SIMULIZI MPYA: TANGA RAHA 01

TANGA RAHA 01
(Return Of Olivia Hitler)

Furaha na amani, vinazidi kuendelea kutawala familia ya bwana Eddy pamoja na mke wake Rahma. Uzuri wa watoto wao ambao kwa sasa wametimia miaka kumi na nane tangu watoke tumboni mwa mama yao mzazi, unaendelea kuchukua twasira mpya kwenye jamii. Kwani mara kadhaa wazamini wa mashindano ya urembo mkoani Tanga, wanapeleka maombi yao mara kwa mara kwa wazazi wa Xaviela na Xaviena, ili waweze kushiriki mashindano ya ulimbwende kumtafuta mrembo wa jiji la Tanga atakaye wakilisha mkoa katika kuwania taji la urembo wa Tanzania na taji la dunia.
"Baba Xaviena hivi unauhakika kweli na hao watu, wanao wataka kina Xaviena wakashiriki huo udubwasha wao?"
Ni sauti ya Rahma akizungumza humu macho yake akimtazama mumewe anaye jikuna kichwa akifikiria jibu la kuwapa wazee saba wanao husika katika maswala ya kuandaa mashindano ya urembo, wanao wasubiria sebleni.
"Hivi hao wanao wewe unawaonaje onaje?"
"Sijakuelewa swali lako mume wangu?"
"Namaanisha wataweza kushiriki hayo mashindano?"
"Sasa Eddy mume wangu, Xaviena kidogo ninaona ndio anavutiwa na hayo mambo ya urembo. Ila Xavila mmmmm sidhani kama ana hata mpango wa kuwa miss."
"Wenyewe wapo wapi?"
"Ndani kwao"
"Wapigie simu waje"
Kutokana na ukubwa wa jumba wanalo ishi Eddy na mke wake, ilimlazimu Rahma kumpigia simu Xaviena, akawaomba waingie kwenye chumba cha kusomea ambapo wapo wazazi wao
Haukupita muda sana Xaviela na Xaviena wakaingia kwenye chumba cha kusomea na kuwakuta wazazi wao wakiwasubiri kwa hamo.
"Wale wazee wamekuja tena?"
Xaviela aliuliza huku akiwatazama wazazi wake.
"Ndio kwani vipi?"
Eddy alijibu huku akirudisha swali kwa mwanaye huyo.
"Lakini dady, hao wazee si uliwakataza wasije?"
"Ndio niliwakataza wasije, kipindi kile mulikuwa mupo shule sasa kipindi hichi munacho subiria matokeo yenu ya mtihani, nimeona niwashirilishe hili jambo"
"Jambo gani baba?"
Xaviena aliuliza kwa upole huku akimtazama baba yake usoni. Eddy akawaelezea watoto wake dhamira ya wazee hao kufika hapo nyumbani kwao mara kwa mara, hadi anamaliza kuzungumza sura ya Xaviena ikawa imechanua kwa tabasamu pana, akifurahia ombi la wazee hao, kwani ni moja ya ndoto zake kuwa mrembo japo hata kwa mtaa anao ishi yeye. Hali ni tofauti kwa Xaviela asiye penda hata kusikia neno urembo, muda wake mwingi anautumia katika kufanya mazoezi ya viungo na kutazama filamu za mapigano.
"Baba na mama, mimi sina muda huo wa kwenda kwenye mashindano hayo ya kipuuzi"
Xaviela alizungumza, akafungua mlango na kuondoka, jambo lililo mfanya Rahma kufungua mlango na kwenda anapo kwenda mtoto wake huyo wa kike, anaye mpenda kupita maelezo.
"Eheee na wewe vipi, jibu ni kama la huyo mwenzio?"
"Hapana baba, mimi nipo tayari kwa hilo"
"Kweli?"
"Kweli Dady"
"Haya usije ukenda kutuaibisha kama unavyo fahamu baba yako ninagombania ubunge uchaguzi unao kuja, itakuwa jambo la kushangaza mtoto wa mbunge akishindwa"
"Mmm jamani dady ngoja nikuonyeshe wanavyo tembea mamiss"
Xaviena akaanza kutembea mbele ya baba yake, huku mara kadhaa akigeuka kwa mapozi kama wanavyo fanya warembo wanao gombabia mataji mbali mbali duniani.
"Amekufundisha nani hivyo?"
"Mimi mwenyewe huwa napenda kutazana mashindano ya urembo"
"Kwahiyo nikawajibu upo tayari"
"Ndio baba"
"Haya"
Eddy akatoka katika chumba alichokuwa na Xaviena na kwenda katika sebule alipo waacha wazee hao
"Jamani samahini kwa kuwaweka sana"
"Hakuna shida ni jukumu letu hilo"
"Bwana nimezungumza na mabinti wangu. Mmoja amekubali ila mmoja amekataa"
"Sawa, hata buyo mmoja anatutosha kwa maana tunatana kusimamisha mrembo ambaye ataliletea sifa jiji letu la Tanga na mkoa mzima"
"Sawa na hao wengine mulio wapitisha mashindano vipi nao?" Eddy sliuliza
"Ahaass hao gelesha tuu, kwani mshindi halisi sisi tunaye ambaye atakuwa ni mwanao"
"Ahaaaa sawa, ila jamani hala hala na mwanangu, kwenye hayo mashindano yenu ninasikia kuna mambo ya kifuska, sinto jisikia vizuri siku mwanangu atakapo fanyiwa upuuzi bado ni mwanafunzi huyo"
"Hilo mkuu wala usiwe na shaka nalo nwanao yupo katika mikono salama kabisa"
"Nyinyi semeni hivyo siku nije kusikia ujinga nitawachinja"
Eddy alizungumza kwa kujiamini, huku akiwatazama machoni wazee hao, walio anza kutazanana wenyewe kwa wenyewe kwani wanamfahamu Eddy ni miongoni mwa matajiri wakubwa mkoani Tanga pamoja na nchini Tanzania.
"Mimi kama mkurugenzi wa mashindano hayo wala sinto kuangusha muheshimiwa mbunge mtarajiwa"
Hawakuwa na lakuzungumza zaidi ya kuaga na kuondoka zao.
***
Kuingia kwa Xaviena siku ya kwanza katika kambi ya warembo, iliyopo katika hoteli ya kitalii Tanga beach reasort, ikaanza kuzuka woga kwa baadhi ya warembo wengine walio ingia katika kambi hiyo siku mbili za nyuma. Uzuri wa Xaviena, umechangiwa na urefu wake, wa futi sita na nchi kadha. Rangi ya chocolate isiyo kolea sana, inazidi kuufanya uzuri wake kuzidi kuongezeka mara dufu.
Sifa zake za uzuri wake ukizilinganisha na warembo wengine waliopo katika kambi hii, ni sawa sawa kulilinganisha ardhi na mbingu, kwani hakuna mrembo anaye mfikia hata kwa asilimia kumi.
"Habari zenu?"
Xaviena akawasalimia warembo wezake wapatao ishirini na tatu, baadhi walimuitilia salamu yake ila wengine wakabaki wakiibenua midomo yao kwa dharau iliyo jaa wivu ndani yake
"Jamani huyu ni mwenzenu atajumuika nasi katika kipindi chote cha kukaa hapa kambini"
Mlezi wao(matroni) alizungumza, akimtambulisha Xaviena mbele yao
"Kwa jina anaitwa Xaviena Eddy, ninaomba tumpe ushirikiano wetu"
"Sawa matroni"
Kutokana ni jioni, warembo wote ukawa ni muda wa wao kuzunguka maeneo mbali mbali ya Hoteli, kuzipumzisha akili zao kwa ajili ya siku inayo fwata.
"Jamani mimi kuna kitu kinaniumiza kichwa"
Msichana mmoja alizungumza akiwa amesimama katilati ya kundi la wezake wapatao wanne
"Jambo gani hilo?"
"Hivi huyu demu aliye kuja ametokea wapi kwa maana hapa sisi kila mmoja ameingia akitokea kwenye kitongoji chake ila huyu mwenzetu hatujui jatoka wapi?"
"Shosti nilidhani ni mimi peke yangu niliye dhani hilo"
"Hawa ndio wale wanao chochomekwa, sasa huyu dawa yake nimesha ijua"
"Unata kumfanya nini?"
"Ngoja usiku ufike nitawaonyesha cha kumfanya. Atajuta kuja hapa atanitambua kwamba ni Asha binti Adalah kutoka Pangani"
Muda wa kulala ukawadia warembo wote akiwemo Xaviena wakaingia katika vyumba vyao vya kupumzikia, na kila chumba kina vitanda viwili vinavyo laliwana na warembo wawili wawili. Kutokana Xaviena amechelewa kuingi kambini ikamlazimu kulala chumba cha kwake peke yake. Mipango ya Asha na wezake katika kutafuta chokocho dhidi ya Xaviena ikakwama kwa usiku huu wa leo, wani hawakutambua ni wapi alipi lala Xaviena.
***
Siku ziku zidi kwenda, warembo wakiendelea kupewa mafunzo mbalimbali kwenye kambi yao, huku kila mmoja akizidi kujijengea matumaini moyoni mwake kwamba anaweza kunyakua taji hilo la urembo wa mkoa wa Tanga. Kitu kilicho washangaza baadhi ya wa rembo akiwemo Asha, ni jinsi ya Xaviena alivyo jaliwa kutambua mambo mengi juu ya urembo. Uwezo wake wa kuyatambua mambo mengi mara kadhaa, ilimzimu mwalimu wao kumuachia darasa Xaviena ili awafundishe wezake. Ukweli ni kwamba baadhi ya washiriki wakaanza kumpatia ushindi Xaviena hata kabla ya mashindano. Ila ipo tofauti kwa Asha na kundi lake la watu watano, ambao wamejipa jina la Team KISHKWAMBI, wakionyesha kuzipeleka nguvu zao zote kwa Asha, ambaye kwa upande wake anajivunia kuwa na asili ya bara la Asia japo amezaliwa Tanzania na kukulia Tanzania.
"Asha, unakosea kitu kimoja unapo takiwa kutembea usiiachie mikono kama imevunjika, kidogo unatakiwa kuikaza ili...."
Asha hakumpa nafasi Xaviena kuimalizia sentensi yake, akaachia msunyo mkali ulio wafanya wezake wote kukaa kimya wakimtaza kusubiria atazungumza kitu gani.
"Kwanza unanifundisha wewe kama nani?"
"No, mwalimi si ameniachia darasa ni jukumu langu kukuelekeza kama mshiriki mwenzangu"
"Heeee makubwa, wewe ni wakunielekaza mimi?"
Asha alizungum huku akimpandisha kwa macho makali Xaviena kuanzia juu hadi chini.
"Hembu jifananishe wewe mwenyewe. Hunahadhi ya kunifundisha mimi."
Asha aliendelea kumtolea maneno ya dharau Xaviena ambaye muda wote macho yake makubwa kiasi yana kazi ya kumtazama Asha jinsi anavyo jichetua mbele yake.
"Basi nisamehe mimi, ninakuomba ukakae kwenye kiti"
"Siendi kukaa"
Asha alizungumza huku mikono yake ikiwa imeshika kiuno chake chembaba kiasi.
"Asma mbona unakuwa mjeuri wewe, mwenzako si anakuambia uje huku kukaa"
Mrembo mmona alizungumza kwa sauti ya upole akimuomba Asha kurudi kukaa kwenhe viti walivyo kalia wao
"Babueee hayakuhusu na wewe, si uwaache wenyewe wamalizane"
Mmoja wa wapambe kwenye kundi la kishkwambi alizungumza kwa sauti ya ukali, iliyo mfanya mrembo aliye jaribu kufungua kinywa chake kukaa kimya asizungumze kitu cha aina yoyote.
"Wewe kunguni uiliye kosa kunyonya damu ya mbwa umekuja kunyonya damu ya binadamu leo utanitambua."
Asha alizungumza huku akimsukuma Xaviena aliye pepesuka kidogo, na kuanguka chini. Bila ya kupoteza muda, Asha akamrukia Xaviena. Akamkalia tumboni na kuanza kumtandika vibao mfululizo vya mashavuni. Warembo walio upande wa Xaviena hawakusita kunyanyuka kwenye viti vyao na kuwatenganisha Xaviena na Asha. Machozi ya uchungu yakaanza kumtiririka Xaviena usoni mwake, kwani hadi sasa hivi hatambui ni sababu gani inayo mfanya Asha pamoja na kundi lake kumchukia sana.
Xaviena hakuona haja ya kuendelea kukaa katika fukwe ya bahari wanapo fanyia mazoezi kila asubuhi na jiono. Kwa mwendo wa haraka huku akijiziba sura yake inayo endelea kutiririkwa na machozi akondoka eneo hilo.
Gafla akastukia mkono wake ukishikwa kwa pembeni, akamtazama mtu aliye mshika mkono
"Unalia nini wewe?"
Sauti ya Xaviela ilizungumza, huku akimtazama mdogo wake Xaviena
"Hapana"
"Hapana nini wakati unalia?"
Xaviela alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo, akiendelea kumtazama Xaviena aliye chafuka mwili mzima kwa micha aliyo mwagiwa na Asha. Siku zote za maisha yao Xaviela hapend kumuona pacha wake huyu akionewa na mtu wa aina yoyote, na endapo itatokea hivyo nilazima afanye kitu chochote dhidi ya kuumupa furaha mdogo wake.
"Sema nani kakupiga?"
Xaviela alizungumza huku akiyageuza geuza mashavu ya Xaviena, yaliyo jichora alama za vidole
"Ni yule dada aliye vaa kibukta cheupe na sidiria nyekundu"
"Ahaaa twende"
Xaviela akamshika mkono Xaviena, wakelekea katika eneo walipo warembo wengine, kila aliye muona Xaviela na Xaviena akabaki akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana. Kwani wana fanana sana na wote ni warembo kuliko hata wao.
"Wewe nguruwe ndio uliye mpiga mdogo wangu?"
Xaviela alizungumza huku akifyatua teke kali lililo ichota kiguu yote ya Asha na kumuangusha chini kama gunia. Xaviela akamshika Asha nywele zake, akamnyanyua juu, hadi akasimama wima kama mlingoti.
"Wewe unamjua huyo ni nani?"
Xàviela alizungumza hukua akiendelea kuzishikilia nywele za Asha. Rafiki mmoja wa Asha akajaribu kumshika Xaviela mkono wake wa kulia ili asiendelee kumshika mkuu wao. Ngumi nzito ikatua kwenye pua ya msichana huyo na kumfanya mrembo huyo kutoa ukelele mkali wa maumivu ulio ambatana na matone ya damu yaliyo anza kumchuruzika puani mwake. Xaviela akamtandika kichwa kizito Asha, akimsindikiza na kofi zito lililo muangusha Asha chini kwa mara ya pili.
"Sikiliza wewe mpumbavu, usirudie ziku nyingune kumgusa mdogo wangu, hii ni mboni ya jicho langu akilia yeye ni sawa sawa nimeli mimi, siku ukirudia kufanya ulicho mfanyia, nitakuua."
Xaviela alizungumza huku akiwa amemuinamia Asma, anaye ona mawenge mawenge kwenye macho yake kwani kichwa hicho kimekata network zote za kujitambua kichwani mwake.
"Kama kuna mtu kati yenu alikuwà anajidanganya kumdhururu mdogu wangu, atambue atadili na mimi kwa marefu, twende zetu Xaviena."
Xaviela akaanza kuondoka na Xaviena akifwatia kwa nyuma. Wakawaacha warembo wakinong'onezana kwani hawakutamba kwamba Xaviena ana pacha mwenzake ambaye ni mkorofi kupita maelezo. Wapambe wa Asha walio salia wakawa na kazi ya kuwainua wezao walio jeruhiwa kwa kipigo hicho.
"Matroni akija lazima niseme"
Asha alizungumza huku akiendelea kulia, jambo lililo wafanya warembo wengine kuanza kumcheka kwa dharua.
"Heeee hee leo timu Kishkwambi, kwisha habari yake, chezea pacha wewe"
Mrembo mmoja alizungumza huku akicheka kicheko kilicho wakasirisha Asha na timu yake nzima.
ITAENDELEA


Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

 

  🔞Wakubwa tu: video kali zote na original app download chini
TAHADHARI WAKUBWA PEKEE NDIO WANARUHUSIWA KUBONYEZA HII LINK WATOTO KAA PEMBENI



No comments:

Powered by Blogger.