MKASA: Bi Mkubwa (Mama mkwe) sehemu ya 1

Related image


( sehemu ya 1 )
Ni mwanamke ambaye alikuwa akiwanga usiku kila chumba katika nyumba yetu iliyokuwa jijini Arusha. Nilikuwa naogopa kumwambia mume wangu kuhusu uchawi wa mama ake na tabia yake ya kutusotea usiku tukiwa tumelala.
Siku moja alikuja chumbani kwetu na kunishusha chini akidhani kuwa amenipumbaza kwa dawa zake alizonimwagia lakini nilikuwa na akili timamu. Nilichukia sana baada ya kuona anataka kutufanyia kitu kibaya mimi na mume wangu ambaye ni mwanaye wa kumzaa.
Baada ya kunishusha juu ya kitanda na kunilaza kwenye zulia chumbani kwetu, mama mkwe alianza kumzunguka mume wangu akiwa kitandani, akachukua dawa yake akainywa kisha akamtemea mume wangu, akachukua kitambaa chekundu akakiloweka kwenye dawa yake akawa anampaka mume wangu sehemu ya siri kisha kumvua bukta yake.
Nilijisemea moyoni Nijifanye nimezinduka? Kutokana na kumuangalia mama mkwe wangu alivyokuwa akimfanyia mume wangu, moyo wangu ulikuwa ukidunda kama vile nimetoka kukimbia mbio ndefu dakika chache, nilikuwa natetemeka sana kwa kile nilichokuwa nakiona ila nilijipa ujasiri na kuendelea kuangali nini mama anakifanya Kwa mume wangu ?
Japoku kulikuwa na giza lakini mwanga wa taa za ulinzi, zilizokuwa zikiwaka nje, ziliniwezesha nione kila kitu alichokifanya mama mkwe dhidi ya mume wangu.
Niliona ni ajabu sana kumwona mama mkwe wangu akifanya mambo ya ajabu kwa mwanae wa kumzaa. Baada ya kumvua bukta akampaka dawa nyingine amabayo ilimfanya mume wangu mwili wake kusisimka na kusimamisha sehemu yake ya siri, mama mkwe wangu naye akavua nguo zake akapanda kitandani akashika sehemu za siri za mume wangu akazipaka mfuta, akaanza kufanya mapenzi na mume wangu huku akiimba nyimbo ambazo sikuzilewa.
Ni ajabu sana kuona mama mtu mzima akihangaika na mwanaye aliyemzaa na akawa anatembea naye huku nikimuona.
Uvumilivu uliniishia nikajifanya nanyoosha miguu huku nikikohoa.
Haraka sana kama vile paka anavyomkamata panya, bi mkubwa yule aliruka kitandani na kusimama huku akiniangalia, nikajifanya sijazinduka usingizini.
Alitoka mbio na kwenda chumbani kwake huku akiniacha nikiwa bado chini kwenye zulia na mume wangu alikuwa yupo kitandani lakini alikuwa hajui lolote linaloendelea maana alikuwa hajitambui.
Sikujua nini alimfanyia mpaka akawa kama aliyezimia, Nadhani ile dawa aliyokunywa na kumtemea ndio iliyomfanya mume wangu asijielewe.
Niliinuka pale chini na kuketi kitandani, 
Ghafla mama mkwe akaingia tena chumbani kwetu huku akiwa na tunguri ndogo ambayo ilikuwa na shanga kibao kuzunguka mdomo wake na ilikuwa imepakwa mafuta.
Baada ya kuniona nikiwa nimekaa kitandani alipigwa na butwaa akashindwa kurudi nyuma kwa sababu aliingia akiwa na spidi kali.
Nilimuuliza Mama kwa nini umeingia chumbani kwetu, Kuna nini? ..
Mama alipata kigugumizi cha miguu maana alishindwa kurudi alipotoka au kuingia ndani kabisa akawa kama kashikwa na bumbuwazi hivi kuniona nikiwa nimekaa kitandani ni jambo ambalo hakulitegemea.
Akawa ananiangalia bila kusema chochote. Niliinuka na kuwasha taa, baada ya kuwasha taa ndipo alipoanza kutetemeka kama vile anaugua malaria kali.
"Mama umefuata nini huku chumbani kwetu?
"'Nime......nime.....
"Nime...Nime...kwani mama huwezi kuongea vizuri, na Mbona mikononi una tunguri ni ya nini? Mama kumbe wewe ni mchawi? Unaturoga?
""Sikiliza wewe mwanamke huyu ni mwanangu na Nina haki ya kupata kila kitu ninachokihitaji kutoka kwake, na wewe umemkuta akiwa amekua kwahiyo na wewe jichunge sana na sitaki kusikia unasema jambo hili kwa mtu yeyote, umenielewa?
Alifoka mama mkwe
Lakini mama kwa nini unatufanyia hivi? ina maana umeshindwa kwenda kwenye nyumba nyingine ukafanya upuuzi huu. Huyu ni mwanao, kwa nini umemvua bukta na kufanya Naye mapenzi?
Nilisema huku nikitetemeka kutokana na hasira.
"Narudia tena, sitaki kabisa kusikia hili jambo kwa mtu yeyote, ikivuja tu nakuumiza, tena ukiendelea kuniuliza maswali ya kijinga nitakuziba hicho unacholingia utabaki na kitobo kidogo tu cha kukojolea sawa , alisema mama mkwe huku akionekana kujawa na hasira.
Wakati anasema hayo nilijitahidi kumuamsha mume wangu lakini alikuwa hajui kinachoendelea. Nilijitahidi kumtikisa lakini akawa haamki wala kusema lolote alibaki kukoroma.
Niliamua kumvalisha bukta yake huku mama yake akiangalia. Nilipandwa na hasira nikatamani nimrukie mama mkwe wangu lakini niliona uhai wa mume wangu ni muhimu zaidi, hivyo nikawa najitahidi kumtingisha huku nikimuita jina.
"Usijifanye kuwa na hasira nakuambia kitu kimoja. Sema hapa kwamba hutasema siri hii kwa watu la sivyo nitamuacha mumeo akiwa katika hali hiyo, tuone utaringia nini?
Maneno hayo yalinifanya niamini kwamba mchawi huwa hana huruma. Kama mwanaye wa kumzaa anathubutu kusema atamuacha akiwa amezimia namna hii, je ningekuwa mimi si angeniacha nife kabisa?
"Mama tafadhali, mrudishie akili yake mume wangu. Nilimsihi lakini yeye akawa hajali na badala yake alikuwa akisema kwa kunongona maneno ambayo sikuwa nafahamu maana yake kwa sababu hayakuwa ya Kiswahili.
Wakati akifanya hivyo ghafla giza lilitanda chumbani. Sikujua nani alizima taa, awali nilidhani Tanesco wamezima umeme lakini niliamini ni mazingaombwe ya yule mama mkwe kwa sababu mwanga wa taa za nyumba ya jirani ulikuwa ukiingia katika nyumba yetu.
Kufumba na kufumbua nikaona mbele yangu limesimama kundi la watu waliokuwa wamevaa nguo nyeusi yaani kaniki. Kila mmoja akiwa amepaka rangi nyeusi usoni na katika mikono yao walikuwa wameshika usinga.
Niliishiwa nguvu na kujikuta nikiwa nimeketi kitandani kando yangu akiwa mume wangu ambaye alikuwa haelewi kinachoendelea.
Itaendelea.......


Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

from Tujifunze Mapenzi https://ift.tt/2zR8Usy
via

No comments:

Powered by Blogger.