufanya mambo ambayo wapenzi wa kawaaida hufanya kwa sababu hatakubaliana na wewe.

#3 Relationship yenu itaboa haraka. Kwa kuwa hakuna kelele, kupigana, kukasirikiana kuhusu mahusiano, unaweza jipata katika mzunguko usiokwa na mwisho. Hakutakuwa na sapraiz ambazo zitasisimua moyo wako, hakuna hisia kutoka kwake ambazo zinaweza kuchangamsha penzi lenu. Kama nyote wawili mumetosheka na vile penzi lenu liko, na hamuwezi kufikiria jambo ambalo litawasisimua, basi kilichobakia ni kutafuta mwingine.

#4. Uhusiano wenu unaweza kuleta majanga. Kumkimu mwanamke asiyekuwa na gharama ni rahisi kuliko mwanamke wa kawaida. Hii inamaanisha kuwa hautapitia zile shida za kawaida ambazo wachumba hupitia – na huku kukosa maarifa kunaweza changia kuwe na majanga katika relationship. Kupigana, kukosana, kusumbuana huwa kunajenga mahusiano yenu kuwa bora zaidi. Kama umeamua kumchagua mwanamke aina hii kwa kuwa ni rahisi kumuweka, basi fahamu kuwa pia ni rahisi kumpoteza.

#5 Mahusiano yenu yanaweza kuwa mafupi. Kuwa na mwanamke asiyekuwa na gharama huwa kunafurahisha mara ya kwanza, lakini itafikia mahali flani ambapo kila kitu kitafikia ukingoni na mambo kuanza kusambaratika. Kama hakuna mmoja kati yenu atajaribu kuyafufua maisha yenu na kuyafanya yawe na mnato, basi bila shaka itafikia mahali flani utajutia kwa nini umemchagua mwanamke aina hii.

#6 Unaweza kumchukulia hivi hivi. Wanawake wasiokuwa na gharama ni wazuri kutembea nao kwa kuwa hawana hasara. Hii itakufanya wewe uwachukulie tu kawaida. Lakini unapaswa kufahamu ya kuwa si eti kwa sababu haombi chochote kutoka kwako basi unapaswa kuyapuuza matakwa yake katika mahusiano. Tatizo hapa ni kuwa unachukulia kila kitu kiko sawa kwake. Umemiss birthday yake? Umevunja deti na yeye kwa kuwa ulienda kuangalia gemu ya Arsenal na Man U na marafiki zako? Ni sawa. Ijapokuwa anaweza kuvumilia haya yote, hakuna sababu yako wewe kumchukulia kama mtu asiyekuwa na thamani.

Anyway katika hii dunia hakuna kitu kilichokamilika. Kila kitu kina dosari. Kama umejikuta uko na mpenzi aina hii hupaswi kumwacha. Jaribu kuongea na yeye na umpatie sababu za kwanini anapaswa kubadilisha tabia yake ama vipi? 

Mafanikio kwako.

No comments:

Powered by Blogger.