Ishara 11 za Mwanamke Anayekupenda, Lakini Anashindwa Kukueleza.


Kwa muda mrefu kumekuwa na wimbi la imani potofu kwa wanawake na wanaume kwamba mwanamke hawezi kumwambia mwanaume ukweli kama anampenda, wengi wao husubiri kwanza mpaka mwanaume aanze kuweka wazi hisia zake, lakini ni ukweli usiopingika kwamba wanawake nao pia hupenda na wengi wao wanakuwa hawapo tayari kuwa wawazi na mara nyingi wao wakianza kupenda huwa wanapenda kweli kufikia hata hatua ya kuhisi kutokuwa sawa katika mambo yao wanayoyafanya. 

Nimekuorodhoshea baadhi ya ishara za mwanamke anaekupenda ila anaogopa kukuambia kwa kuhofia namna atakavyoonekana mbele ya macho ya jamii au kuwa na hofu na jambo analotaka kukueleza kwa kufikiria kuwa itakuwaje endapo hautakuwa tayari kuwa nae na hapo ndio hukumbwa na hofu ya kuelezea hisia zake.

1. Kukupa majaribu madogomadogo ili kujua thamani yake kwako.
Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda na kumthamini au lah, mfano wa mambo hayo ni kama kujifanya anaumwa na kauangalia muitikio wako kwake, ili kutambua ni kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake.

2. Kugusa sehemu ya mwili wako.

Mwanamke anaekuwa na hisia za mapenzi huwa haoni aibu kugusa sehemu ya mwili wako. Anaweza kukushika mkono ama kukutomasa au hata kukumbatia kwa hisia za kimapenzi. Kwa kufanya hivyo huweza kujiwekea asilimia kadhaa za kujua kawa ni kwa asilimia kiasi gani anaweza kuwa na wewe kwenye mahusiano endapo ataweka wazi hisia zake kwako, na kwa mwitikio wako kwake, kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe kwa namna yoyote.

3. Kuweka ukaribu na wewe.
Huweza kukubaliana na wewe kwa jambo lolote hata kama halina maana endapo wewe tu utazungumza ili tu kuonesha kuwa yupo pamoja na wewe na pengine kurahisisha kazi yake ya kukueleza hisia zake za mapenzi juu yako. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli na hupenda kuwa karibu nawe hata kwa mawasiliano, kukutembelea kazini kwako au nyumbani pia na huwa yupo tayari kutumia gharama ya aina yoyote ili kuwa karibu na wewe.

4. Wivu.
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Wanaweza kuwa wafanyakazi wenzako au umeongozana na ndugu zako lakini yeye pasipo kutambua hilo, huwa na kiasi kikubwa cha wivu mara tu anapokuona katika mazingira ya kuzungukwa na wasichana wengine, na huwa anaumia kama akisikia mnaitana majina ya kimapenzi haijalishi kama mnataniana yeye huwa na wivu na hapendi. Hupenda mambo hayo afanyiwe yeye tu hata kama sio mpenzi wako.

5. Hukumbuka matukio yote ya muhimu kuhusu wewe.
Hukumbuka matukio yote ya muhimu kuhusu wewe kama vile siku zako muhimu na hata mwenendo wa maisha yako kama wewe ni mwanafunzi atajua siku yako ya mahafari, mfanyakazi, na endapo utakuwa mchezaji wa mpira anaweza kujua ratiba yako ya mashindano, timu unazozipenda na kadharika. Hukumbuka siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifauli mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mstari wa mbele kukupongeza.

6. Hupenda kukutazama kwa shauku.
Hupendelea sana kukutazama machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaweza kuzisoma hisia zake. Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda hivyo huwaagalia mara chache sana ila ni kwa hisia za kimapenzi ambazo zinaweza kupelekea mwanaume kuhisi kuna kitu kinaendelea kwa mwanamke huyo.

7. Hupenda kuwa na wewe kutaka kukujua zaidi.
Hupenda kukaa muda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata dakika ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu na hukaa bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya hata kama ilikua ni kazi ya muhimu ili ajumuike pamoja na wewe na akikaa na wewe hupendelea sana mwanzoni kukujua wewe zaidi na hukujengea mazingira ya wewe kuwa muwazi ili umwambie mengi kuhusu wewe. na pia akiwa na wewe atakuwa muwazi zaidi kuhusu yeye hupenda sana kujua mambo yako na kukuambia mambo yake na hupenda kujua ni mavazi gani yeye akivaa anakuvutia zaidi na atajitahidi kukufurahisha kwa kadri awezavyo.

8. Hujitoa.
Kama msichana anakupenda yupo tayari kujitolea kwa hali yoyote. Ni jambo ambacho hufanywa kwa nadra na watu wa kawaida kwako. Yaani yupo tayari akose mahitaji yake muhimu lakini wewe upate. Na huweza kumwambia mtu mwingine kuwa hana kitu, lakini akajitahidi akakupa wewe unachohitaji kama vile pesa na vitu vingine.

9. Hupenda kutatua migogoro yenu kwa amani.
Migogoro ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakwambia nakupenda, inawezekana wewe ndie uliekosea na kuwa chanzo cha mgogoro lakini yeye hujishusha kwa kuwa anakupenda na endapo ikitokea kutokuelewana basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose na kuhakikisha urafiki wenu unakuwa kama zamani.

10. Hupenda kukununulia zawadi.
Mwanamke anaekupenda hupenda kujua mengi sana kuhusu wewe na hapo hutumia njia nyingi kuwasilisha hisia zake kwa mfano kukununulia zawadi kama nguo za ndani, au kukununulia perfume, sabuni ya kuogea ya manukato, soksi, bukta, saa, raba, t-shirt. Na kama mkitoka pamoja mkaenda sehemu mbalimbali za manunuzi atapenda kukuonyesha vitu na wewe ukionekana umependa kitu hatonunua siku hiyo ila atanunua siku nyingine na kukuletea kama suprise.

11. Hupenda mshiriki matukio ya muhimu pamoja.
Mwanamke anaekupenda ili akujue zaidi hupendelea kuwa na wewe katika nyakati tofautitofauti kama kupata chakula pamoja, na wakati mwingine atapendelea kuja kupika kwako na ili apate nafasi ya kushiriki chakula pamoja na wewe, kwenda uwanjani kutazama mashindano au hata kumbi za starehe mkiwa pamoja


No comments:

Powered by Blogger.