MKASA: Bi Mkubwa (Mama mkwe) sehemu ya 2
BI MKUBWA
( sehemu ya 2 )
Endeleaa........
Kufumba na kufumbua nikaona mbele yangu limesimama kundi la watu waliokuwa wamevaa nguo nyeusi yaani kaniki. Kila mmoja akiwa amepaka rangi nyeusi usoni na katika mikono yao walikuwa wameshika usinga.
Niliishiwa nguvu na kujikuta nikiwa nimeketi kitandani kando yangu akiwa mume wangu ambaye alikuwa haelewi kinachoendelea.
Mama mkwe baada ya kuwaona watu wale ambao alikuwa kawaita wameingia akaanza kuwapa shughuli aliyowaitia,
sikujua waliingilia wapi kwa kuwa milango na madirisha ilikuwa imefungwa, walianza kuimba
polepole huku wakicheza.
Nilimwagiwa na mama mkwe unga fulani
ulionifanya niishiwe nguvu na kujikuta
nikimdondokea mume wangu ambaye alikuwa amelala fofofo.
Japokuwa nguvu ziliisha lakini ubongo wangu ulikuwa ukijua kila kilichokuwa kinaendelea pale, Nilifumba mambo kwa hofu kwamba nikiwaangalia
wanaweza kuniangamiza kabisa au kunipa dawa zaidi ambazo zitaniumiza.
Nilitamani mume wangu naye apate fahamu ili ajionee mauzauza haya anayofanya mama yake na ushirikina wake kwa mambo ya ulozi.
Mzee mmoja ambaye sikuwa namjua jina nilimsikia akimuuliza mama mkwe.
“Tuambie, umetuitia nini?
” Mama mkwe nilihisi alihama pale alipokuwa amesimama na sasa alikuwa karibu kabisa na pale tulipolala mimi na mume wangu.
"Akanifunua nguo ya kulalia kwa kutumia usinga alioshika, kisha akamwambia yule mzee 'Vipi hapa ujapapenda? Alikuwa akionesha sehemu za mapaja yangu.
"Yule mzee akanisogelea akachukua kitamba chekundu akachovya dawa yake akanipaka sehemu ya siri, baada ya kunipaa tu ile dawa nilijisikia raha sana, nilitamani sana aje karibu yangu ili aje anipe chakula cha usiku japo kuwa nilikuwa naogopa sana, akaniangalia vizuri akaniona nipo tayari Kwa ajiri ya kunihondomola, Mwisho akajibu swali la mama 'Yupo vizuri ila Kwa Leo tupo vizuri kwahiyo hatutaweza kufanya chochote hadi Siku nyingine, niliposikia hivyo nilitamani nimrukie maana nilikuwa na hisia Kali sana ya tendo la ndoa ila nilishindwa kutokana na hofu.
Yule mzee akamuuliza mama
"Kwani ni nani yako huyu?
“Huyu ni mkwe wangu?,
"Sasa Tufanyeje na sisi Leo tushalizika tulikotoka, au kuna lingine?
"Ndio lingine lipo na ndio haswaa nililowaitia hapa
"Ni nini hicho ?
"Huyu mkwe wangu amenigundua leo kuwa mimi ni mchawi, nikaona ni vema niwaiteni wenzangu mnishauri nifanye nini?”
"Kwanini amegundua unakuwa mzembe sio?
"Sio hivyo sikujua kuwa.......
"Hukujua nini wewe tunakujua vizuri unaharaka sana, ndio matokeo yake hayaa.
Waliendeleaa kubishana pale wakati huo nilikuwa na wasiwasi sana, Baada ya kusikia kilichowafanya wale wachawi
waje pale, moyo wangu ulienda mbio nikajua kuwa siku ya mwisho wa maisha yangu imefika.
Baada ya mda wakatulia na kuendelea na maongezi wakiwa wanaelewana vizuri "sasa nawaombeni nyie wenzangu mnishauli nimfanye nini huyu mkwe wangu?
“kwahiyo Unataka tukuchagulie sisi cha kumfanya mkweo?” Mchawi mwingine aliuliza, nadhani alikuwa wa kike
kutokana na sauti yake kuwa nyororo
“Ndio, kwani kuomba ushauri kuna ubaya? Mimi nilijua kuwa mtapita hapa kunipitia nikaona ni vema niwaombe muingie humu ndani mnishauri.”
Mama mkwe akanywa dawa yake akanitemea Mimi na Mme wangu
“Sasa mbona unawatemea dawa kabla hatujakushauli ni ya nini?
Alidakia mwingine.
“Ahaa hii dawa ni ya kumfanya asizinduke sasa hivi mpaka tumalize mazungumzo yetu, wasijue mnashauri nini.”
“Kwani mkweo anaitwa nani?”
“Jina lake ni Johari, ni mkazi wa Ndanda
ndiyo kwao,” mama mkwe aliwajibu
“Je unataka huyu johari tumfanye
zezeta?”
“Hapana, Kwa jinsi mwanangu anavyompenda, atapata shida sana kwani hatamuacha, atakuwa
akimhudumia, sasa kwa kuwa huyu atakuwa hana akili, atateseka mwanangu sababu anampenda sana.
"Basi tumuue kabisa huyu?
"Kwa kweli Wazazi wake nawaogopa sana
“Sasa ni juu yako kuamua utamfanya nini mkweo, kwa sababu kila tunachokuambia unawakuwa na
huruma, sasa uamuzi ni wako.”
“Sawa niachieni nitajua la kufanya,” alisema mama mkwe.
Baada ya mda kidogo wale wachawi wakatoweka, bimkubwa akabaki na sisi, akachukua kitambaa cheupe akachovya dawa ya kutuzindua na yeye akatoweka kimazingara.
Japokuwa tulipĆ kwa dawa ya kutuzindua lakini hatukuweza kuamka kwa mda ule tuliendelea kulala fofofo na hatimaye kulikucha.
Nilishitukia asubuhi naitwa jina na mume wangu.
“Baby johari,
"Abeee mume wangu.
"Mbona leo umechelewa kuamka?”
amka basi,” alisema mume wangu huku akinitikisa mguu.
Moyo wangu ulienda mbio baada ya kutikiswa mguu nilidhani bado ni usiku na nilikuwa natikiswa na wale wachawi walioalikwa na mama mkwe.
Nilipofumbua macho nilimuona mume wangu akiwa amesimama nyuma ya miguu yangu huku akiwa amefunga taulo kiunoni na mdomoni alikuwa na
mswaki.
Nahisi ndiyo maana sikuweza kumtambua sauti wakati ananiita nikiwa usingizini kwa sababu mswaki ulimfanya asitoe sauti niliyoizoea.
Nilifikicha macho ili nimuone vizuri na kwa kuwa ndani ya chumba chetu cha kulala kuna saa niliiangalia na kuona kuwa ilikuwa saa 12.30 asubuhi na kweli muda huo mimi huwa nimeshaoga
na kuanza kazi ndogondogo hapa nyumbani kwangu.
Niliamka na kuketi kitandani lakini ghafla
nikakumbuka sakata la wachawi wa usiku na nikaanza kutokwa na machozi.
“Kwa nini unalia mke wangu?”
“Nilishindwa kujieleza kwa sababu nilifikiri sana na kujiambia kimoyomoyo kuwa nikisema, mama mkwe alikuja chumbani usiku akafanya yale
yasiyofaa kwa mume wangu na mimi hapa saizi nikimwambia huyu mwenzangu sijui kama atanielewa.
Nilitafakari sana juu ya hilo, hivyo nikashindwa pa kuanzia badala yake machozi yakawa yanatiririka
bila kujua niseme nini kwa mume wangu.
Nilikuwa na maswali ya kujiuliza kwamba je nikimwambia mume wangu kuwa mama yake ni mchawi atakubaliana nami? Nikajiuliza pia kuwa nikimfahamisha kuwa usiku alimvua bukta nami kunilaza chini ya zulia na akamfanyia mambo mabaya atanielewa?
Maswali hayo nilishindwa kujijibu nikabaki natokwa na machozi.
“Johari nieleze, umepatwa na nini?”
Mume wangu alizidi kudadisi.
“Mume wangu Naomba niache kwa muda, nitakuambia,” nilimjibu lakini hakuona kuwa ni haki abaki na maswali mengi kichwani mwake bila kujua nini kinaniliza.
Alinibembeleza nimueleze kinachoniliza lakini sikutaka kupasua jipu wakati ule hasa ikizingatiwa kuwa mama yake ambaye nimetokea kumchukia
ghafla baada ya kumbamba akiwa chumbani kwetu akifanya uchafu na mtoto wake wa kumzaa.
Nilimuambia mume wangu kuwa aende
kazini na akirudi jioni nitampa kisa kizito.
“Kisa kizito?
"Sitaweza kufanya kazi bila kuniambia,
Kama kuna jambo limekukwaza tafadhali sana niambie wala usiwe na mashaka juu yangu kwa sababu lako ni langu na langu ni lako.
"""Niambie umekwazwa na nini?”
“ Mume wangu tafadhali sana niamini,
kinachonikwaza wala hakihusiani na wewe ni matatizo yangu tu ya maisha haya tuliyonayo.”
“Matatizo ya maisha ndiyo yakufanye uhaiirishe kuniambia linalokukwaza sasa mpaka jioni nitakaporudi kazini? Hapana, utakuwa hunitendei haki.
” Baada ya kufikiria sana niliamua kumueleza mume wangu uongo ili tu kumfanya aende kazini.
“Sikiliza mume wangu.
Mimi huwa nasikia moyo ukinienda mbio sana nahisi nina tatizo la moyo na ndiyo maana nalia. Nawaza kama moyo wangu ni mkubwa si ndiyo mwisho wa maisha yangu na kukuacha peke yako mume wangu?
“Mke wangu kama hilo ndilo tatizo
ulipaswa kuniambia mapema, kwani umeanza kupata tatizo hilo lini?”
“Ni usiku. Nilijaribu kukuamsha lakini ukawa huamki, hapo ndipo nilipoanza kulia.”
“Nakuapia kwa jina la Mungu, sikujua kabisa kama uliniamsha. Kweli unaweza kuniamsha nikaacha kuamka tena usiku? Hakuna asiyejua kuwa usiku
una mambo. Tafadhali sana mke wangu nisamehe sikufanya kusudi.”
“Nimekusamehe mume wangu.”
“Kama hivyo ndivyo, basi ngoja nipige simu ofisini kuomba ruhusa kisha nikupeleke hospitali.”
“Unaona? Ndiyo maana nilikuwa sitaki kukueleza, nilijua utakatisha
safari yako ya kwenda ofisini. Nenda ofisini na mimi nitakwenda mwenyewe hospitali.”
“Itakuwa ni kichekesho. Mtu ambaye usiku hakulala kwa maumivu ya kitu nyeti, moyo, aende hospitali peke yake? Nitaonekana mpumbavu mbele ya jamii.
Jiandae twende sote hospitali.
Ilinibidi nijikaze tu sasa niwe kama naumwa kweli ili tu nisimwambie mume wangu kilichotokea usiku, Kabla ya kuondoka na kwenda kwenye tiba hospitalini niliingia bafuni
kuoga.
Wakati naingia nilimkuta mama mkwe akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia bafuni. Alikuwa ananitazama wakati namkaribia pale aliposimama, Nilitegemea angenipisha ili nipite
badala yake akawa bado amesimama mlangoni huku mkono wake ukiwa umeshika upande mmoja wa mlango.
Nilisimama ili kuona kama atanipisha badala yake akanisogelea na kuanza kuninong’oneza.
“Ukimwambia mumeo kilichotokea usiku nakuua, umesikia?”
“ Kwa nini uniue?”
“Kwa sababu ile ni siri ya wachawi. Thubutu kumwambia uone kitakachokupata. Usione nipo hivi, nimechukia sana kuona
unafahamu siri yetu rejareja, jaribu kumuambia mumeo uone. Umesikia?
Sikumjibu neno badala yake nilikuwa namuangalia kwa kumshangaa mama
kwa kuendekeza uchawi.
Akaendelea kunitisha.
“Nilikuwa nakusikiliza kwa makini sana
ulipokuwa chumbani na mume wangu lakini nilifurahi kuona kuwa hukumwambia mumeo
ambaye ni mwanangu yale mambo ya usiku.
Endelea kuficha siri, Na ukitaka kujiunga na sisi nitakuruhusu sababu unajua siri yetu, alafu kumbuka usiku kuna raha sana si wewe mwenyewe umeona pale nilikuwa nakula raha na mume wako hata mwenyewe ajui,
"Sasa vipi nikufanyie mpango ujiunge au?
Itaendelea........
Usisahau kushare post hii.š Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
from Tujifunze Mapenzi https://ift.tt/2PxvM5q
via
No comments: