Makosa sita yanayofanywa Siku ya Valentine



Related image

Siku ya Wapendanao, maarufu kama Siku ya Valentine, pamoja na kwamba haitambuliki kama moja ya siku maalumu za kiserikali, lakini imekuwa ikijipatia umaarufu kila kukicha katika kila pembe ya dunia ifikapo Februari 14.
Inawezekana wengi wa wanaofanya hivyo hawatambui utamaduni huu ulitokea wapi.
Kihistoria jina la sherehe hizi lilitokana na jina la mtakatifu wa madhehebu ya Kikatoliki aliyekuwa akijulikana kama Valentine au Valentinus.
Mtakatifu huyo aliishi duniani katika karne ya tatu mjini Rome, wakati wa utawala wa Claudius II, ambaye alikuwa amezuia vijana kutooa, kutokana na imani kwamba wangekuwa wanajeshi imara kuliko wale wenye familia na waliooa.
Kutokana na imani hiyo, akaona ni bora azuie vijana kutooa ili waweze kuwa wanajeshi bora, lakini Mtakatifu Valentine, alionekana kutokubaliana na hilo, aliendelea kufungisha ndoa za siri kwa vijana hao.
Baada ya kugunduliwa amekiuka amri ya mfalme, Claudius alitoa amri ya kukamatwa na kuuawa. Ili kumkumbuka ndipo zikaanzishwa sherehe hizi.
Lakini, pamoja na historia hiyo fupi kumekuwa na makosa ambayo yamegunduliwa kufanyika katika sherehe hizi ambazo ni maalumu kwa wapendanao kuzidisha upendo.
Katika siku hii, hasa wanaume wamekuwa wakifanya makosa ambayo wanayaona ya kawaida kwao bila kujali yanaathiri mahusiano yao kwa kiasi gani.
1. Kosa la kwanza
Hata kama una tabia ya kutozungumza maneno ya hekima hakikisha katika siku hii unazungumza maneno ya busara, ikiwa ni pamoja na kumuandikia ujumbe mpendwa wako wa kumfurahisha, kwani katika uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa wanawake wengi wanapenda kuzawadiwa kadi na kuandikiwa maneno mazuri ya mapenzi huku wakiwa sambamba na wapendwa wao.
2. Kosa la pili
Uchaguzi wa zawadi
Mtaalamu wa masuala ya saikolojia ya mapenzi, Dk. Terri Orbuch, anasema zaidi ya asilimia 75 ya wanawake wamekuwa wakipenda kupewa zawadi zaidi ya wao kutoa.
Lakini, wanaume wengi wamekuwa wakishindwa kuwanunulia zawadi kutokana na fikra potofu, wakidhani zawadi nzuri ni kubwa peke yake ndiyo itaweza kumpatia heshima.
Wanafikiria zawadi ni lazima ununue vitu kama magari au vito vya thamani, kumbe wanawake hufurahia zawadi za kawaida kama chocolate, kadi na maua ikiwa ni pamoja na kuambiwa maneno matamu ya kimahaba.
Ni vizuri katika siku hii kwenda dukani na kumnunulia mpendwa wako zawadi za maua mazuri, vitabu vya mahaba, DVD za mapenzi, mishumaa, chocolates na nyingine za aina hiyo.
Tahadhari
Jihadhari kuzembea kutoonesha tabasamu lako unapokuwa na mpenzi wako kwani haistahili kuwa ‘siliasi’ au watoto wa siku hizi wanasema usioneshe uso wa mbuzi.
Kwa nini unashauriwa kununua zawadi za kawaida? Hii inakuwa inamsaidia mpenzi wako hata asiyekuwa na uwezo naye kukununulia kama hiyo, kwani wengi wamekuwa na mtindo wa kurudisha zawadi inayofanana na ile uliyomnunulia.
Kama unajua mwenzi wako hana uwezo halafu wewe unamnunulia vito vya samani utampa shida kukununulia zawadi ambayo itakwenda sawa na ile uliyomnunulia.
3. Kutokabili maudhi
Inashauriwa kwa wapendanao kuandaana kabla ya siku yenyewe kufika na kuhakikisha mnajihadhari kufanya au kumuonesha mwenzako mambo ambayo unajua yataleta maudhi kwake, hivyo kufanya siku hiyo kuwa mbaya kwenu.
Tahadhari
Unashauriwa ujihadhari kutafuta filamu za kuhuzunisha ambazo zitasababisha kumfanya mwenzi wako apate mawazo, hali itakayosababisha kupunguza furaha yenu na kuifanya siku hii kuwa mbaya au kuweka wimbo ambao utaonekana kama kijembe kwake.
4. Kubadilishana mawazo
Hili la kubadilishana mawazo linasaidia kuongeza upendo kwa wawili na hii haijalishi ni njia gani unaitumia, iwe kutuma ujumbe wa simu au barua pepe za mtandaoni au unaweza kutumia mitandao ya Facebook na Twitter, hii itamfariji hata yule aliye mbali nawe.
Wakati mwingine unaweza kutumia barua ambayo itakuwa na maneno mazuri ikiwa sambamba na picha ambayo nyuma yake utakuwa umeiandika ujumbe mzuri wa kimahaba, ikiwa ni pamoja na CD iliyojaa nyimbo za mapenzi ili asikilize ukiwa umempatia kama zawadi.
5. Kutomsikiliza mwenzio kwa mipango ya familia
Kwa nchini Marekani, inadaiwa asilimia 64 za wanafamilia hutumia siku hii kupanga uzazi kwa kusikiliza mipango ya mwenzi wako.
Aidha, hutumia kuombana misamaha na kuondoa migongano iliyowahi kutokea hapo nyuma, kwani kwa kufanya hivyo siku hiyo itakuwa ya furaha kwa wapendanao. Kumsikiliza mwenzio kutakuwa kunaonesha namna unavyomjali mwenzi wako.
Tahadhari
Kama utakuwa hauna fedha za kumtoa mwenza wako katika sehemu za starehe haimaanishi hutasherehekea bali utasherehekea kwa kufurahia na mpenzi wako nyumbani kwako.
Unachotakiwa kufanya ni kuandaa chakula ambacho unaamini nyote wawili mnakipenda na kukifurahia huku mkiwa mmewasha mshumaa juu ya meza. Katika meza hiyo unatakiwa kuweka chupa ya kinywaji cha ‘wine’.
6. Namna ya uvaaji
Siku hii pia ina namna yake ya kuvaa, nia ikiwa ni kutegemea na wapendanao. Kwa mwanamke anashauriwa kuepuka kuvaa jinsi, hii haijalishi ni kwa kiasi gani inakutoa bomba, kwani vazi hili halihamasishi pindi mnapokuwa wawili kwenye mapenzi yenu muda wa jioni.
Pindi unapokuwa na mpenzi wako unatakiwa kuvaa gauni jipya na fupi ambalo litamvutia mwenzio.
Kwa upande wa mwanamume anatakiwa avae pamba nyepesi, nikimaanisha suruali ya kitambaa na shati la mikono mirefu au mifupi na si vibaya kama utavaa tai ndogo, wakati mwingine si vibaya kujipigilia suti.


Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

 

  Install Application ya Raha Ya Mapenzi Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi



No comments:

Powered by Blogger.