Zingatia Hili Unapotafuta Mchumba
napotafuta mchumba "tumia kichwa chako kwanza" na tumia moyo wako ukisharidhika naye.
Katika ndoa kuna namna tofauti ya kupambana na matatizo au kutoelewana au kubishana au kutokubaliana na jambo au shida yoyote na kila wanandoa wana namna yao, hii ina maana kwamba tatizo lilelile ambalo wengine wanavurugana na kuachana kwa wengine ni opportunity ya kujenga ndoa yao.
Inaweza kutokea kwamba mke anapenda kuwa karibu na mume wake kimapenzi (intimacy) na mume akawa anapenda kuwa mwenyewe (privacy), inaweza kuwa mke hupenda kuchelewa kulala na mume ni mtu wa kuwahi kulala na kuamka mapema, inaweza kuwa mume anapenda kuhakikisha anapata milo 3 ya uhakika kwa siku, wakati mke anapenda milo miwili tu na imetoka. Inawezakena mke anapenda sana kuongea na mume ni mtu wa kuwa silent.
Hata hivyo bila wanandoa kuwa na aina ya kuchukuliana (flexibility/adaptivity) itakuwa ngumu sana kwa wanandoa kuridhika na ndoa yao.
Kwa kijana mgeni na masuala ya mapenzi anashauriwa kutumia kichwa na si moyo ili kuweza kumfahamu binti au kaka anayempenda awe mke wake kwa maisha ya baadae.
Kwani ukishampenda unaweza kupoteza mwelekeo kwa kupelekeshwa na emotions hadi kupoteza lengo la mke au mume uliyekuwa unategemea uoane naye.
Kwa wastani inachukua hadi miaka 2 tangu umemuweka kichwani (mke/au mume mtarajiwa) hadi kuoana.
Kwani bila kuchunguza kwa makini unaweza kujikuta unaingia kwenye jehanamu ndogo.
Kumbuka mwanaume ambaye anakupelekesha na kukukalia wakati wa uchumba akikuoa hiyo tabia yake itakuwa maradufu.
Kama binti hajiamini wakati wa uchumba, akiolewa ndo hatajiamini zaidi.
Utakuwa unajidanganya sana ukiamini kwamba kuoa au kuolewa kunaweza kuondoa au kutatua matatizo kama wivu, hasira, uchoyo, ukali, kukosa uaminifu, ubabe, kutojiamini nk
Ukweli ni kwamba kama Unaona tabia mbaya kwa mchumba wako basi tegemea hali mbaya zaidi baada ya kuona.
Pia, wapo watu ambao huamua kuoana baada ya kujuana au kufahamiana kwa muda mdogo sana kama vile mwezi mmoja au miezi miwili.
Kama unaamini ndoa ni hadi kifo kitakapowatenganisha, kwa nini uchukue uamuzi ambao utalazimika kuishi naye maisha yote huku unateseka kwa kuwa ulifanya mambo haraka haraka.
Pia siri kubwa ambayo wengi hawaijui ni kwamba kati ya asilimia 80 hadi 90 ya wanaume au wanawake unaowaona si wazuri kiasi cha kutosha kuoana na wewe.
Hii ina maana kwamba ni asilimia 80 hadi 90 ya watu hao wanakupenda lakini wanatamani sana wakubadilishe kwanza ndipo wakupende na mapenzi ya kweli ni kumpenda mtu na kumchukua kama alivyo.
Kumtafuta mke au mume wa kudumu katika maisha siyo “mchezo wa kitoto” ukienda kizembe kama mtoto utaoana na mtu mwenye akili za kitoto.
Ukweli ni kwamba unamtafuta mtu asiye wa kawaida, ambaye ana sifa maalumu unazohitaji na hakuna mchezo wa kukisi bali lazima uwe na uhakika.
Pia lazima ufahamu maeneo ambayo unaweza kumpata mwanamke mwenye sifa au mwanaume mwenye sifa.
No comments: