Sababu Za Kwanini Unamkumbuka Ex Wako Mara Kwa Mara

Imekuwa miezi kadhaa tangu uachane na ex wako. Kwa sababu zisizoweza kuepukika uliamua kukata uhusiano wako na mpenzi wako ili utafute maisha yako.

Lakini kuna tatizo ambalo linajitokeza mara kwa mara. Kila ukikaa ama kupumzika unamkumbuka ex wako. Na si kwa sababu unamtamani, la. Ex wako umeachana naye na labda sahizi uko na mpenzi mwingine. Tatizo ni kuwa huelewi ni kwa nini unaendelea kumkumbuka ex wako.

Well, sababu tunazo. Kuna mambo ambayo yanakufanya umkumbuke ex wako bila kukusudia. Na ni kama yafuatayo.

#1 Mko na marafiki ambao mnagawa. Nyote wawili mko katika group moja. Mara nyingi kwa kawaida huwa wapenzi wawili wanakuwa na marafiki wanaogawa. Rafiki yako anaweza kuwa rafiki ya mpenzi wako hivyo kuna kuwa na mshikamano flani. Kama hali kama hii imetokea kwako, kwa mfano katika mtandao rafiki yako anaweza kurusha picha akiwa na ex wako hivyo unaweza kukumbuka hisia na upendo ambao ex wako alikuwa akikuonyesha.

#2 Nilikuwa nikiagiza chakula changu hapa. Je unakumbuka wakati ex wako ulikuwa ukienda nae katika hoteli flani kila wakati kula chakula flani? Wazikumbuka zile hisia nzuri ambazo ulikuwa ukizipitia huo wakati?

Hio huwa ni kawaida. Kukumbuka kitu ambacho ex wako alikuwa akikufanyia haimaanishi kuwa bado unamtamani. Inakuja tu kwa kuwa unakumbuka ukumbusho ambao ulikuwa unapenda haswa wakati mlipokuwa mnakula pamoja.

#3 Nilikuwa hapa mwaka jana. Nikiwa na ex wangu. Na leo umekuja katika sehemu hio hio na kumbukumbu za wewe na ex wako zinajitokeza. Ni kawaida kuwa na kumbukumbu haswa iwapo wewe na ex wako mlikuwa mnapenda kutembelea hio sehemu mara kwa mara.

#4 Unamwona ex wako kila mahali. Ni vigumu kumuona mtu ambaye umekuwa ukimjua halafu usiweze kuwafikiria katika hali moja au nyingine. Kama umeenda katika mkahawa ukakutana na ex wako, ama anafanya kazi katika shirikia flani na ni njia unayoipitia kila siku basi ujue huwezi kumuondoa kwa akili yako.

Kumkumbuka ex wako na kukumbuka mambo matamu na mazuri ambayo mmekuwa mkifurahi ukiwa na ex wako ni vitu viwili tofauti. Kama ni kumbukumbu ambayo imekuja tu kwa ghafla basi isiwe jambo kubwa la kutatiza. Itakuwa ni akili yako tu ndio ilijaribu kukukumbusha yale mambo mazuri ambayo ulipitia ukiwa na ex wako.

#5 Kizazi cha mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ina manufaa na maafa. Kwanza ni kuwa unajiunga na karibu kila mtu ambaye unajuana naye. So wakati ex wako anapost kitu flani kwa mtandao, fikra zako zinakuja kutaka kujua ni kwa nini ex wako amepost kitu kama hicho online.

Hii ni kama tu vile marafiki zako katika mtandao wangependa kujua umemaanisha nini baada ya kupost status flani. So fikra zao ni kama tu zile fikra za marafiki zako katika mitandao ya kijamii, ikijumlisha ex wako.

#6 Nguvu za hisi. Miili yetu imeumbwa kiajabu. Unaweza kunusa ama kuona kitu halafu ukakumbuka jambo flani. Hivyo hivyo unaweza ukakumbana na harufu ya marashi flani halafu ghafla ukaanza kumkumbuka ex wako vile alivyokuwa akipenda marashi hayo.

So usichukulie uzito kwa kuwa hatuwezi kukontrol mawazo yetu, kwa sababu akili yako itakuwa inajaribu kukukumbusha mambo ya zamani.

#7 Vitu ambavyo unamiliki. Ukiachana na mpenzi wako haimaanishi kuwa kila kitu ambacho amekupatia unafaa kumrudishia, la. Kuna wakati unawezakuwa na nguo ambazo umenunuliwa, simu ama PS4. Hivi huwezi kuvitupa.

So sahizi umeachana naye halafu ukakumbuka unashikilia kitu ambacho umepewa na ex wako. Hii haimaanishi kuwa kumiliki vitu hivyo kunamaanisha hutaki kumsahau ex wako.

#8 Mazungumzo ya miguso ya moyo. Unaweza kuwa na marafiki zako halafu uanze kuwapa ushauri nasaha. Halafu katika mazungumzo yako inakuja kwamba unawashauri kulingana na experience umepitia ulipokuwa na ex wako. Kama itakuwa ngumu kuongea kuhusu experience zako na ex wako basi inamaanisha kuwa una chembechembe za hisia na ex wako. Lakini kama utaongea bila wasiwasi bila kuzua hisia basi utakuwa uko sawa.

Kumbuka kuwa kumkumbuka ex wako hakumaanishi kuwa unamtamani ama uko la feelings na yeye. Kukumbuka zama za kale na kutamani zama za kale zirudi ni mambo mawili tofauti. Kumbuka haya wakati fikra za ex wako zitakuja tena.

No comments:

Powered by Blogger.