KITU GANI UNACHOKIPENDA UMEKIFICHA KUHUSU MWENZA WAKO?
Nguvu zetu na madhaifu yetu mara nyingi zinakuwa sawa. zinavutana kila wakati, kila moja upande wa mwingine, kitu fulani chenye uwezo na udhaifu , kitu ambacho kinamfanya mwingine ajisikie vibaya. Lakini pia ipo faida kama ukiangalia plan B Yaani nguvu iliopo.
Mara nyingi kwenye mahusiano huangukia kwenye nguvu aliyonayo mtu. Hii inaweza kuwepo katika njia zote ndogo na kubwa. Kwa mfano unachukizwa na mwenza wako anapokuwa hayuko makini kununua vitu kwa wakati, na mara nyingi ananunua vitu ambavyo havihitajiki kwa wakati huo.
Kwa matarajio makubwa unategemea kuwa ataweza kugundua kutokana na kutopendezwa kwako na hali ile, lakini bado anaendelea kufanya vitu vilevile. badala ya kumwambia unalalamika kila siku pembeni , sasa atajuaje kosa lake? Ni vizuri kama ukamwambia kwa njia nzuri ya kueleweka, njia ambayo hatajiona kama mtu asiye na akili ya kupanga mipango bali kama mtu mwenye akili. Jielezee kwa njia rahisi ya ufahamu wako kwa kumpa sifa mbalimbali mwenza wako.
Kitu Gani Unapenda kwa mwenza wako Na hujawahi Kumwambia?
Ngoja nikupe baadhi ya mifano ya kukufungulia fikra zako.
1.Huenda mwenza wako anatumia muda mwingi na marafiki, kuwasaidia majirani, unatamani kukaa naye lakini mara wanakuja watu na anaanza kuwasaidia kwa sababu ya umaarufiu alionao.
2.Kila mara mwenza wako anakukera na maswali ya kutaka kujua matumizi ya computer au simu . Kwa sababu hana ujuzi na hivyo vitu. halafu muda mwingi anatumia katika hivyo vifaa.
3. Ni mtu anayependa maisha ya juu, hataki kukaa mahali ambapo hakuna kiwango , hasa mnapotoka kwenda hotelini kula.
4.Anawajali watoto kuliko wewe, lakini unapenda uvumilivu wake
5.Hapendi kuongea kuongea , lakini anajali familia na kuhakikisha kuwa kila kitu kimekaa sawa, hakuna kitu kinachoweza kudhuru maisha yenu.
6. Mwenza wako hapendi mashuka yajikunje kunje kama ametandika halafu wewe ukae na kuharibu, mara nyingine jinsi ya kutumia dawa ya mswaki unaminya kila sehemu , huna utaratibu . Unaacha nywele kwenye chanuo, Wewe unataka kila kitu kikae kama ulivyoweka.
7.Tabia yake haibadiliki tangu mwanzo ulipokutana naye, umechemsha hapo. jaribu kujibadilisha wewe, jaribu kufanya mambo mapya, utaona na yeye atatamani kufanya kama wewe, lakini hutaweza kumbadilisha mtu.
Kama Unapata Taabu Kufikiri Kuhusu Mawazo Yako
1.Fikiri ni kitu gani ulikuwa unakipenda kabla hujaamua kuishi naye na hicho kitu labda kimekosa thamani.
2.Jaribu Kufikiri kuhusu mahusiano ya watu wengine. wakati mwingine ni rahisi kufikiri kuhusu wengine kuliko wewe mwenyewe.
3.Jaribu kuorodhesha vitu ambavyo huvipendi na vile unavyovipenda . andika sifa zake na kuangalia jinsi gani unavifanyia kazi.
Kama unaona mahusiano yako hayakai vizuri, tambua kuwa mawasiliano sio mazuri kati yenu. Mweleze mwenza wako jinsi unavyojisikia , elezea hisia zako, madhaifu yaliopo , nguvu iliopo, Elewa kuwa huenda sio makusudi afanyavyo, anaweza kukuelewa.
No comments: