SIMULIZI MPYA: TANGA RAHA 17 & 18




ILIPOISHIA
‘Olvia utalipa kwa haya yote yanayo tokewa kwenye familia yangu’
Xaviela alizungumza huku akimtazama mama yake aliye alala huku hajitambui kabisa. Xaviena akaka uwanja huo wa ndege hadi ilipo ondoka na kupotea kabisa kwenye uwepo wa macho yake. Gafla Xaviena akastuka mara baada ya kuguswa begani mwake. Akageuka nyuma kwa haraka, hakuamini kumuona Olvia Hitler eneo hilo, tena akiwa na baba yake na wote wawili wana tabasamu kwa kejeli.
ENDELEA
“Shikamoo baba”
Xaviena alisasalimia kwa heshima pasipo kujali tofauti iliyo sababishwa na Olvia Hitler katika familia yake.
“Marahaba”
“Shikamoo Olvia”
“Ahaa huyu kwa sasa ni mama yako. Hivyo una paswa kumpa heshima ya umama”
Eddy alizungumza na kumfanya Xaviena kustuka kidogo, kile alicho kuwa akikisikia leo hii ndio baba yake amekidhihirisha kabisa kwake.
“Sawa shikamoo mama”
“Marahaba Xaviena. Pole sana kwa kupata shida ya kila jambo lililo mkuta mama yenu”
“Nashukuru”
“Okay na sisi tumekuja hapa na ndege ya asubuhi. Saa nane tuna ondoka kueleka Dubai kwa fungate la ndoa yetu”
Eddy alizungumza huku akimuonyesha Xaviena pete ya ndoa walio funga na Olvia Hitler.
“Hongereni”
Xaviena alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Kitu anacho kifanya baba yake hakika ni udhalilishaji wa familia yao. Kwenye kipindi chote cha maisha yao, hakuwahi kumuona baba yake akiwa katika hali ya ajabu kama hii. Amekuwa ni mu asiye jali, mtu asiye tilia maanani usalama wa familia yake.
“Xaviena kwa nini tusiende wote?”
Olvia alizungumza huku akimkazia macho Xaviena usoni mwake. Machozi yakamchuruzika Xaviena na kujikuta akijifuta na kujikaza kusimama na watu hao wawili ambao hakika wana uchafua sana moyo wake.
“Ahahaa mama si una kumbuka kwamba nina wadhamini wanahitaji kufanya kazi na mimi hivyo sinto weza kuondoka nanyi”
“Ohoo ni kweli mwanangu sikukumbuka. Basi ubaki salama na nikienda huko nita kuhakikishia kwamba nina kutafutia wana mitindo wakubwa sana, ili uingie kwenye mitindo na uzidi kutengeneza pesa”
Olvia Hitler alizungumza huku akimsogelea kwa ukaribu sana Xaviena.
“Natambua ni kipindi kigumu una pitia kuhusiana na mama. Ila jikaze ni muda wa wewe kusimama na baada ya wiki mbili tutarudi Tanzania”
“Sawa”
“Nikuletee zawadi gani mwanangu?”
Swali la Eddy likamfanya Xaviena kuzudi kukasirika kwani haonyeshi hata majuto ya kumsababishia mama yake matatizo ya kichwa.
“Chochote baba. Ninaomba niweze kuondoka kwa maana kwa sasa nina hitaji kuelekea kwenye ofisi za Cocacola hapa Dar hivyo niwatakie safari njema”
“Sawa Xaviena”
Olvia Hitler akambusu Xaviena kwenye paji lake la uso kisha Xaviena akaondoka eneo hilo. Akatoka nje ya uwanja wa ndege, akaingia kwenye gari maalumu alilo tumiwa na mkurugenzi wa Cocacola. Xaviena akaanza kuangua kilio huku akijilamu ni kwa nini mama yake alikubaki kuolewa na mwanaume kama Eddy.
‘Hana hata utu jamani. Hajui mama ana ishi vipi, hajui tuna kula nini. Ehee Mungu nisimamie kwenye hili nahisi kushindwa sasa’
Xaviena alizungungumza kimoyo moyo huku akiendelea kulia kwa uchungu sana hadi dereva anaye muendesha akapatwa na mshangao. Wakafika katika ofisi za Cocacola na akapokelewa na mkurugenzi wa kampuni hiyo pamoja na mkurugenzi wa mashindano ya miss Tanga. Ujio wake katika ofisi hiyo, kila mtu aliye muona akatamani kupiga naye picha. Kila mtu akakiri kwamba Xaviena ni mzuri na uzuri wake ni wa kipekee sana.
Xaviena akakabidhiwa Script ya matangazo mawili atakayo kwenda kuyacheza na matangazo hayo yatatumika dunia kote inapo patikana sada ya Cocacola.
***
‘Hakuna haja ya kumdhuru Xaviena
Olvia Hitler alizungumza mara ya kukaa kwenye siti ya ndege wanayo safiri nayo kueleka Dubai.
“Mbona una onekana una mawazo mke wangu?”
“Hapana mume wangu nipo sawa tu’
“Hapana mimi nina kujua, niambi tatizo ni nini?”
“Namuonea huruma Xaviena kwa sasa ame baki yeye mwenyewe”
“Usijali amesha kua. Nimekuwa nikimfundisha ujasiri kipindi chote nilipo kuwa naye. Nina imani kwamba ata fanyia kazi mafunzo yote niliyo mfundisha”
“Sawa mume wangu. Ila nina hofia sana watoto wako kunichuki”
“Hilo usijali, kwani mimi ndio mtu pekee mwenye maamuzi yangu kwenye kila kitu ninacho kifanya hivyo acha nile maisha mama”
Eddy alizungumza kwa furaha huku akimtazama Olvia Hitler. Ndege ikaacha ardhi ya jiji la Dar es Salaama na kuianza safari rasmi.
***
Xaviela na mama yake pamoja na madaktari wakafika nchini India. Wakapokelewa uwanja wa ndege na gari maalumu la wagonjwa lililo tokea katika hospitali waliyo tafutiwa na madaktari wa nchini Tanzania. Hapakuwa na muda wa kupoteza, moja kwa moja wakapelekewa katika hospitali hiyo na madaktari walio toka nchini Tanzania, wakasaini fomu ya makabidiano ya Raham kisha wao wakaelekea hotelini na kumuacha Xaviela hospitalini.
Rahma akapelekewa kwenye chumba cha upasuaji na upasuaji ukaanza upya huku makosa kadhaa yaliyo fwanya na madokta wa kitanzania yakiwekwa sawa.
“Sawa uwezekano wa mama yako kupona ni asilimia mia moja”
Dokta Rajah alizugumza na Xaviena mara baada ya kumaliza upasuaji huo.
“Kweli?”
“Ndio, tuna uhakika na pia tatizo lake sio kubwa kivile kama vile mulivyo elezwa na kuna makosa kadhaa yalifanyika katika upasuaji, ila hali yake itakuwa salama”
“Ohoo asane Mungu je akili yake itarudi kama kawaida?”
“Ndio akili yake itarudi kama kawaida. Kikubwa hakikisheni kwamba akirudi kwenye hali yake ya kawaida hapati msongamano mkubwa wa mawazo. Kwani hali hiyo inaweza kuepelea kichwa chake kumuuma sana”
“Sawa sawa daktari nimekuelewa. Ninaomba niulize swali tofauti na hili tulilo zungumzia”
“Uliza”
“Umejuaje kiswahili, ikiwa wewe ni Muhindi?”
“Hahaa unajua sifa moja wapo ya kuajiriwa kwenye hii hospitali nilazima ufahamu lugha si chini ya sita. Hivyo katika kusoka kwangu pia nimesha soma kiswahili na nilikuwa nina kipenda sana.”
“Ahaa sawa sawa”
“Mama yako ni muarabu?”
“Ndio”
“Je una fahamu familia yake, labda wazazi wake?”
“Hapana sijawahi kufwatilia swala hilo. Alafu daktari nina sikia hapa Indi kuna waganga wazuri sana wanao weza kuagua na kumkinga mtu”
“Ndio wapo”
“Lini una weza kupata muda ukanipeleka kwa watu hao?”
“Hata muda huu kwa maana, nipo likizo na nilipigiwa simu kwamba kuna mgonjwa ana tarajia kufanyiwa upasuaji leo. Ikabidi nije na ninashukuru Mungu upasuaji umekwenda vizuri.”
“Mama yangu si hato zinduka sasa hivi?”
“Ndio”
“Basi twende”
Dokta Rajah na Xavielaa kwa muda mfupi wakajikuta wazioena kana kwamba ni watuw alio onana kw amuda mrefu sana. Wakaondoka hospitalini hapo na kuelekea kwa mganga anaye sifika sana nchini hapo India.
“Usiogope”
Dokta Rajah alimuambia Xaviela mara baada ya kukuta nyoka wengi aina ya cobra nyumbani kwa mganga hyyo.
“Kwa nini kuna nyoka wengi hivi?”
“Hao ni walinzi wa hiyo nyumba yake. Endapo utakuwa umekuja kwa lengo baya katika hii nyumba basi wana kuvamia na kuvung’ata na huyu nyoka sumu yake ni kali sana kwa maana akikung’ata una kufa hapo hapo”
“Aisee”
“Ndio”
Wakakaribishwa na vijakazi wamganga hao. Wakaombwa waweze kusubiria mtu aliye ndani amalize kutibiwa. Baada ya robo saa wakaruhusiwa kuingia ndani, Xaviela akajikuta akimshangaa mzee huyo mwenye ndevu nyingi pamoja na nywele nyingi zinazo gusa hadi chini huku nywele zake zikiwa na rangi nyeupe. Nyuma ya mzee huyo kuna joka kubwa na lina vichwa saba kiu kilicho mfanya Xaviela kuzidi kuogopa kwani kwenye maisha yake hajawahi kuona vitu hivyo. Mzee huyo akaanza kuzungumza huku akimtazama dokta Rajah.
“Mzee ana sema kwamba huyo unaye taka kupambana naye ni kiumbe hatari”
Dokta Rajah alimtafsiria Xaviela kitu ambacho amekizungumza mzee huyo.
“Muulize kiumbe gani?”
“Mzee ana sema kiumbe hicho kina itwa Olvia Hitler”
Xaviela akastuka huku akiwaza kwa nini mzee huyo ameamua kumuita Olvia Hitler kiumbe.
“Ana maanisha nini kusema Olvia Hitler ni kiumbe”
Xaviela aliuliza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.
Dokta Rajah akamsikiliza mzee huyo anacho zungumza kisha akamtazama Xaviela.
“Ana seme kwamba Olivia Hitler sio binadamu. Yeye ni jini tena jini mwenye nguvu kubwa na mamlaka hapa duniani na endapo utajaribu kushindana naye atakuangamiza mara moja. Na yeye hana uwezo wa kupambana na jini Olvia Hitler”
Xaviela akajikuta akipatwa na mstuko mkubwa sana kwani mama yake alisha wahi kukiri kwamba Olvia Hitler sio mtu bali ni jini ila kutokana upeo wao mdogo walibisha hususani yeye na alidiriki kwenda kumuuliza Olvia Hitler juu ya ualisia wake.



TANGA RAHA  18

“Anasema kwamba pia ujiepushe sana kuwa karibu sana na Olvia Hitler kwani ana uwezo wa kukutawanyisha katika muda mfupi sana. Ila amesema ana dawa anayo weza kukupatia ili uweze ujikinga na Olvia Hitler asiweze kukudhuru”
Dokta Rajah alizungumza huku akimtazama Xaviela anaye tetemeka mwili mzima kwa woga. Hapa ndipo akaanza kupata picha kwamba mambo yote yanayo fanywa na baba yake si akili zake halisi kwani katika kupindi chote cha wao kukua, baba yao amekuwa ni mtu akiwapenda sana kuliko hata anavyo jipenda yeye mwenyewe.
Mzee huyo akampatia Xaviela dawa hiyo ya kujikinga na Olvia Hitler huku akimuomba ajipake yeye na mama yake mara saba kwa siku saba katika nyuso zao, asubuhi na usiku. Xaviela baada ya kukabidhiwa dawa hiyo akatoa kiasi cha pesa, ila mzee huyo akamkatalia.
“Anasema kwamba ana wasaidia”
“Shukrani sana”
Xaviela alizungumza huku viganja vya mikono yake akiwa amevifumbata kwa pamoja. Xaviela na dokta Rajah wakaondoka eneo hilo na kurudi hospitalini huku Xaviela akiwa amejawa na mawazo mengi sana juu yake.
***
Upeo wake mkubwa wa kuelewa na kipaji chake cha kuigiza, ukamfanya Xaviena kupendwa sana na watengenezaji wa matangazo ya kampuni ya cocacola, kwani kila alicho andikiwa na kuelekezwa kufanya ndio hivyo jinsi alivyo tenda. Matangazo ya Xaviena yakamalizwa kutengeneza na yakabakia siku tu ya kuweze kuarushwa duniani kote kwa pamoja.
“Ahaa…hili ninalo hitaji kulizungumza ni la kuhusiana na filamu sijui utakuwa upo tayari kucheza filamu?”
Mtengenezaji mmoja maarufu wa filamu kutoka nchini Marekani ambaye naye amehusika katika kutengeneza tangazo hilo alizungumza huku akimtazama Xaviena.
“Ahaa ni filamu za aina gani ammbazo muna hitaji kuzitengeneza?”
“Filamu za mapigano. Unajua wewe jinsi ulivyo hivi na mwili wako tuna imani kwamba una weza kutengeneza soko kubwa sana katika soko la Hollywood.”
“Mmmm filamu za mapigano kwa kweli mimi siziwezi.”
“Kila kitu una fundishwa Xaviena, wala usiwe na shaka”
“Sawa kama ni hivyo hakuna shaka. Ila kuna filamu nitaicheza hapa karibuni kutoka na watengezaji huko huko Marekani. Nikimaliza kufanya filamu hiyo basi tutawasiliana”
“Sawa hakuna tatizo Xaviena nashukuru kwa ushirikiano wako”
“Hata wewe bwana nani vile”
“Tomas Minller”
“Ahaa sawa nashukuru kukufahamu bwana Minller”
Xaviana akaagana na muandaaji filamu huyo kisha jamaa huyo akaondoka na kumuacha peke yake katika hoteli hiyo waliyo fikizia katika kutengeneza matangazo ya filamu. Simu ya Xaviena ikaanza kuita, akaitazama kwa haraka, alipo ona ni namba ngeni kutoka nje ya nchi, akaipokea kwa haraka na kuiweka sikioni mwake.
“Haloo”
Xaviena alizungumza kwa shahuku kubwa sana ya kutaka kumfahamu ni nani ambaye ana zungumza naye.
“Xaviena”
Sauti ya unyonge ya Xaviela ika mstua sana kwani si kawaida ya dada yake huyo kuwa mnyonge.
“Bee niambie dada yangu. Kuna tatizo gani linalo endelea. Mama ana endeaje?”
“Aha mama ana endelea vizuri na madakatri wame nihakikishia kwamba kila jambo jambo lina kwenda kuwa sawa hivi karibuni”
“Ohoo asante Mungu. Vipi mbona una zungumza kwa unyonge una tatizo gani?”
“Leo nimetoka kwa mtaalamu”
“Mtaalamu!! Mtaalamu wa nini?”
“Mtaalamu wa kienyenji”
“Ohoo Xaviela ume kwenda kwa mganga”
Xaviena alizungumza kwa sauti ya chini ili watu walipo karibu naye wasiweze kusikia chochote kinacho endelea.
“Ndio. Xaviena yaani niliyo kwenda kukutana nayo huko hakika yana tisha. Yaani hadi sasa hivi nina wasiwasi mwingi sana. Sijui haka kama hii vita iliyopo mbele yetu tutaishinda”
Xaviela aliendelea kuzungumza kwa upole na unyonge sana hadi akazidi kumpa wasiwasi mwingi Xaviena anaye endelea kumsikiliza kwa umakini.
“Hembu niambie basi ni nini kinacho endelea”
“Baba haya yote anayo yafanya sio akili yake”
“Ndio naamini hilo baba kuna jambo lime mtokea. Kwa maana huyu sio yule baba yetu tuliye mzoea na hapa ninavyo kuambia kwa sasa wapo Dubai na Olvia Hitler wana kula maisha na wamesha funga ndoa.”
“Ohoo Mungu wangu”
“Ndio”
“Sasa nilipelekwa kwa huyo mganga na dokta mmoja hapa ana itwa dokta Rajah. Ana zungumza kiswahili fasaha japo yeye ni muhindi”
“Ehee ikawaje?”
“Yule mzee ameniambia kwamba Olvia Hitler sio binadamu bali ni jini”
“JINI!!!?”
Xaviena aliuliza huku akiwa amejawa na mstuko mkubwa sana hadi baadhi ya watu walioko karibu yake wakamtazama kwa mshangao. Xaviena akasimama na kundoka eneo hilo na kutafuta sehemu iliyo tulia ili kuendelea kumsikiliza dada yake.
“Ndio ni jini tena mwenye mamlaka makubwa sana hapa duniani. Ametuambia kwamba endapo tuta fanya jambo lolote la kumpinga basi ata tutawanyisha hapa duniani. Hapa ndio maana nahisi nimepata picha kwani haya yote anayo yafanya baba nina hisi ni kutokana na kutulinda sisi. Baba amejitoa maisha yake kwa ajili ya sisi”
Xaviela alizungumza hukua kilia na kumfanya Xaviena naye kuanza kumwagikwa na machozi. Hali hiyo hakika ni mbaya sana kwenye maisha ya familia yao. Kumpoteza kiongozi katika familia yao ni jambo kubwa na linalo yagarimu maisha yao siku hadi siku na ukizingatia ni mabinti wa miaka kumi na nane tu.
“Tutafanya nini dada”
Xaviena alizungumza huku akilia kwa uchungu sana.
“Sifahamu mdogo wangu. Hapa nina muomba Mungu arudi kwenye hali yake, nina imani kwa kupitia mama tuna weza kupata njia ya kufanya”
“Ohoo Mungu kwa nini haya mambo yanatokea hivi sasa”
“Ndio hivyo mdogo wangu yaani hapa nakosa hata raha”
“Nakuomba ulinde mama. Habari za Olivia na baba kwa sasa tuachane nazo. Tuna paswa kuishi maisha yetu hivi sasa pasipo kuangalia mambo mengine ambayo kwa namna moja yata tuumiza mimi na wewe dada. Sawa”
“Sawa nimekuelewa mdogo wangu”
“Unakaa hapo hospitalini au ume panga hoteli?”
“Hapa hapa hospitali, chumba cha mama kina tosha mimi kuishi hapo”
“Sawa dada yangu”
“Vipi wewe maswala yako”
“Yanakwenda safi. Tumemaliza kutengeza matangazo ya Cocacola na nimepata ofa moja ya kufanya filamu. Ila bado si rasmi”
“Mungu ni mwema mdogo wangu. Hakikisha una fanya kazi zako kwa ufasaha”
“Sawa dada”
“Nikutakie usiku mwema”
“Huko hivi sasa ni usiku?”
“Yaa tayari kiza kimesha tanda”
“Sawa nawe pia”
Xaviena akakata simu huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana, hata furaha ya kumaliza kufanya matangazo nayo ikatoweka huku akizidi kumfikiria Olvia Hitler aliye ambiwa kwamba ni jini tena mwenye mamlaka makubwa sana.
***
‘Lazima afe’
Olvia Hitler alizungumza huku akimfikiria mganga huyo wa kihindi ambaye ametoboa siri yake kwa mtoto wa Eddy. Olvia akamtazama Eddy anaye jifuta futa maji mwilini mwake kwa ajili ya kupanda kitandani kwa ajili ya kulala.
“Mume wangu mazingira ya hapa Dubai ume yaonaje?”
“Ni mazuri kwa kweli. Nimeyapenda.”
“Hakika mapumziko yetu ya ndoa yatakuwa yanakwenda fresh ehee?”
“Yaa fresh sana.”
Taratibu Eddy akapanda kitandani. Akamvuta Olvia Hitler aliye uchi kama alivyo zaliwa. Akashika ziwa lake la upande wa kushoto, kisha akaanza kulinyonya taratibu na kumfanya Olvia Hitler kupatwa na msisimko mkali sana wa kimapenzi.
“Nakupenda sana Eddy”
“Nakupenda sana Olvia wangu”
“Kweli?”
“Ndio”
Taratibu wakaanza kupeana utamu huku Olvia Hitler akizidi kupagawa kwa penzi analo patiwa na Eddy. Japo yeye ni jini ila ana penzi hilo hajawahi kulipata kwa mwanaume wa iana yoyote katika maisha yake yote ya ujini.
‘Nafanya hivi kwa ajili ya kuiweka familia yangu salama. Ila lazima nikuue tena’
Eddy aliwaza kimoyo moyo huku akiendelea kumbinua binua Olvia Hitler hapo kitandani. Kitu ambacho Olvia Hitler hawezi kukijua kwa Eddy ni kuweza kusoma mawazo ya mwamaume huyo ambaye hadi sasa hivi ana amani kwamba amemshika kimahaba.
‘Samahani sana Rahma mke wangu, sijapenda iwe hivi ila ninafanya haya kwa ajili ya wanangu. Sitaki kuwapoteza nyinyi nyote’
Eddy aliendelea kuwaza akilini mwake huku akiwa ametawaliwa na machungu mengi sana kwneye maisha yake. Kwani familia na furaha aliyo ijenga kwa miaka kumi na tisa hajapenda zipotee hivi hivi. Hadi wana maliza mtanange huo wote wawili wamechoka huku kila mmoja akiwa ana tokwa na jasho.
“Nakupenda sana Eddy hakika una niwezea”
“Kweli?”
“Ndio una niwezea yaani una nipa vitu ambavyo sijawahi kuvipata kwenye maisha yangu yote”
“Usijali mke wangu nitakupa utamu wote unao hitaji”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu vile.”
Olvia Hitler na Eddy wakaendelea kuzungumza mambo mengi huku wakipanga mambo mengi juu ya maisha yao ya baadaye. Taratibu usingizi ukaanza kumchukua Eddy ambaye amechoka sana. Olvia Hitler alipo hakikisha kwamba Eddy amelala, akashuka kitandani, akavaa gauni lake jekundu kisha akapotea ndani ya chumba hicho. Safari ya kutoka Dubai hadi India hayakumchukua muda mrefu sana kwani ni safari ya sekunde kadhaa. Olvia Hitler akatokea kwenye nyumba ya mganga ambaye Xaviela na dokta Rajah walikwenda masaa kadhaa yaliyo pita. Nyoka ambao wote wameizunguka nyumba hiyo kama walinzi, hawakua kizuizi cha Olvia Hitler kuingia ndani humo, kwani kwa kuwakausha kwa mto mkali unao toka mikononi mwake ukawafanya nyoka hao wote kufa. Olvia Hitler akaingia katika chumba cha mganga huyo na kukutana na joka kubwa la vichwa saba. Joka hilo kikaanza kushambuliana na Olvia Hitler ili kumlinda mganga huyo. Walinzi wapatao saba wa Olvia Hitler ambao nao ni majini, wakatokea katika chumba hicho na kuanza kupambana na joka jilo lenye nguvu sana. Olvia Hitler akamsogelea mganga huyo huko macho yake yakiwaka moto.
“Niambie ni dawa gani ambayo ume wapatia Xavila?”
Swali hilo la Xaviela likamfanya mganga huyo kukaa kimya huku akimtazama Olvia Hitler kwa macho ya ujasiri mkubwa sana. Mganga akashuhudia jinsi joka lake hilo likiuwawa kwa kukatwa katwa na walinzi wa Olvia Hitler. Mganga huyo akapiga mayowe makubwa sana yanayo ambatana na uchungu wa joka lake kuuwawa. Ila mayowe hayo hayakumzuia Olvia Hitler kunyanyua kwa mkono mmoja huku akiiminya shingo yake na akizidi kumuuliza ni dawa gani alivyo mpatia Xaviela kwani dawa hiyo itamfanya Olvia Hitler kushindwa kumuua Rahma kwani ndio kinga itakayo muweka salama Rahma.
ITAENDELEA


Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

 

  🔞Wakubwa tu: video kali zote na original app download chini
TAHADHARI WAKUBWA PEKEE NDIO WANARUHUSIWA KUBONYEZA HII LINK WATOTO KAA PEMBENI



No comments:

Powered by Blogger.