Usiogope Kumruhusu Mtu Ambae Amekupenda

89967619-1024x683 Usiogope Kumruhusu Mtu Ambae Amekupenda

Wakati mwingine unaweza kuwa single kwa muda mrefu kwa sababu ya kuogopa  na kutokutambua mtu ambaye anaonyesha upendo wa kweli kwako.
Upendo ambao unaufanya kwa ajili yako unatosha na unajipa moyo kwamba huna haja  ya kuwa na mtu.Huhitaji mtu wa kukuambia jinsi gani ulivyo mzuri.
Unajisikia vizuri ukiwa mahali pako, kwenye Ulimwengu wako mwenyewe,kwenye kujipenda mwenyewe. Unasahau kuwa kuna mtu anahitaji kuwa  sehemu ya maisha yako. Huna ufahamu na umekataa hilo.
Umekuwa bora na  uko wazi ingawa huna uhakika , hata kidogo, kama unahitaji kumruhusu mtu  aonyeshe kukujali kwa upendo alionao.
Lakini Jaribu Kumpa Nafasi
Jaribu kumkaribisha maishani mwako, hata kama unao ujasiri kuwa unaweza kuishi ukiwa peke yako. mruhusu mtu kukuonyesha jinsi unavyostahili  kupendwa.mtu ambaye atakufanya ujisikie  kupata upendo ambao unaweza kuhamisha milima na bahari. mtu ambaye anataka kukulinda kwa gharama yoyote.
Kubali kupendwa na mtu ambaye  ni mvumilivu kukutia moyo kwamba hutakiwi kuwa peke yako katika maisha haya.Ni sawa kutokuwa na nguvu muda wote, hakuna tatizo unapoomba msaada. Hutakuwa mnyonge unapomwachia mtu kukushika mkono na kukuongoza.
Mpe mtu nafasi ya kukuhakikishia kwamba yuko tofauti na wengine waliokuvunja moyo. hatakukimbia  anapopata uamuzi mzuri.hawezi kukuumiza, hawezi kukuliza , na kukufanya ujisikie mpweke.
Hatacheza na hisia zako kwa sababu atakuwa anaogopa kukupoteza, atakuwa anaogopa kupoteza nafasi pekee ambayo unampa. Anaogopa kuwa siku moja atajuta kama atakuacha.
Mruhusu Mtu Akuweke Kwenye Mazingira Magumu Tena.Jiruhusu usiwe mgumu, uwe mpole, ili kuaminiwa. Kuwa Wazi Kwa Mtu Ambaye Ana Hamu Ya kukufahamu.
o-WINE_LAUGH_ALAMY-facebook-1024x683 Usiogope Kumruhusu Mtu Ambae Amekupenda
Mpe mtu nafasi ya kuujali moyo wako. mtu ambaye anafurahi kugundua kila kila kitu kuhusu wewe.  mtu ambaye hawezi kukuchoka na ambaye anataka kila mara kuwepo na wewe.
Jiruhusu kumpenda mtu ambaye anakutakiwa kila kilicho bora katika maisha yako.mtu ambaye anataka kuchukua majukumu  ya kukujali na kukulinda kwa sababu anakupenda. wewe ndiye unamfanya awe na tabasamu kila wakati. Umempa mwanga wa maisha.
Chukua Nafasi Hio. Chukua hatua kubwa. Take the riskiest option. Ni bora  kumpenda mtu kuliko kutokupa  uzoefu wa kupenda.
piggyback-ride-579x453 Usiogope Kumruhusu Mtu Ambae Amekupenda
Mpe mtu nafasi ya kuupenda moyo   uliopo ndani yako. jipe nafasi ya kukubali na kujali upendo ambao unatolewa kwa ajili yako,  upatie ulimwengu nafasi  ya kukuletea  huyo mtu ambaye anakupenda.
Huhitaji kuishi peke yako na kufurahia ukiwa peke yako. huna haja ya kumwonyesha kila mtu kwamba unaweza muda wote. kubali kupenda tena.
Na pata uzoefu  wa kufahamu jinsi maisha yalivyo mazuri,  unapokuwa na mtu ambaye unampenda kwa moyo wako, na ni Upendo wa kweli.

No comments:

Powered by Blogger.