Maneno ya hekima kwa wenye hekima

Related image

1-Chozi la aliyedhulumiwa
2-Chozi la yatima
3-Chozi la baba na mama yako
Moja ya machozi haya yakitiririka, umejifungulia jahannam


# Usimuumize aliyekupita umri, na wala usimkatize.. siku moja utakuwa kama yeye


# Kufanya utani kwa maandishi kunaweza kufahamika vibaya kwa sababu ya kukosekana ishara ya uso na mikwaruzo ya sauti.. basi kuwa makini katika kuchagua maneno yako, kwani wengi wa watu ni wanatafsiri vyengine


# Utamu wa maisha ni kuishi kwa staili yako, na si staili ya wengine


# Ni kweli kwamba maji yanarudi kwenye mkondo wake, lakini yakirudi yanakuwa hayafai kuyanywa

# Usijaribu kufuatilia kila kitu, huenda ukafahamu sivyo na ukawapoteza wengi walio karibu yako kwa sababu ya fikra zako.. jambo la kufanya; kuwa na dhana njema kwa walio karibu nawe


# Watu wengi wanazungumzia kutenda na hawafanyi lolote.. na wengine hawasemi watakalofanya na wanafanya na kupata wanayotaka



# Hakuna tofauti kati ya rangi ya chumvi na ya sukari.. vyote viwili ni rangi moja.. lakini tofauti utaijuwa baada ya kujaribu! halikadhalika wanadamu



# Wengi wanaoongelea aibu za watu ni watu ambao hawaangalii aibu zao kubwa, miongoni mwa hizo ni vile wao kuhadithia aibu za watu


# Marafiki hawabadiliki bali sisi tunafanya haraka kuwaita baadhi ya watu marafiki



# Baadhi ya watu watakuacha, lakini hiyo si mwisho wa kisa cha maisha yako, bali ni mwisho wa nafasi yao kwenye kisa chako si zaidi


# Hutaweza kubadilisha umbo lako ili uwe mzuri zaidi kwenye macho ya watu, lakini unaweza kudhibiti tabia yako na kuipendezesha adabu yako ili uwe mzuri kwenye macho ya watu




# Sisi ni jamii tukitaka haraka tunasema jambo jema ni bora lifanywe haraka.. na tukitaka kuchelewesha tunasema kuchelewa kuna kheri yake.. masuala ni mizaji, si zaidi



Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

 

  Install Application ya Raha Ya Mapenzi Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi



No comments:

Powered by Blogger.